Kundi la kigaidi la Islamic state lateka bandari muhimu Msumbiji

China hakuwahi kuwa na koloni Afrika
Wala hapigi atu za kimaendeleo kwa kutumia mtutu wa bunduki kupora mali!
Russia hakwenda kuibomoa Iraq wala Libya!!
Koloni la mmarekani Africa ni lipi?.

Nb: hayo uliyoyataja hapa its all about interests.. kila Nchi inapigania interests zake.

ndio maana rusia aliwai ivamia Afrighstan.
1969 marekani akaikoa China dhidi ya Urusi.

Nb: wizi wa mtutu unaouongelea hapa ni upi huo?.
ni kampuni gani inayojihusha na huo wizi?.
 
Bandari muhimu ya Mocimboa da Praia , ya Msumbiji yatekwa na wapiganaji wa ' kundi la IS ' Wanamgambo wanaotajwa kuwa na uhusiano na kundi la Islamic State wamekamata bandari yenye ulinzi mkali nchini Msumbiji baada ya mapigano ya siku kadhaa

Vyombo vya habari vya Msumbiji vimesema askari wa serikali waliokuwa katika mji wa kaskazini wa Mocimboa da Praia walikimbia, wengi wao wakiondoka kwa boti, baada ya wapiganaji wa kiislamu kuishambulia bandari ya mji huo. Mji huo uko karibu na kituo cha mradi wa gesi asilia wenye thamani ya dola za Kimarekani milioni 60m

Katika miezi ya hivi karibuni wapiganaji hao wamekuwa wakitwaa maeneo kadhaa ya miji ya kaskazini , na kuwafanya maelfu ya watu wa huko kukimbia makazi yao . Shambulizi la safari hii dhidi ya vikosi vya serikali ya Msumbiji , linaonekana kupangwa vizuri na washambuliaji . Mashambulizi katika jimbo la Kaskazini la Cabo Delgado yalianza tangu mwaka 2017 , lakini mwaka huu yameongezeka baada ya kundi linaloihusika la Ahlu Sunnah Wa - Jama, kutangaza utii kwa kundi la IS

View attachment 1535770

====
Pia soma
US: Kikundi kinachodhaminiwa na IS cha Msumbiji kisipodhibitiwa, uasi unaweza kuhamia Tanzania
nchi za SADC kazi ipo tusikubali wahuni km hawa watuchezee akili wanaturudisha nyuma sana..
ila kuna baadhi ya nchi ni very weak isee..
 
Mwafrika ni Mwanadamu anaepitia kipindi kigumu sana.
Mapigano yote ndani ya Bara hili la Afrika ni ya kutengenezwa na wazungu wakishirikiana na baadhi ya waafrika vibaraka.
Ni wakati sasa regional blocks Kama ECOWAS, EAC, SADC etc zichukue hizi changamoto na kuzifanyia kazi kwa nguvu.
Haya ya Msumbiji si ya kubeza. Angalia Kenya wanavyopata taabu na Al shababu, je sisi tutakuwa salama? Angalia Boko Haram wanavyosumbua west Africa. Hatuko salama.
Africa tuamke tunachezewa
 
Hakuna cha waislam wala nani, Hapa kuna resources zinatafutwa kwa nguvu ili zichimbwe kwa bei che au bure..kama mnakumbuka Central Africa Republic ambako waislam wako less than 5% kuna Kundi lilijiita anti Seleka wakawa wanapigana kutoka mpaka wa Chad kumuondoa aliekua rais François Bozize na walifanikiwa kumuondoa ,walikua wakidai kwamba wanahitaji an equal representation in all public sectors.

Wale watu media zilituaminisha kwamba ni wa Tuareg from the northern parts, lakin walikua wanajeshi wa nchi fulani waliokuwa kwenye kikosi cha UN Darfur na kamanda mkuu wa UN alikua kutoka nchi hiyo.

Wanajeshi hao walitafuta vibaraka wachache ambao watakua wasemaji wa Kundi hilo ila vitaa ilipiganwa na jeshi hilo mpaka nchi ikatekwa. Walikua wanapewa all financial support na marekani.
Mkuu haya uliyoandika hapa yana ukweli?...🙄🙄🙄...
 
Back
Top Bottom