Kuoa binti mwenye mtoto

unajua mkuu nyoka ukimtoa porini ukaishi nae ipo siku atakumbuka porini kwake kumbuka huyo kashazalishwa!!!!!!!!
 
Wako wanaume wengi wanaoa wanawake ambao tayari wana mtoto/watoto na ndoa zao kuwa nzuri tu. Mwanamke kuwa na mtoto si sababu muafaka ya njemba kutoamua kufunga naye pingu za maisha.

unajua mkuu nyoka ukimtoa porini ukaishi nae ipo siku atakumbuka porini kwake kumbuka huyo kashazalishwa!!!!!!!!
 
Naendelea kunufaika na ushauri wenu wadau....
 
kwa jamii kubwa ni fedheha na wewe unahisi hivyo ndo maana umekuja kuuliza. Kama mnapendana (kupendana tu haitoshi) na mnaendana vya kutosha kuoana, mtoto ni mojawapo ya swala muhimu la kujadili kabla hamjaingia kwenye ndoa. Kufunga ndoa na mwenzi mwenye mtoto kunaweza kusiwe na shida endapo kutakuwa na mipaka ya mahusiano kati ya mwenzi na mzazi mwenzie. Ni lazima mkubaliane protokali toka mwanzo na mwenzi mwenye mtoto ahakikishe anazingatia.

Umesema baba mwenye mtoto hajihusishi kabisa na huyu mtoto. Kama hajihusishi huwa ni rahisi, lakini utashangaa akiskia mzazi mwenzie ana mchumba anajitokeza na kuanza kuleta fujo za hapa na pale, ikiwa ni pamoja na kujaribu kumsihi mama mtoto amrudie yeye, na mama mtoto akikataa basi atatishia kumtaka mwanae. Hapa linakuwa ni jukumu la mama mtoto kuonyesha msimamo na kumuwekea mipaka huyu mwanaume. Huyo mwanamke akionyesha kuyumba hapa basi itakula kwako.

Sasa hili linalofuata halihusiani na ubaya au wema wa kuoa mwanamke mwenye mtoto. Linahusu huo uamuzi wako wa kuoa. Ni nini hasa kinachokufanya utuambie lengo lako ni huu mwaka usiishe uoe? Ni masharti ya mganga au? Kijana hakuna umri sahihi au mbovu wa kuoa. Kuna wakati sahihi au mbovu wa kuoa. Huyo msichana unayetaka kumuoa kabla huu mwaka haujaisha unamfahamu kiasi gani zaidi ya ule upendo wa sekondari? Ni lini mmekuwa marafiki kiasi cha kuona sasa huu urafiki wetu umeiva kiasi cha kuashiria kuingia hatua nyingine? Binti huenda anaharakisha umuoe kwa kuwa anaujua unyanyapaa wa hii jamii. Anahisi akikukosa wewe uliyeonyesha nia anajua atasubiri sana kuolewa na mtu mwingine. Wewe je una haraka gani? Kwamba utamkosa huyu?

Halafu ndo kwanza umeanza kazi, uko mwaka wa kwanza chuo..................in short slow down bro. Iwe unataka kumuoa huyu au unataka tu mwaka usiishe hujaoa, slow down. Bado miezi mitano mwaka uishe. Ni michache sana kufanya maamuzi na maandalizi. NI MTAZAMO TU
 
Hakuna shida kama atafanya maamuz huyu bint
Asijekuwa bado anajikumbushia kwa x wake

Haina shida unaweza kumuoa tu
 
mwezi wa 11 natimiza 27

lakini huo umri wako kwa maisha ya leo si unatosha kujifunza kupitia makosa ya wengine?

mimi nashindwa kukwambia ukweli maana waswahili wengi ni maadui wa ukweli.

ninachoweza tu kukwambia think twice and learn from other people mistake, ungekuwa mwanamke tungesema uko desperate sasa wewe wa kiume tena msomi, unajuwa maana ya mtoto wa kwanza?
 
Unamjua Binti wewe?. binti ni mwanamke lika la kuolewa. akisha zaa huyo anakuwa mwanamke, hatakama anamiaka mitano.
 
Nimekupata sana mkuu nakushukuru naamini it is a sincere advice thanks bro.
 
yaah its true i have to think twice na ndo maana nikaona nianze kuwashirikisha wadau humu wenye experience tofauti katika maisha. Thans.
 
nikiona changamoto kama hizi naogopa kumtundika binti kibendi nisawa na kuaribu future yake...wacha nisubili mpaka ndoa!
 
mkuu experience ya wazi inaonyesha wazazi hawaachani lazma watakumbukana na kufarijiana siku moja. Kama umeamua kuoa jiandae kisaikolojia kuukubali ukweli huo. Vinginevyo kumuoa sio mbaya.
 

tukushauri nini kama unataka tukushauri weka picha yake hapa
 
Nimesema jamii unaelewa lakini maana ya jamii? Wanaume chungu nzima katika jamii yetu wanaoa wanawake wenye watoto na kuwatunza vizuri kama watoto wao na ndoa zinakuwa hazina matatizo yoyote yale. Usimchuuze huyu aliyeomba ushauri hapa akamtema binti wanayependana naye akamtema kisa tu kwa kuwa huyo binti ana mtoto aliyempata kabla ya kukutana naye.

Sema wewe hau-reflect au hujaona wadau wengine wame-reflect tofauti na wewe?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…