Kuna watu wakatili aisee; nilishuhudia mgeni rasmi akitoa zawadi ya mfuko wa pipi tu

NIMEONA

JF-Expert Member
Aug 4, 2019
3,865
5,684
Ni mwaka jana tu katika mahafali ya darasa la saba sehemu fulani niliyoalikwa na mkuu wa shule huyo ambaye ni rafiki yangu mzuri. Tumetulia mara mgeni rasmi kafika na suti yake kuuubwa. Yamefanyika yaliyofanyika hadi muda wa kukaribishwa yeye ukafika. Akaongea vizuri kwa kutoa rai murua kabisa huku hoja zilizoelekezwa kwake kwenye risala akizipotezea kimtindo (niligundua hilo).

Mara ikafika sehemu ya kutoa zawadi yake aliyokuja nayo; akamwita kiongozi wa wanafunzi wa darasa la saba na, kwa mshangao mkubwa, akamkabidhi mfuko wa pipi. Kwenye vyoooote muhimu (madaftari, peni n.k) mheshimiwa huyu ye akaona mfuko wa pipi ndo zawadi bora kwenye tukio hili....dah!!!

Aisee kuna watu wakatili sana, sikia tu.
 
Itakuwa alikurupuka, may be siku aliyoamka Kuka kwenye hafla/sherehe labda aliamka na hangover...
 
Mwenyekiti wa Yanga alipogawa zawadi ya biskuti wodini huku akitazama Camera picha zitokee vizuri
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom