Kununua gari au kujenga nyumba

Kununua gari au kujenga nyumba

KIDOLEGUMBA

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2013
Posts
498
Reaction score
110
Habari wadau, Nina rafiki yangu wa siku nyingi alinifuata hivi karibuni kuniomba ushauri, yeye ameoa na wamebahatika kupata watoto wawili, kwa sasa anaishi nyumba ya kupanga. Ameniambia yeye na mkewe wapo katika malumbano ya kuhusu kipi waanze kukifanya kati ya kununua gari ama kununua kiwanja na kuanza ujenzi!! Kipato chao kwa mwez jumla huwa kati ya sh lak 8 hadi mil 1 na lak 2. sijui ndugu zangu mngewashauri waanze na ujenzi au gari?
 
Jamani kuwa na usafiri sio anasa, ukiwa na Gari itakusaidia sana kwenye supervision ya ujenzi Wako. Ukiiba kapesa kidogo kazini unapitia duka la ujenzi faster unaweka kwenye Gari yako huyooooo moja kwa moja kwenye site yako. ILA sielewi Kwanini watu wana misconceptions Hii ya kuwa na Gari. Huu ni mtazamo binafsi
 
Kwa kipato hicho ni bora watafute kiwanja waanze ujenzi...

Kuwa na gari ni kweli sio anasa lakini matunzo ya gari ni makubwa na mwisho wa siku wanaweza wakajikuta wanaishia kwenye nyumba za kupanga...

Ushauri wangu utabadilika kama kuna vyanzo vingine vya mapato zaidi ya hivyo ulivyotaja...
 
Kuna zile basic needs 3
1.chakula
2.malazi
3.mavazi
kwa dunia ya sasa mi napendekeza waongeze
4.usafiri, kwa 7bu dunia inakimbia, muda hautoshag kila siku, thr4 ili urahisishe mambo mengi ya kifamilia, kijamii, kiuchumi, kikazi aisee huwez kukwepa gari! Gari kwanza.
 
Kwa kipato hicho ni bora watafute kiwanja waanze ujenzi...

Kuwa na gari ni kweli sio anasa lakini matunzo ya gari ni makubwa na mwisho wa siku wanaweza wakajikuta wanaishia kwenye nyumba za kupanga...

Ushauri wangu utabadilika kama kuna vyanzo vingine vya mapato zaidi ya hivyo ulivyotaja...

Mpwa wangu unajua Kwanini inatugharimu sana kuendesha magari? Kwasababu wengi tunanunua magari ambayo yameshacboka sana kiasi kwamba maintenance costs zake zinakua kubwa sana. Mimi natumia Duet kwasababu ninachohitaji ni usafiri tu kwa maana ya usafiri na sio show-off najikuta siumii kuiendesha na Kila service yake hunigharimu 45;000 au 50;000. Tatizo ni kwamba tunanunua magari makubwa ambayo huwa shida sana kuyaendesha......
 
Kuna baba mwenye nyumba,hakuna baba mwenye gari,bora waanze ujenzi aisee,gari kuhudumia yenyewe ni kazi wanaweza kununua gari na wasijenge kabisaaaa coz gari yataka matunzo!na mwisho wa cku wakajikuta wanaipaki hata hyo gari!
 
Mpwa wangu unajua Kwanini inatugharimu sana kuendesha magari? Kwasababu wengi tunanunua magari ambayo yameshacboka sana kiasi kwamba maintenance costs zake zinakua kubwa sana. Mimi natumia Duet kwasababu ninachohitaji ni usafiri tu kwa maana ya usafiri na sio show-off najikuta siumii kuiendesha na Kila service yake hunigharimu 45;000 au 50;000. Tatizo ni kwamba tunanunua magari makubwa ambayo huwa shida sana kuyaendesha......

Halafu nyymba ina cost zaidi ya 20m lakini gari hata 7m unapata.
 
Ushauri Muhimu kabisa waanze na Nyumba kwa sababu:
1/Nyumba ni mali isiyohamishika hivyo ni dhamana muhimu mahali popote pale duniani iwe Mahakamani, Benki, Biashara, Maishani, Kazini nk.

2/Thamani ya Nyumba inakwenda inaongezeka kila siku(Hata siku wakitaka kuiuza wataiuza kwa thamani kubwa zaidi).

3/Watakuwa wameondoa gharama za kupanga na usumbufu wake(Watakuwa huru sana)

4/Nyumba ni Akiba ya kudumu maishani(Wataishi wao na vizazi vyao)

5/Nyumba ni kipimo cha Heshima, Hekima, Busara na Upeo kijamii, kifamilia, kimila, kiserikali nk.

6/Nyumba ni Mtaji wa Maisha(Hawatatoa tena pesa zao kila siku au kila Mwezi kulipia gharama za kuishi kwenye hiyo nyumba zaidi wanaweza kupata kipato zaidi kama sehemu ya hiyo nyumba watapangisha)

7/Nyumba inaweza kuwaletea vitu vingine vingi kama Gari kama watafanya mahesabu vizuri(Kwa mfano wanaweza kuitumia kama dhamana katika taasisi za kipesa kukopa pesa za kununulia gari nk.)

NOTE;
Kwanini wasianze na Gari:
A/Gari inahitaji gharama kubwa sana kulihudumia(Kwa mfano Insurance, Kodi ya Mapato, Mafuta ya kila siku, Service ya kila mara, Parking ya kila siku, Trafiki, Vipuri nk)

B/Gari itakuzidishia gharama zaidi za maisha pasipo msingi.(Mfumo wako wa maisha unaweza ukabadilika ili kukidhi tu fahari ya kumiliki gari. eg.Kula, kuvaa, Makazi, matembezi, Marafiki, Ndugu, Jamaa nk.) Hili jambo nimeliona kwa watu wengi sana mijini. Kifupi Gari halipatani sana na mbana matumizi!!!

C/Thamani ya Gari mara nyingi inakwenda ikipungua tokea ile siku unalimiki.

D/Gari ni chombo kinachochakaa kwa upesi sana kadri siku zinavyokwenda au unavyolitumia(Mara nyingi magari mengi yanakuwa yameanza kuchakaa vibaya baada ya miaka mitatu tu!!)

E/Gari lina tabia ya kukugeuza kuwa Mtumwa wake(Kwa mfano Wakati wote litakuhitaji kutoa pesa zako mfukoni ili uweze kulitumia). Kifupi Gharama za Gari ziko juu zaidi wakati wa kulitumia kuliko hata wakati wa kulinunua!!
 
Wakinunua gari kwanza basi wajue kwamba wamracha kujenga. Gari siyo mhimu kama nyumba bana tusidanganyane. Utagundua hili pale mwenye nyumba wako anapoamua kukataa mkataba mwingine inapokubidi kutafuta nyumba nyingine kero na madalali. Ukiwa na nyumba hata kama ni ya aina gani unakuwa na anuani ya kudumu(permanent adress). Kumbuka pia majukumu yanaongezeka kwa kasi kuliko kipato kinavyongezeka. Ila kama unataka sifa gari ni mhimu sana kuliko makazi
 
Kwa hali ya dar usafiri muhimu saanaa....inakurahisishia mambo yako mengi mno..wanunue gari ya wastani tu ila pia kiwanja wanacho.?????..sio wanunue gari ht shamba la laki8 hawana...I dont regret having a car...ingawa nilianza nunua shamba/kiwanja kabla ya gari....
 
Halafu nyymba ina cost zaidi ya 20m lakini gari hata 7m unapata.

Hahahahaaaaa wanadhani milion Saba unajenga nyumba!!!!! Narudia tena ukinunua Gari kuukuu ujie gharama za uendeshaji zitakua kubwa....ukiwa na Gari that means unauwezo WA kujenga pia. Ni suala la priority na Sababu za kukufanya ununue gari
 
Mhh kwa Dar gari kwa kweli,kw family yao IST yawatosha,then nyumba,kwa kipato chao nyumba itacost muda mrefu kujenga..so in the end wataenjoy both nyumba yao na gari,kama mkoani ambapo shida za usafiri sio nyingi basi nyumba ianze
 
Hahahahaaaaa wanadhani milion Saba unajenga nyumba!!!!! Narudia tena ukinunua Gari kuukuu ujie gharama za uendeshaji zitakua kubwa....ukiwa na Gari that means unauwezo WA kujenga pia. Ni suala la priority na Sababu za kukufanya ununue gari

Nyumba inachukua mda na unaweza kuishia kwenye lenta tu.
 
Hapana nyumba huwezi kufananisha na gari, au huna baba mwenye nyumba? Anasumbua huyoooo. Kiwanja kila siku kinapanda bei, gari kila siku zinashuka bei. Mwambie kama anahela alete 20,000,000 nimpe kiwanja, kipo nje kidogo ya mji
 
Nyumba au gari inategemea na factors nyingi. gari ni liability because it takes from ur pocket. kiwanja na nyumba ni very coastful unless una hela yote kwa mara moja.
itategemea kwa sasa tatizo kubwa ni lipi. magari ya kawaida si ghali sana kwa hivi kama tatizo kubwa ni usafiri ni bora kununua gari kwanza maana si kweli kuwa ukinunua gari hutaweza kujenga tena kwani itategemea aina ya gari. lakini ukianza kujenga si rahisi kununua gari kabla ya kumaliza.
kwa kuhitimisa ni kuwa kama hela ya kujenga inaoisheleza basi bora kujenga maana thamani yake huongezeka. kama kujenga ni kwa kudunduliza ni bora ununue gari kama usafiri ni muhimu sana kwa sasa
 
kwa kipato cha laki 8 kwa mwezi ... kipi rahisi kununua kiwanja na kujenga nyumba au kununua gari...? thnnkers use ur brains plz we are not comparing the value here.... maybe which should start first.
 
tatizo siyo kununua gari. tatizo ni gharama za kila za ilo siku. usione uku America ,Asia, Europe na Arabs watu wana magari uku watu uwa awanunui gari kwa cash kama tz.

unalilipia taratibu. Nyumba ndio muhimu. Mnaoshauri gari baada ya miaka 8 hao wazazi wakifariki ilo gari litawasaidia nini watoto?

pia mjue kulingana na kipato chao wakianza gari ujenzi ndio bye bye. gari linaitaj mafuta. service etc.

angalien future nyie
 
Halafu nyymba ina cost zaidi ya 20m lakini gari hata 7m unapata.

anatakiwa alijaze mafuta kila anapotoka nalo kumbuka, halafu kuna hela ya parking kama anakaa nyumba isiyo na mahali pa kupaki gari hapo oandoa mambo ya maintanace maana sio kila mara.
 
Back
Top Bottom