Kuna watu hawakustahili kufa

Namshukuru Mungu kunikutanisha naye. Alikuwa mbaraka mkubwa kwenye miaka 7 ya urafiki wetu.

Ameondoka mapema. Nilidhani tungekuwa pamoja miaka mingi ila hata ujana hakuumaliza.
Kila nikisogea natamani angekuwepo nimwambie.
Natumai tutakutana pasipo kifo.
 
Baba je
 
Kama baba akifika level za kukaa na ujauzito miezi 9, kutanua miguu na kuzaa, kulea kichanga - usiku na mchana bila kulala, kunyonyesha, na kuwa nguzo kuu kipindi chote basi naweza kumweka ligi 1 na mama. Kwa tukio 1 tu la kutafuta chakula baba siwezi mfananisha na mama hata chembe - wamama kibao ni watafutaji wazuri sana, tunawaona mitaani wanafungua vigenge, wanachoma vitumbua, wanafagia mabarabara, wanabeba hata zege.

Mama yupo kwenye ligi la kibabe la aina yake kabisa. Nihitimishe kwa kusema "usimfananishe mama na vitu vya kawaida kawaida".
 
Kweli Mungu hufanya mengi juu yetu, na mipango ya maisha ya mtu anayo tokea kuzaliwa kwake. Ila kuna wakati tunawakumbuka wapendwa wetu na kujawa na majonzi maradufu
 
Sikutaka Bob Marley afe kwa kwel,,,nikimsikilizaga na kujiuliza angekua mpka sasa hiv ingekuaje,,inaniuma mpka leo
 
Umetisha mkuu haaa
 
Brother Mshana...una huge spirit ya fatherhood in you..i bet wanaume wengi wanayo ila ya kwako imeenda mbali kidogo. Kusoma huu ujumbe kumenikumbusha mengi..kumtegemea Mungu in all times....kuheshimu na kutambua uwepo wa watu muhimu kwenye maisha when we have them as hapa duniani wote tunapita...na kila mtu ana mapito yake binafsi...especially kwenye kuwapoteza watu wa karibu kwenye maisha..
 
Kila jambo linalomtokea mwanadamu katika maisha yake huwa lina makusudi yake ,

Wakati mwingine mungu anawachukuwa watu ambao ni muhimu na msaada kwetu ,ili tujifunze kusimama wenyewe ..

Mola awalaze pema wale wote waliotangulia na walikuwa msaada mkubwa kwetu
 
ktk kitu nilikua sitaki kuona ni kifo cha Mama yangu nilikua naomba Mungu anichukue mm kabla yake lkn ikawa tofauti, Mungu amlaze mahali pema peponi mama yangu namkumbuka na kumpenda siku zote za maisha yangu [emoji120]

nilikua najiuliza nitaishi vipi bila Mama lkn Mungu mkubwa mpk leo naishi na nina maisha yangu hakika Mungu ni mwema sana.
 
amina
 
Pole mkuu . RIP your mom and my mom.
 
Ningempendekezaaaaa.........
Nimefikiria nikaona sina wa kumpendekeza afe maana nafsi inanisuta, ila ingekuwa wa kuwapendekeza wasife daaah!!
[emoji24] [emoji24] [emoji24] [emoji24] [emoji24]
 
Babu yangu

Huyu alikuwa na watoto wengi akiwemo mama

Ila aliniamini sana mimi, alinipenda sana

Alikuwa na pesa ya kutosha

Alifariki nikiwa form two

Baada ya kufariki watoto walipiga mali mnada

Badae iliniathiri hadi mimi kwani nilikuwa nasoma shule nzuri

Badae nikahamishiwa ya ada nafuu



R. I. P babu yangu, nitajitahid walau robo kurudisha heshima yako

Nb watoto wake Wote walisoma enzi hizo miaka ya 70 na 80
Moja aliwahi kuwa mhadhiri pale UDSM lakini hakuwa na msaada hata kidogo kwa mzee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…