Kuoa mwanamke aliyekuzidi kipato/elimu ni changamoto kubwa sana

Analyse

JF-Expert Member
Jan 19, 2014
6,860
2,000
Trust me on this. Ukitaka kujua mwanamke ni jeuri/kiburi basi awe kakuzidi elimu au kipato. Na akikuzidi vyote hapo lazima uisome namba.

Leo tulienda kumtembelea jamaa ambaye tulisomaga nae kipindi hicho (recently alipatwa na msiba). Fika kwake,tulikaribishwa vizuri tu. Agiziwa vinywaji,story za hapa na pale zikaanza.

Tulivyofika tuliwakuta sebleni akiwaa na mkewe na watoto wanaangalia movie ya Kikorea. Tulipoingia wakapause kutukaribisha. Baada ya utambulisho watoto wote na msaidizi wa kazi waliondoka sebleni,baadae kidogo na shem (mke wa jamaa nae akatoka) so tukabaki wanaume tu tunatwanga story.

Baadae jamaa akaona ngoja a turn kwenye king'amuzi (dstv) tuangalie mechi ya Arsenal. Kutokana na device nyingi kuwa connected,ilibidi achomoe deki ili kuunga king'amuzi. Kabla hajachomoa akatokea msaidizi wa kazi akasema "Baba,Mama amesema eti deki usiizime"

Jamaa akatoka kwenda kuongea nae kujua kulikoni. Sikujua waliongea nini huko walipokuwa,ila wakati natokea wash room nilimsikia mwanamke akisema "Mshahara wako wenyewe hautoshi hata kulipia kodi ya nyumba,ndio utaweza kutoa na ya king'amuzi au hizo unit 28 za luku ulizonunua ndio zinakupa jeuri"

Nilifedheheka as if nimeambiwa mimi yale maneno. Me nikarudi zangu sebleni as if sijaskia chochote.

Jamaa alivyorudi anasema rimoti ya deki imeharibika,tukiizima hapa itawapa tabu kujua walipoanzia,so sijui itakuwaje.

"Tuendeleze story" ndio jibu tulilotoa.
 

Analyse

JF-Expert Member
Jan 19, 2014
6,860
2,000
Kuna nguvu nyuma yake inampa hicho kiburi c degree wala kipato tu amini hivyo wanawake wachepukaji maofisini n hatari
Ofcourse ni kweli mwanamke mchepukaji anakiburi,ila huyu nadhan kipato ndio chanzo cha kiburi chake.
 

Sir_Mimi

JF-Expert Member
Jun 21, 2013
6,662
2,000
Bro....maisha aisee,kuna kausemi fulani maarufu sana mitaani japo kakiwa kanasemwa ktk hali ya kawaida huonekana sio ka maana sana ila in reality kana maana kubwa sana nako ni "kosea kujenga nyumba usikosee kuowa",unawezakuta jamaa kabla hajamuowa huyo mwanamke kuna baadhi ya tabia zake mbaya alikuwa ameshaziona ila akajipa imani kwamba atabadilika mbele kwa mbele na wengi ndo wanavyofanya.hili jambo ni hatari sana maana mwanaume unaweza kufa hata siku sio zako kutokana na unakuwa na msononeko ndani ya nafsi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom