kununua vitu kutoka amazon.com | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

kununua vitu kutoka amazon.com

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Makenya, Apr 15, 2011.

 1. Makenya

  Makenya Member

  #1
  Apr 15, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  jamani kuna wabongo ambao wananunua vitu kutoka amazon.com.? naomba experience zao..mmi nasita kdgo coz sijawahi kununua vitu online
   
 2. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #2
  Apr 15, 2011
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,953
  Likes Received: 1,509
  Trophy Points: 280
  Kuna mtu hapa kwenye jukwa allisema ukiwa bongo haiwezekaniki ila wao wanaweza kukunulia na wanamwakilishi wao pale Haidary Plaza,wanakuharge kiasi fulani kwanza mnakubaliana halafu ndio wanakutumia hicho kitu nawe unampa hela huyo mwakilishi wao
   
 3. Kaka Sam

  Kaka Sam JF-Expert Member

  #3
  Apr 15, 2011
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 543
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  huyo mwakilishi wao yuko ofisi ipi?
  kiufupi mi nilitaka kununua PS3 lakini kwa kumtumia mtu aliyeko uingereza kisha aje nayo huku bongo, ila sijajua kama unataka kununua kitu kikubwa kama TV huyu mtu akifika hapa uwanja wa ndege hatatozwa kodi?? ...
   
 4. C

  Chief JF-Expert Member

  #4
  Apr 17, 2011
  Joined: Jun 5, 2006
  Messages: 1,490
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Inawezekana kabisa. Inabidi uwe na debit card ya Visa/Mastercard ambayo imekuwa activated kufanya online transactions. Kodi kutozwa ni lazima:)
   
 5. Msarendo

  Msarendo JF-Expert Member

  #5
  Apr 17, 2011
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 9,155
  Likes Received: 3,353
  Trophy Points: 280
  Sidhani kama bongo wanaweza ku deliver.
   
 6. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #6
  Apr 18, 2011
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,225
  Likes Received: 2,091
  Trophy Points: 280
  Hata mie wasiwasi wangu kwa bongo ni devlivery!
  Posta ni wazembe sana, labda kama utawatumia DHL, hawa huenda wakafikisha mzigo ukiwa katika good order.
   
 7. S

  Soki JF-Expert Member

  #7
  Apr 18, 2011
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 1,308
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Unaweza kabisa kununua vitu online ukiwa Tanzania. Uwe na kadi iliyowezehswa kama ya CRDB nk then unanunua. Tatizo ni shipping! Yaani kukituma hicho kitu toka huko nje hadi kwako! Ila kama gharama ya shipping siyo tatizo you can buy. Nenda na kadi yako ya CRDB uwajulishe utajaza form maalum then utaweza kununua vitu online
   
 8. S

  Soki JF-Expert Member

  #8
  Apr 18, 2011
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 1,308
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  LAkini DHL nighali sana. Posta ukiwekea mizigo yako insurance inafika salama kabisa hadi kwenye sanduku lako la Posta! Nimewahi kufanya hivyo siyo maramoja!
   
 9. S

  Soki JF-Expert Member

  #9
  Apr 18, 2011
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 1,308
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Mkuu una namba za hao jamaa za simu unipatie? Mizigo yangu itakuwa na security yoyote?
   
 10. S

  Soki JF-Expert Member

  #10
  Apr 18, 2011
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 1,308
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Nakushauri kama una mtu huko bora akununulie yeye na aje nao utaokoa gharama kubwa sana!
   
 11. Makenya

  Makenya Member

  #11
  Apr 18, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  okay bro pale, haidary plaza office gani mkuu?
   
 12. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #12
  Apr 19, 2011
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 8,253
  Likes Received: 4,276
  Trophy Points: 280
  Mkuu,

  Njia pekee kwa sasa ni kuwasiliana na mtu ambae yupo Marekani au Ulaya na atakununulia kitu chochote kutoka amazon iwe ni kule Amazon.com ya Marekani au Amazon.co.uk na akutumie huko Tanzania kwa kutumia DHL.

  Itabidi muelewane kwenye suala la pesa na wewe utakuwa unafidia gharama za huyo mtu kukutumia mzigo wako.

  Tatizo ni shipping kama alivyosema mmoja wa wachangiaji lakini unaweza kupata mzigo wako ikiwa tu utatumwa kupitia DHL.

  Mimi ni mwanachama wa muda mrefu wa amazon na nimekuwa sipati tatizo kutuma mizigo Tanzania sema tu gharama za DHL ni za juu sana ila ukituma mizigo mikubwa huwa inapungua.

  Pia unaweza kutumia kadi yenye nembo ya VISA ya CRDB endapo tu ukiwa utakuwa na anuani ya uhakika na post code inayoeleweka na watu wa amazon wakatambua hilo maana Afrika mpaka sasa hawajawahi kutuma mizigo!
   
 13. Kaka Sam

  Kaka Sam JF-Expert Member

  #13
  Apr 19, 2011
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 543
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Senks kwa maelezo yako, lakini nataka kujua kuhusu kodi, endapo mzigo utatumwa kupitia DHL je utatakiwa kulipia kodi? na je hiyo kodi unalipa mzigo ukifika au wakati wakuorder unalipia kodi kabisa TRA? mwenye idea plz
   
 14. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #14
  Apr 20, 2011
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 8,253
  Likes Received: 4,276
  Trophy Points: 280
  Nafikiri DHL kwa kukutoza pesa ya kukuletea mzigo wako wanakuwa wamekwishakukutoza kodi kabisa kwani mzigo wako wanakutelea kwenye anuani yako.
   
 15. R

  Rwiai Member

  #15
  May 14, 2011
  Joined: Jul 17, 2009
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  hapa Tanzania ipo Online Shopping gateway ambao wanauza products za kila aina of high quality genuine products. mimi nimenunua kwao computer, Tv (Led Series), home theatre nk. wasiliana kwa anuani hii: Tanzania Online Shopping gateway
   
 16. BobKinguti

  BobKinguti JF-Expert Member

  #16
  May 14, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 222
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Online purchases inawezekana ikiwa tu unayo debit visa/master card ambayo itakuwa imewezeshwa, kama ambavyo wadau kadhaa walivyosema. Tatizo ambalo lipo hapa kwetu ni delivery! Nakumbuka wakati fulani nilijaribu kufanya online purchase from amazon.com, baada ya ku-submit order, walijibu hawawezi kudeliver hicho kifaa nchini kwangu(Tanzania). Sikufuatilia zaidi kujua kwanini. Kwakweli njia ya uhakika na salama ni ya kumtumia mtu unayemjua.

  Nimeshaagiza zaidi ya mara moja laptop toka US kwa kumtumia shemeji yangu mmoja aishie huko. Na zote nilizipata hapa hapa nilipo(Morogoro) kupitia posta. Alinipa website ya kampuni ya huko U.S.A aliyotumia kusafirisha mzigo pamoja na serial number ambazo alipewa na hiyo kampuni. Hii serial number inakuwezesha kupata information through the website given, mzigo uko wapi na lini utaingia destination port. Kwa ufupi unakuwa na uwezo wa kufuatilia jinsi mzigo wako unavyosafiri.
   
Loading...