Kila jambo lina wakati wake, mambo ya miaka ya 60 na 70 hayakuwa na nafasi na katika ulimwengu huu wa Mobile phone, satellite nk.
Wala mambo ya miaka ya 1930 na 1940 hayakufaa kabisa wakati wa miaka ya 1960 na 1970.
Tunasoma kwenye historia, tunajifunza kwenye historia ilikurekebisha makosa au mazuri yawakati ule kuboreshwa zaid na zaid sio kung'ang'ania yaliyovunda na kuoza yaani yamepitwa nawakati
Babu yako, babu yangu nawengine, walifungwa minyororo nakubeba chunvi na meno ya tembo, walijisikia sawa kabisa nawakiitwa waliitika ndiyo bwana mkubwa - Waarabu tunaambiwa walitobowa matumbo ya wenye mimba ilikuona mtoto amekaaje, wazungu kwenye mashamba ya mkonge, kahawa waliuwa watu na kuwatesa vibaya nk
Mwalim aliingia bungeni kwa sifa zifuatazo
1. Rais mstaafu
2. Mshauri mkuu wa serikali na viongozi, kwa maana ya uzoefu wake madarakan, weledi na umahili wake katika diplomasia nk
3. Mmmoja wa wazee wenyekukubalika kwa wakati huo
4. Baba wa taifa, heshima yake na nafasi yake katika kutetea na kuwezesha taifa la tanzania kusimama imara na umoja
Mwl Julius kambarage Nyerere hakuwa mnafiki wala hakusita kuusema ukweli aliouamini alikemea mengi hadharani
-Alimkemea John S malecela - dodoma
-Alimkemea mwinyi akiwa mbeya sikuku ya wafanyakazi
-Aliwakemea maasikofu na wachungaji Serikali haina dini watu wake wana dini
-Aliwakemea mashekhe - serikali haina dini watu wake wana dini
Alituasa kuhusu nyufa za umoja na mshikamano
a) Udini
b) Ukabila refer mnkara ......
c) Uzanzibar na uzanzibar refer ukishakula nyama ya mtu.......
d) Gap kati ya walionacho na wasio nacho
.
.
.
.
Ninaamini Nyerere angelikuwapo leo, viongozi kadhaa wa CCM wangetoshwa hadharan tena kupitia maredio na ma -television tungehabarishwa Maana hili la mahakama ya Kadhi ambalo nikuwachanganya raia waziwazi asingelifumbia macho kama wanavyofanya wanafiki Ally Hassan mwinyi na Benjamin Willium Mkapa.
Kifupi Mwalim alifanya vile kulingana na wakati, kumbuka mara nyingi alipozidiwa nakuelewa hoja zake zimepitwa na wakati alikubali hadharani mfano - Vyama vingi, -Kunatuka madarakani nk
80% walisema wanataka mfumo wa chama kimoja
20% walisema wanataka mfumo wa vyama vingi
Nyerere na wenzie waka opt kwenye 20%
Wasalaam.