Kuoa bila sherehe, mtazamo wako.

Kuoa bila sherehe, mtazamo wako.

yani me nishatoa tangazo la la siku 21 pale bomani ,bado siku nane..naenda kufunga ndoa kimya kimya na mashahidi ...naenda kwetu kwa wazaz wangu,tunapata chakula na wakwe na rafiki zetu wachache...siku inayofuata me na wife zenjiiiiii...tukirudi likizo ya week 2 zimeisha mke job me job...kwisha habari yake....life goos on!,
 
yani me nishatoa tangazo la la siku 21 pale bomani ,bado siku nane..naenda kufunga ndoa kimya kimya na mashahidi ...naenda kwetu kwa wazaz wangu,tunapata chakula na wakwe na rafiki zetu wachache...siku inayofuata me na wife zenjiiiiii...tukirudi likizo ya week 2 zimeisha mke job me job...kwisha habari yake....life goos on!,

Hongera sana kaka
Mungu na awatangulie ndoa yenu iwe ya furaha na upendo
 
Kwa sasa ndoa nyingi nikutaka kujionyesha tu kwa jamii inayokuzunguka, sherehe kuuubwa, mbwembwe kibaao, siku mbili tatu wiki ndoa chaali:
Hii ni sawa na kusema ni
"Ndoa za sherehe."
Sherehe zikiisha na Ndoa kwishaaaaaa
 
Si kila mtazamo unaokuwa nao ni sahihi kuutumia, unaweza ukawa na mtazamo ambao si mbaya ukiutekeleza lakini hapohapo uwezo wa kuutekeleza hauna. Watu wengi michango ya harusi huwa hawatoi kwa moyo mmoja kuwa kwamba tunamchangia ndugu/jirani/rafiki/jamaa yetu ili afanye sherehe baada ya ndoa. Wengi huchangia kuondoa lawama kuwa nitaonekanaje nisipomchangia jamaa.

Na huku wafunga ndoa wengine hugeuza mchango kama deni na kero, mtu unakuta amekupatia kadi kwenye kukumbushia mchango anakutumia texts za kukukumbushia mchango mara 3 kwa siku zote zikidai mchango. Wengine hufikia hata kukulaumu na kukusema vibaya kisa tuu hujachangia harusi yake.

Mtu unakuta ana plan ya kufunga harusi ya million 15, lakini yeye yupo tayari kuchangia pesa isiyozidi laki 5 ili kufanikisha na kutegemea michango kiasi kilichobaki. Sidhani kama hili ni sahihi.
nakuelewa unachosema n i agree,mi nilichokua nasema wafanye sherehe kwa uwezo wao kama wana hela ndogo wawe wabunifu sherehe ndogo ila nzuri au kama dada aana uwezo, ila wasiache kufanya sherehe
 
Ndoa bila sherehe za mbwembwe na michango michango au vikao vya harusi mimi naona ndiyo mpango mzima.........

ila sasa hao wabongo ( ndugu , jamaa na marafiki) watakusemaje kuwa unaringa na mchoyo mpaka uone maisha machungu aseeee......

siyo hilo tu , hata Big wedding ni dream ya almost all women ( sijasema wote)
 
Mfanyakzi wa halmashauri wa mji flani alioa around 43 age mchango wa harussi alipata more than 69milioni kamati ilimpa 30milioni cash,na tena mfanyakazi mwingine akaozesha binti yake kwenye ofice hiyo2 akapata mchango wa more than 95miloni yule binti alipewa kazawadi ka gari ya 15m


ofisi gani hiyo mkuu ? tukachangishe na sisi hiyo michango tupige bingo hapa mjini.
 
Kuoa uoe wewe kugegeda ugegede wewe michango tutoe sie majanga mbona majanga!!
~kuoa kwa sherehe kubwa kwa kutegemea michango ni sawa na kufuga mbwa halafu unategemea nnya ya walevi au kupanda matembele kutegemea walevi wamwagilie kwa mikojo yao! Kama msuli mdogo usitanue upaja.
 
Wakae tu chini wafikie muafaka, na kila moja aridhike, watu wengine tunapenda sherehe kweli.
 
Thats the way it should be.

Sio matarumbeta mara gari ya uwazi thats old school.
 
Kuoa uoe wewe, mie nitoe hela ili ufanye sherehe! Ili iweje, je mke ni wa kwako ama wa kwetu?
 
Bora huyo bw. harusi mtaraijwa ameona mbali, tumechoka kuchangia sherehe za harusi, michango yenyewe mtaji wa biashara kabisa, mbaya zaidi ndoa nyingi zenye bajeti ya mamilioni hazidumu

Mwambie rafiki yako, sherehe sio lazima, yeye afunge ndoa aendelee na maisha au nanataka kuwafurahisha na kuonekana kwa watu kuwa na yeye kaolewa?
 
mimi mtu akinijia eti anaomba hela iliafanye sherehe yakumpata mwenza simpi bora nikatoe sadaka khaa ishakua kero mtu unajikuta una madeni lukuki ukijiuliza chanzo eti nikufanikisha sherehe za watu sasa hivi watu watakaa sana na kadi zao za michango
 
Mi nilioa bila sherehe na mwaka wa tatu huu sasa nadunda na wife. Watu wanataka makubwa kwa kutegemea KUKAMUA watu. Pesa nyingi hupotea kwenye sherehe alafu maharusi wanasuffer baada ya ndoa.

Baada ya sherehe ni majanga. Kuna jamaa mmoja ana bifu na shangazi yake kisa hela za zawadi alizozawadiwa siku ya harusi.
Ilikuwa hivi:
Mshikaji mchaga ana kabiashara kake kariakoo akaamua aoe kwa sherehe...........kaitisha vikao watu wakaahidi kama kawa. Mpaka siku ya mwisho michango iko robo ya bajeti. Jamaa akaamua avunje kibubu, lkn wapiiiiiiiiii, mwishowe akaishia kuchota mtaji. Asante Mungu sherehe ikafanyika, sasa siku ya harusi si kuna watu wanatoa zawadi za pesa! mpokeaji shangazi mtu, baada ya harusi katokomea na hizo pesa. Jamaa anasubiri aletewe hiyo zawadi kumbe ilishaliwa long time. Baada ya harusi maisha magumu, hana hata hera ya kujikimu.............hasira zote zikaishia kwa shangazi. Mpaka leo hii hawaongei na huyo shangazi
 
Mi nilioa bila sherehe na mwaka wa tatu huu sasa nadunda na wife. Watu wanataka makubwa kwa kutegemea KUKAMUA watu. Pesa nyingi hupotea kwenye sherehe alafu maharusi wanasuffer baada ya ndoa.

Umeonaeee! Kuna familia zimekreeemu! Kila ndoa ya mwanafamilia shengesha kibao, afu awana kitu, ukikataa kutoa wanakuona m'baya.... Aagh! Hadi shida! Zanzibar inaongoza kwa kukrem, hasa hasa ndoa ya kwanza, mh! Utachoka mwenyewe!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom