Kuoa au kuolewa ni muhimu sana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuoa au kuolewa ni muhimu sana

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by JOHN MADIBA, Jun 27, 2011.

 1. JOHN MADIBA

  JOHN MADIBA JF-Expert Member

  #1
  Jun 27, 2011
  Joined: Jan 30, 2011
  Messages: 251
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  NDOA ni shida tupu�sioni kama kuna umuhimu wa kuoa au kuolewa,� ndivyo wengi wanavyojisemea. Hayo ni mawazo ambayo wengi siku hizi wanayakuza.

  Ni kweli ndoa zina matatizo, kama yalivyo mambo mengine. Msingi wa ndoa nyingi kuwa mbaya ni kwa sababu wengi wanaanza vibaya.

  Nilikuwa nazungumza na jamaa mmoja Mwanza, akawa ananiambia ndugu yangu siku hizi kupata gesti ni kugumu zaidi kuliko kumpata msichana wa kufanya naye ngono. Unaweza kwenda gesti ukaambia hapa hatuna mambo yenu hayo ya �shoti taimu�, mara ooh imejaa, lakini wengi wanajirahisi.

  Kwanini wanajirahisi? Wengi wako kimaslahi zaidi, wako kibiashara zaidi. Wanategemea kuvuna, anajua ukienda naye, si rahisi usimpe hata nauli, soda, fedha ya mfukoni nk.

  Wapo pia wanaume wenye tabia hizi, anakuwa na msichana kwa sababu ya kutegemea atamhonga chochote kitu. Kuna wanaume wengine, bajeti ya nyumbani ni mke mwenye kufanya kila kitu.

  Wengine wanakuwa wepesi wa kuingia kwenye ngono kwa sababu ya pengine kuangalia au kufuatilia simulizi za mambo ya ngono nk. Hata hivyo lililo la msingi katika maisha ni kuwa na muda wa kuzungumza ili kuondoa tofauti, kila mtu anapaswa kuwajibika. Ni makosa makubwa kwa mfano mwanamume au mwanamke kujinunulia nguo za ndani.

  Mwambie mwenzi wako, kuanzia leo suala la nguo hizi za ndani ni lake, ikiwezekana mpe kipande cha gazeti asome. Hata kama mtu ataamua kujinunulia, bado mwenzi wake ndiye hasa mwenye kupaswa kumnunulia.

  Hii ni mojawapo ya faida ya kuoa au kuolewa, kwamba angalau unakuwa na mtu ambaye anawajibika juu ya mwili wako. Jambo jingine la msingi sana katika ndoa, ni makosa makubwa kunyimana.

  Nalizungumza hili mara nyingi kwa sababu ndilo linalosababisha wanaume kwa wanawake wengi kwenda nje ya ndoa. Maana kuna wengine ukimlazimisha sana anasema kwa hasira �haya njoo, au hutaki, nataka kuwahi kuandaa watoto bwana�. Ukweli ukiambiwa hivi, shauku yote inakwisha. Mapenzi yanahitaji mwenzi wako pia aonyeshe kuhitaji, si kufanya kama hivi.

  Iwe ni mtu maarufu, iwe ni mtu mwenye fedha, iwe ni mtu maskini au mtu wa hali yoyote, bado kuna faida kubwa ya kuoana. Mnapokuwa kwenye ndoa, iko heshima kutoka kwa jamii na pia ni jambo ambalo linakupa hadhi ya aina yake mbele ya Mungu.

  Unapaswa kufahamu kuwa kuna faida za kuoa mapema hasa ile kwamba mpangilia maisha�ndoa tamu bwana asikwambie mtu�raha uipate ukiwa kijana, nyumba ujenge ukiwa kijana, gari ununue ukiwa kijana, siyo hadi unakuwa babu.

  Faida ni kujenga maisha mapema, kujipanga vizuri na kujenga familia. Ni furaha unapokuwa na watoto ambao ni kama wadogo zako. Kuzaa ujanani ni raha zaidi kuliko ukizaa ukiwa na zaidi ya miaka 35.

  Pia usiogope kuoa mapema kwamba eti utapitwa na mambo ya ujana si kweli, mambo ya kujinafasi bado yapo, yalikuwepo na yataendelea kuwepo na yanakuwa ni ya kiutu uzima zaidi, ni ya staha na heshima mbele, fujo fujo hakuna. Pia kuna tafiti za kisayansi zinaonyesha watu wanaopata watoto wakiwa na zaidi ya umri wa miaka 35, wanapata watoto wenye akili ndogo �IQ� (intelligence quotient).

  Wenye hoja za kutokuwa na mpango kabisa wa kuoa, wana matatizo ya kisaokolojia na wanapaswa kuachana na fikra hizo mbaya kwamba kuoana ni kubaya. Na ukizoea sana kuishi kisela au kubadili wanaume au wanawake kama nguo, mwishowe unakuwa huwezi tena kutulia, na ndio hao ambao baadhi yao wamekuwa wakiona hakuna haja tena ya kuoana.

  Kuna wanaoogopa kuoa au kuolewa wakiamini ni jela fulani hivi, kumbe hilo si kweli, ukweli ni kwamba ukiwa kwenye uhusiano na mkaelewana vizuri, mafanikio huwa makubwa sana katika ndoa au uhusiano huo.

  Katika maisha pia kuna suala la nyota, kwamba wapo watu ambao ukiwa nao ni kama kujitia mikosi, kuna mwingine ukiwa naye tu, unashangaa mambo yanakwenda safi, ni suala la kutafakari kwa makini suala la kuwa na mwenza ambaye ni wa kudumu na ambaye anatambulika kisheria na mbele ya Mungu.
   
 2. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #2
  Jun 27, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  Mmmmhhh
  Kwa kweli
  Kuna sehemu nyingi za kukujubu na kuuliza..
  Ila mie naomba niongelee ya nguo za ndani
  Naomba fikiria kidogo majukumu na matatizo ya hapa nyumbani..
  Sijui Ada imepelea, watakiwa uweke chakula
  Mezani, huku watakiwa kutuma fedha kudogo kijijini.. etc..
  Hivi kweli utamwambi mumeo ni jukumu
  Lako kuni nunulia "chupi". Kwa hiyo binafsi
  Sikubaliani nawe hapo uliposema
  " ni makosa makubwa mwanamke/mwanaume kujinunulia nguo za ndani " .
  Naomba uangalie kwa maisha ya hapa mkuu.
  Kama ni huko Western countries labda..
  Na wale wa TZ wawili watatu walioendelea.
  Lakini kwa asilimia kubwa chupi ni kitu
  Kifikiriwacho baada ya mboga za watoto..
   
 3. Rose1980

  Rose1980 JF-Expert Member

  #3
  Jun 27, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 5,701
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  trueeeeeeeeeeeeeee!!!!!!


  lakin naona umebase zaid kwa wadada..et ni rahisi ngumu kupata gest lakin ni rahisi sana kupata msichana...

  si kweli
  acha kutusi watu
  si wasichana wote wapo ivi

  wat if nkisema wanaume wa kuoa siku izi hawapo cz wote ni MASHOGA?....yeeeeeeeeeees nkitumia kigezo tu cha shoga mmoja basi nikaconclude wanaume wote mashoga?

  km wasichana wako ni ao wa usiku so mpk gest znajaa bas ni hao na si wasichana wote ni wakununuliwa/kupenda mali/wa kupewa soda na kukubali...


  the rest is good umeongea fresh.

  nawasilisha.
   
 4. K

  Kiduku JF-Expert Member

  #4
  Jun 27, 2011
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 480
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hapo penye umri imekaaje?

  sisi wenye 40yrs na bado yupotupo inakuaje?
   
Loading...