UZUSHI Kunyanyua vyuma kunaweza kuleta dalili za mapema za kukoma hedhi

Baada ya tathmini, tumebaini kuwa taarifa hii ni ya uzushi
Kukoma hedhi ni wakati ambapo mzunguko wa hedhi wa mwanamke hukata. Ki kawaida hutokea mwanamke anapokaribia umri wa miaka hamsini.

Wakati hedhi inapokaribia kukata, wanawake hupitia dalili mbalimbali kama mzunguko wa hedhi usio wa kawaida, matatizo ya kihisia na ya kimwili ambayo hawajawahi kuyapata.
360_F_608240326_T11mUR6snvmOWkGxM6ICZXbBAX4xYefF.jpg

Mwanamke akinyanyua vyuma vizito (Chanzo: Adobe Stock)
Kuna nadharia kwamba wanawake wanaofanya mazoezi ya kutunisha misuli na kunyanyua vyuma vizito vinaweza kusababisha mwanamke kufika (menopause) mapema kabla ya umri wake. Umri wa mwanamke kufikia kikomo cha hedhi ni umri wa 50.
 
Tunachokijua
Hedhi ni tendo la kiasili na kibaiolojia linalotokea kwa mwanamke aliyevunja ungo. Tendo hili hutokea kila mwezi likiambatana na mabadiliko makubwa ya kihisia.

Huuandaa mwili ili ujauzito uweze kutungwa, na ikiwa mwezi husika yai la mwanamke halitarutubishwa na mbegu ya mwanaume, ukuta wa mji wa uzazi hubomoka na kutolewa nje kama hedhi.

Umri wa ukomo wa Hedhi
Hedhi haidumu milele. Baadhi ya wanawake hukoma wakifikia umri wa miaka 50, lakini wengine huendelea hadi wakiwa na miaka 60.

Hata hivyo, kwa mujibu wa Taasisi za Mayo Clinic na Cleveland Clinic, umri wa wastani wa kufikia ukomo wa hedhi ni miaka 51.

Hata hivyo, utafiti mwingine wa mwaka 2011 unabainisha kuwa wanawake wengi kwenye nchi za maendeleo makubwa ya viwanda hufikia ukomo wa hedhi wakiwa na umri wa kati ya miaka 50-52.

Mchango wa Mazoezi katika kufikia Mapema ukomo wa Hedhi
Kuna nadharia kwamba wanawake wanaofanya mazoezi ya kutunisha misuli na kunyanyua vyuma vizito vinaweza kusababisha kufika (menopause) mapema kabla ya umri sahihi. Mdau aliyeanzisha mada hii ni mmojawapo wa watu waliosikia ikisemwa.

Kwa mujibu wa tafiti za sasa, unyanyuaji wa vyuma hauwezi kusababisha mwanamke afikie kipindi cha ukomo wa hedhi mapema.

Hata hivyo, utafiti uliochapishwa katika jarida la Tiba ya Uzazi la Binadamu, moja ya majarida ya tiba ya uzazi yanayoongoza duniani, umechambua data kutoka kwa wanawake 107,275, ambao walifuatiliwa kwa uangalifu tangu walipojiunga na Utafiti wa Afya ya Wauguzi mwaka 1989 hadi 2011, na hakukupatikana uhusiano wowote kati ya shughuli za kimwili katika umri wowote na kukoma mapema kwa hedhi.

Dkt. Elizabeth Bertone-Johnson, Profesa wa Epidemiolojia katika Chuo Kikuu cha Massachusetts, USA, ambaye aliongoza utafiti huo, alisema utafiti wao unatoa taarifa kubwa katika kusaidia kuelewa uhusiano kati ya shughuli anazofanya mwanamke na muda wa kuingia umomo wa hedhi ambapo majibu ya utafiti huu pamoja na tafiti nyingine yanatoa ushahidi wa kutosha kwamba shughuli za kimwili hazina uhusiano na kuwahi au kuchelewa kufikia umri wa ukomo wa hedhi.

Badala yake, mazoezi husaidia kupunguza ukubwa wa dalili zinaoambatana na kufikia umri wa ukomo wa hedhi.

JamiiCheck yazungumza na Wataalamu
JamiiCheck imefanya jitihada za kuwasiliana na wataalamu wa Afya ambapo ilimpata Bingwa wa Masuala ya Uzazi wa Wanawake, Dkt. Fatma Ahmed aliyesema jambo hilo halina ukweli isipokuwa mwanamke anaweza kupatwa na Pelvic Organ Prolapse, yaani kushuka kwa baadhi ya viungo vilivyopo kwenye nyonga kuelekea ukeni.

Kwa mujibu wa tafiti, unyanyuaji wa vyuma vizito huongeza mgandamizo wa misuli na tishu zinazoshikilia viungo vilivyohifadhiwa kwenye sehemu ya sakafu ya nyonga hivyo kuongeza hatari ya kupatwa na tatizo la Pelvic Organ Prolapse.

Takriban 50% ya wanawake wote kwenye kipindi fulani cha maisha yao hupatwa na changamoto hii.
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom