Mtukutu wa Nyaigela
JF-Expert Member
- Sep 4, 2018
- 6,560
- 11,117
kuna watu asilimia kubwa wana tabia za kijinga kama za kwako. unakopa halafu unatafuta visingizio vya kutokulipa. shilingi 19,997. unakimbi deniMwaka jana mwezi wa tatu nilipokuwa nafanya muamala wa M-Pesa nilijikuta nimekopa hela ya nyongeza kutoka SONGESHA ili kukamilisha muamala kwani nilipungukiwa na sikuwa na namna nyingine zaidi ya kukopa.
Nilizoea kukopa na kulipa kwa wakati, lakini baada ya kukopa tena mwezi wa tatu mwaka jana nilishindwa kulipa maana uchumi ulienda kinyume na uchumi wa nchi.
Niliamua kuzitekeleza huduma zote za mtandao wa Vodacom Tanzania ila laini ilibaki tu kuwa hewani, nilihamia mtandao wa Halotel.
Muda ukaendelea kuyoyoma dalili za kulipa deni zikawa hazionekani, SONGESHA wakaanza kudai deni lao. Kila siku nikawa natumiwa sms zaidi ya mara tatu kwa siku kukumbushwa kulipa. Moyoni nikawa najisemea hawa watakoma kunikopesha.
Mwaka ukaisha, ukaingia mwaka huu bado sijalipa deni.
Sasa kuanzia January mwaka huu, SONGESHA wameanza kunitaarifu kuwa wamenisamehe deni lao kwa mjibu wa sms hii
Habari, Makato ya SONGESHA kwenye Akaunti yako yameondolewa. Sasa utaweza kupokea na kuweka hela kwenye Akaunti yako bila kukatwa hela yoyote. Piga *150*00# ambayo wananitumia mara kwa mara.
Juzi niliweka 100 M-Pesa ili nione kama wataikata au la, hawakuikata. Lakini nina hofu huenda kwa sababu ni ndogo haiwezi kukidhi deni lao la Tsh 19,997/= ambalo wananidai.
Nikiangalia salio la deni la SONGESHA bado linaonekana, halijafutwa kama kweli wamenisamehe jinsi wanavyonijulisha.
Nikiangalia pia kiwango ninachoweza kukopa tena, kinaonekana ni buku moja tu ila wananiambia siwezi kukopeshwa kwa sababu bado sijalipa deni lililopita.
Nyie Vodacom Tanzania mimi ni mteja wenu mkongwe lakini hamuwezi kuniingiza kwenye 18 zenu kiboya hivi, acheni kujisumbua na sms zenu, deni lenu sijui nitawalipa lini.
unasababisha wenzio waonekane wahuni na wasiaminike
hii hulka wala siyo suala la uwezo
jamaa bogus sanaYaani Tsh 19,997 unashindwa kulipa?? Tukikukopeha milioni si utahama dunia uamie mars
Vodacom Tanzania