ilovebrenda
Senior Member
- Jun 23, 2019
- 105
- 74
Watoto (walimu ajira mpya) wameripoti mwezi May, lakini mpaka leo, ni miezi miwili sasa hawajapewa pesa ya kujikim, achilia mbali mshahara ambao wengine hawakupata kabisa kwa baadhi ya H/shauri. Ila cha ajabu kuna H/shauri nyingine walishapewa hizo pesa(za kujikim), sasa je kwa nini wengine wakose? Na nini lengo la pesa ya kujikim, ni mtu imsaidie mara tu anaporipoti kazini kabla ya kupata mshahara, au apewe baadae akiwa keshateseka sana? Tunaomba mamlaka husika ifuatilie suala hili na watoto wapatiwe haki yao, kuna waliokosa mshahara iwasaidie, hata wale waliokopa walipe madeni ili waweze kuishi.