Mbao za Mawe
JF-Expert Member
- May 11, 2015
- 23,367
- 55,055
Ndo hivyo tenaNa hili ndo tumaini pekee na nadhani ndo mantiki kuu ya kuwepo kwa dini na yote yanayofungamana nayo. Pasingekuwepo na kifo hata Mungu asingepata uungwaji mkono wa leo.
Pole sana Mkuu! Wazazi ni muhimu sana mama anachukua nafasi ya kwanza. Mama ni mlezi mwalimu protector mhubiri na zaidi ya yote ni Mungu wa pili duniani.Mama ameondoka hata hajaona mafanikio yangu, ameenda nikiwa mchanga sana kimaisha nilitamani siku moja awe mlezi wa wanangu pindi nipo kazini ila hakupata muda huo.
Nilimwambia mama nimepata mtoto kipindi nimeenda masomoni Arusha alifurahi sana ila hakupata nafasi ya kumwona wala kumshika mtoto wa kijana wake.
Inaniuma sana na nimetambua umuhimu wa mama baada ya kuona mji ulivyobadilika, jinsi mji ulivyojaa upweke mawazo kwa kila mmoja wetu.
Najua ni kazi ya MUNGU ila hakika nilitamani akupe maisha marefu hapa duniani ila kaamua sina uwezo wa kukurejesha kuna Muda naogopa kusema umefariki nikijua bado u hai ila baadae natambua kuwa ni kweli umefariki.
R.I.P Mama.
Yes pia wapate nafasi yakumrudia muumba wao/kutubu makosa yao.Na ndio maana watu wabaya hupewa maisha marefu ili tupate pa kujifunzia
Mambo vipi kaka mshanaHuwa nasoma hizi post Za JF, nawasiliana na watu pm, wengine tunakutana mitaani, na baadhi tunasoma habari zao
Naamini kwa dhati ya moyo wangu, wengi wetu hapa na kwingineko tumewapoteza watu muhimu sana kwetu kijamii na hata kitaifa na wakati mwingine kimataifa
Tuna wengi katika jamii yetu hii wako katika hali fulani kimaisha na wanakumbuka kwamba Kama fulani angekuwa hai Leo hii nisingekuwa hivi ama nisingekuwa hapa au nisingekuwa na haya mateso
Hawa ni wazazi wetu walezi ndugu marafiki jamaa na hata watu baki.. Wanatokea katika maisha yetu na kuwa watu muhimu mno watu wa msaada sana watu wa upendo sana....halafu ghafla wanazimika na kuzima ndoto nyingi, matumaini mengi fursa nyingi na hata misaada
Mambo yanapokuwa magumu, shida zinapozidi, unapopoteza matumaini Unakumbuka na kujisemea fulani angekua hai haya yote yasingetokea
Bahati mbaya ama nzuri mipango ya Mungu si ya mwanadamu, yeye ndie ajuaye Kutoka kwetu na kuingia kwetu....kila jambo linafanyika na kutokea kwa sababu..
Mungu hawezi kamwe kuziba milango yote lazima kuna mmoja atauacha wazi... Jitahidi uuuone.....
Cha kusikitisha ni kwamba wema anawachukua wabaya anawaacha... Imagine Leo hii ungeambiwa nani angestahili kufa ama kubaki ungempendekeza nani?
Mpk sasa umepoteza watu wangapi ambao walikuwa very potential kwakoPouwa
Pole aiseeMungu awarehemu i miss them so
Shukran mkuu imepagwa hatuwezi kukataa mipango ya mmiliki wetu.Pole sana Mkuu! Wazazi ni muhimu sana mama anachukua nafasi ya kwanza. Mama ni mlezi mwalimu protector mhubiri na zaidi ya yote ni Mungu wa pili duniani.
I was on my way back ngoja tutaongea kule
Tumsifuni Yesu kristo
mkuu kweli kabisa, kifo ndio kimefanya tumuogofyeNa hili ndo tumaini pekee na nadhani ndo mantiki kuu ya kuwepo kwa dini na yote yanayofungamana nayo. Pasingekuwepo na kifo hata Mungu asingepata uungwaji mkono wa leo.
Life goes onMwisho wa siku maisha lazima yaendelee