Kuna watu hawakustahili ndoa

Kuna watu hawakustahili ndoa

and 998 others

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2012
Posts
28,509
Reaction score
40,346
Baadhi ya Watu (bila kujali jinsia) kwa tabia zao hawakustahili kuolewa/kuoa.

1. Mtu ana-complain kila kitu hata kama ni cha maendeleo ya familia.

2. Anaweka vitu moyoni (hata kama uliomba msamaha na kujirekebisha) miaka na miaka. Siku akikumbuka utajuta kumjua.

Ndoa ni chuo cha kuvumiliana na msamaha.

Mola tupe busara kwenye ndoa hizi na wadada wa mwendokasi. Unaishi na mtu ana matusi utadhani hajafundishwa kwao.
 
Kuna watu hawakustahili kuandika post

1. Hawana mada ya kuandika
2. Hawaheshimu sheria na vituo vya uandishi
3. Kuandika yenyewe pia wavivu
 
Mungu tusaidie katika hili. Chungu tunaiona. Inafika wakat unajuta hata kwa nn ulimuoa mtu huyu

Mlikaa kwenye uhusiano muda gani na ulimuoa sababu ipi
Tatizo wengi wenu mnataka toto jeupeee shepu hilo mara shombeshombe masela wakupigie salute wakina asha ngedere wamewavumilia tangu chuo mnanuka vikwapa hata deodorant hamjui manawapiga chenga na kujirusha na wadada wa mjini madai watafutaji kumbe wadangaji
 
Inaonyesha umeumizwa sana hadi kuamua kuandika hapa ni vizuri kwa kuwa umetua mzigo ulokuwa nao moyon
Pole Sana ndo mambo ya ndoa hayo
 
Baadhi ya Watu (bila kujali jinsia) kwa tabia zao hawakustahili kuolewa/kuoa.
1. Mtu ana-complain kila kitu hata kama ni cha maendeleo ya familia. 2. Anaweka vitu moyoni (hata kama uliomba msamaha na kujirekebisha) miaka na miaka. Siku akikumbuka utajuta kumjua.
*Ndoa ni chuo cha kuvumiliana na msamaha.
** Mola tupe busara kwenye ndoa hizi na wadada wa mwendokasi. Unaishi na mtu ana matusi utadhani hajafundishwa kwao.
uchaguzi uliofanya hukuwa sahihi.. ndiyo maana unakumbana nayo
 
Pole sana mkuu kwa changamoto za ndoa unazopitia, kuna vitu vingi vya kuchunguza kabla ya kumtamkia mchumba wako ndoa vitu ambavyo vinahitaji muda pia maana ukishamtamkia tu utamuoa kabla ya kumchunguza ataficha makucha yake na kukuonyesha only good side of her habit na kwa haraka utaona ni wife material kumbe ni wife disaster ukishaoa ndiyo utagundua ulioa au uliolewa na mtoto wa shetani na kama ni mkristo inabidi ukeshe kwa maombi pepo la uzinzi limvagae au arudi mavumbini kinyume na hapo ni mzigo wako huo.

Linapokuja suala la kuoa au kuolewa kama ulikuwa hauombi ndiyo muda wa kuomba kwelikweli ili Bwana akupe mtu sahihi
 
Pole Sana na hongera kwa uvumilivu wako Boss, Kwakuwa mmepiga hatua kubwa hivo suluhisho ni maombi tu ,Mungu akuongezee hekima ili utambue kusudi la maisha yenu kwenye hyo ndoa na akuwezeshe kufanya maamuzi sahihi pia.
 
Mkuu umeandika kwa hisia sana....najua uko kwenye peak ya uvumilivu....uvumilivu mkuu...... dont ever think the past,,,,think the future....only the future......iko mikononi mwako.......uendelee kuteseka au.......pole sana........ni njia tunapitia wanaume wengi...
 
Back
Top Bottom