Kunyang'anywa kwa kadi ya NHIF na Mwajiri

Rusumo one

JF-Expert Member
Oct 4, 2018
3,079
3,610
Habari za mchana wandugu? Nina shida moja wakuu nina mjomba wangu amestaafu utumishi wa Umma mnamo mwezi wa 4, 2023.

Baada ya kustaafu mnamo mwezi huu 7,2023 tarehe za mwanzoni ameitwa na Meneja wake na kutakiwa kuwasilisha kadi za NHIF ambazo alipewa akiwa kazini. Naomba kufahamu utaratibu upoje kwa mstaafu akimaliza utumishi je ni halali kunyang'anywa kwa kadi hizo ili hali bado anasubiri mafao yake?

Na ninakumbuka kuwa huduma ya NHIF kwa mstaafu na mwenza wake ilikuwa ni life time till their death sasa sijui iwapo kuna mabadiliko yoyote kwa miaka 2 hii au laa.

Naomba kuwasilisha.
 
Je amechangia zaidi ya miaka kumi? Kama jibu ni ndio hapaswi kunyang'anywa anaziliwasilisha NHIF atasajiliwa kama mstaafu yeye na mwenzawake. Ila kadi za wategemezi zenyewe zitakoma baada ya mtumishi kustaafu, hizo ndo zinatakiwa kurejeshwa
Ndiyo mkuu toka 2011 hadi sasa na baada ya kunyan'anywa hajapewa utaratibu wowote akiumwa anatumia cash yaani ni kutesana sasa na kutotambua utaratibu anaona Sawa. Asante mkuu kwa ufafanuzi mzuri
 
Back
Top Bottom