Karibu sana tupate kuelimishana.. Hope utakuja the soonestKifo kwa baati mbaya wengi hawakijui kiundani. Kuna hatua tano za kufikia ukamilifu wa kifo, ukweli usiojulikana na pasipo kujua watu wengi wamekuwa wakizikwa wakiwa hai. kama hatua tano za kifo hazikukamilika matukio kama maiti kuamka na kutembea, kupiga chafya, kutingishika, kutoka jasho sana na mengine mengi hujitokeza na kuna uwezekano mtu mapigo ya moyo yakashuka, hawezi kufumbua macho wala kuongea walakutikisika lakini anasikia kila kitu mnachoongea . Sababu mojawapo inayofanya watu kudhani wamekufa ni woga wa kuangalia maiti, utaalamu au vifaa duni vya kupimia.
Asilimia kubwa ya watu wanaotajwa wamefufuliwa kwa njia yoyote ile (kama maombezi) wengi wao walikuwa hawajafa.
Nikipata muda nitakuja kufafanua hatua tano za kufa, na wanaofufuka wanafufukaje
[emoji102][emoji102][emoji102][emoji15][emoji23][emoji23][emoji23]Kuna siku nipo nje mchana na washikaji tunalamba kirikuu nipo nimemshika mbwa wangu ametulia. Akapita mshikaji anafanya kazi mochwari huwezi amini yule mbwa alimbwekea sanaa mshikaji yaani ikawa vurugu mechi, jamaa akacheka na kusema atakuwa ameninusa harufu ya kifo
Sent using Jamii Forums mobile app
Kifo kwa baati mbaya wengi hawakijui kiundani. Kuna hatua tano za kufikia ukamilifu wa kifo, ukweli usiojulikana na pasipo kujua watu wengi wamekuwa wakizikwa wakiwa hai. kama hatua tano za kifo hazikukamilika matukio kama maiti kuamka na kutembea, kupiga chafya, kutingishika, kutoka jasho sana na mengine mengi hujitokeza na kuna uwezekano mtu mapigo ya moyo yakashuka, hawezi kufumbua macho wala kuongea walakutikisika lakini anasikia kila kitu mnachoongea . Sababu mojawapo inayofanya watu kudhani wamekufa ni woga wa kuangalia maiti, utaalamu au vifaa duni vya kupimia.
Asilimia kubwa ya watu wanaotajwa wamefufuliwa kwa njia yoyote ile (kama maombezi) wengi wao walikuwa hawajafa.
Nikipata muda nitakuja kufafanua hatua tano za kufa, na wanaofufuka wanafufukaje
Kwa Mara nyingine tena nimejuta kufungua Uzi wako dah
Hahahahahaha yaan lazima tutishane tu dah[emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji848][emoji848][emoji848][emoji144][emoji144][emoji144][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
π³π³π³Mwaka 1999 tukiwa nchi fulani hapo bara Asia tukaitwa kuhudumu mahali, kazi yetu ilikuwa ni kumvisha vizuri marehemu tayari kwa heshima za mwisho aliyekufa kwa kupigwa risasi na majambazi na kuporwa pesa nyingi
Jamaa alikuwa maarufu na mwenye pesa hivyo ukumbi ulikuwa umefurika watu wanasubiri kuaga, tukaingia chumba maalum kwa huduma maalum ya kumuandaa jamaa! Dah kumcheki tu tukaona huyu sie kafa na hasira na maumivu hivyo uso na mwili vilikuwa vimekakamaa na alikuwa kama kajikunja
Tukajaribu kutumia mbinu zote tujuazo ili akae vema tumvalishe lakini ikashindikana tukaona anatuletea ujinga tukamletea ukauzu tukampa live kwamba hatujui hatumjui na tunafanya haya kwa ajili yake na watu wake hatulipwi chochote hivyo akiendelea kukomaa tutamvunjavunja viungo nguo ziingie!!! Mbona alilainika na tukamvisha fasta
Kipindi kile ukimwi unaua sana. Kuna njemba iliRIP wananchi wakapanga kuzika jioni. Wakati wa ibada ya kikatoliki padre akaimwagia maiti yale maji wanasema ya baraka.... kulaaleki maiti ikapiga chafya.... Nakumbuka Padre aliyekuwa anawapa watu faraja ndio aliongoza zile mbio za marathoni... Sijawahi ona riadha ya namna ile maana hata kilema alisahau magongo akaunga msafara wa marathoni...
Maiti inatisha acheni masihara. Sijui kwanini zinamheshimu mshana jr
ππππππ
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji116]