ACADEMIA TODAY
Senior Member
- Jun 7, 2013
- 179
- 86
- Thread starter
- #21
umeona eehh kongosho
Kwani mkipika Pilau lenu nyumbani bila kualika wasio wahusika sio sherehe?
Kwani mkipika Pilau lenu nyumbani bila kualika wasio wahusika sio sherehe?
Binafsi sikubaliani na dhana ya kuchangishana fedha kwa ajili ya harusi..na kama tusipolisemea hili sasa...kesho tu watu watakuja kuomba wachangiwe na mahari kabisa...Tatizo kubwa letu watz ni kuwa huwa tunapenda sana show offs...kusema ni rahisi but kutekeleza naona ndio mzigo....tubadilike bana!...i wish ningekuwa kijana nionyeshe mfano....
Mshauri hivi, afanye bonge la send-off la kufa mtu yeye mwenyewe maana send-off iko upande wake huyo rafiki yako. Kwa upande wa huyo mumewe mtarajiwa, amruhusu ajifanyie kisherehe kilicho ndani ya uwezo wake. Sioni mantiki ya kumlazimisha mtu kufanya misherehe mikubwa wakati hana uwezo au kama ulivyosema ni anti-social, atachangiwa na nani? Au ndo yale mnamaliza kufunga ndoa mnaishia kulipa madeni?
sio kutofautiana kiivyo mkuu....dah? Hawajaoana tayari weshaanza kutofautiana!
kuna harusi nilihudhuria ambayo gharama yake ilikuwa Tsh. 25mil lakini kiukweli ilikuwa haifanani na gharama hizo which means baadhi ya wajumbe wa kamati walichakachua michango.....Unanifaa sana wewe, hasara za kuwajaza watu waje kula na kunywa ni heri hiyo pesa nikutwange na ka GX 110.
Snowball umezungumza vyema
ni kautamaduni ambako hakafai
na kanadhalilisha sana
mtu anapanga kuoa kwa bajeti ya kuchangisha watu!!
ili tuu aonekane duniani ameoa!!!
i hate michango ya harusi
Bora tuanze kuchangia elimu kwa wasiojiweza.
Ndoa bila sherehe ina wezekana.
pole yao! wafanye sherehe inayomatch uwezo wao, sherehe kupendeza siyo ukubwa au gharama mnayotumia rather ubunifu na kinacho matter mwisho wa siku ni nyie wenyewe mme enjoy kias gani, au kama dada ana uwezo wagawane gharama za harusi, ila huyo kaka asimnyime dada wa watu sherehe.... jaman wafanye ya gharama ndogo as I said, ni dream ya most women kuwa na harusi nzuri, SO SHE SHOULD NOT BE DENIED THAT.
nipo na jamaa yangu hapa, yeye aliamua kutofanya sherehe kabisa, kilichotokea upande wa mwanamke wamevunja send off, na ile 12m walioikusanya kwa ajili ya send off itumike kwenye harusi, basi jamaa yupo hapa hajielewi elewi!
Kwani kusipokuwa na sherehe baada ya ndoa haitokuwa harusi nzuri.?
kama mtu ana mtazamo/anaamini kuwa lazima sherehe iwepo then haitakua nzuri definetly!
Upande wa mwanamke wamevunja sendoff kwa sababu gani.?
Hii ndiyo staili ya kisasa hata ulaya. Unakwenda kwa City mayor... mnafunga ndoa.... unatoka nje ya ukumbi... mnapiga picha mnakunywa vinywaji (cock tail)..... marafiki wanatoa zawadi ... mnatawanyika, maharusi wanakwenda honeymoon. Suala hapa si kuokoa resources in terms of money tu, bali in terms of time pia. Sherehe kubwa na mbwembwe siyo guarantee kwamba ndoa yenu itadumu. Tuzinduke.Suala sio kuwa social au anti-social suala ni resource, nilifunga ndoa na kulikua na sherehe lakini maumivu yanayobaki baada ya hapo ni mimi ninayejua. sema niliona mke wambae sio complicated, sasa imebaki story. Kuna kipindi wakati niko chuo pale Mlimani niliona watu siku ya jumatano I think walienda pale CCT kanisani wakafungishwa ndoa wakaondoka zao na mashahidi wao, mwengine ni classmate wangu,alifunga kimya kimya alipomaliza ndugu yake akawachukua wakaenda baharini wakatafuta mahali wakala wakanywa kiasi hao nduki...life goes on
tumebaki na maswali yasiyokuwa na majibu, ila ni kwamba huyo binti mtarajiwa ndo kaamua iwe hivyo, yaani badala ya kusanya sedoff yeye kaamua hiyo pesa itumike kwa ajili ya harusi, sasa upande wa mwanaume haukujiandaa na hilo, na upande wa mke unauliza pesa ya upande wa muoaji, ili ijumlishwe, na harusi ni wiki mbili zijazo