Kuna wanaolindwa na nguvu za ziada

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,595
215,273
Kuna dada mmoja aliolewa na mkaka mlokole. Si unafahamu ule wakati umekaa kwenye shelf mpaka age mates zako wote wameolewa, mwisho unaamua anaekuja nitamkubali, ndicho kilichomtokea huyu dada.

Yeye alikua mkristu wa Jumapili tu lakini mume wake aliamka na kuomba kwanza kabla hajatoka chumbani. Alisaidia wenye shida. Mara nyingi alilipa ada za watoto wa wajane na kuwasaidia kodi ya pango. Alimpenda sana mke wake na aliamini kuna siku Mungu atamgusa na watasali pamoja.

Huyu dada na shost yake wakianzisha business empire. Walikodi nyumba na kuiwekea furniture. Wakaanza ku recruit vijana wa kike na wakiume kwa kutoa huduma za ngono kwa wahitaji. Wakitoka vijana mikoani, waliwafundisha kunywa vinyaji vya aina mbali mbali, kushika umma na kisu na hata kuongea Kiingereza. Soko lao walilenga wenye pesa, wawe raia wa Tanzania au wa kigeni.

Sasa biashara ilitaka uwangalizi wa karibu na bi shost yuko kwenye ndoa. Business partner alimuonya hii tabia ya kumuacha yeye kwenye danguro muda mrefu alafu wagawane faida ni kheri amnunue ajue biashara ni ya kwake.

Ni dada alitafakari, aliamua kwenda kwa mganga ili awe na sauti kwa mume wake, hata akichelewa kurudi mume wake asimuulize. Mganga alipatikana Malawi.

Mganga alitoa dawa tatu, moja unaweka kwenye chakula, moja katika mafuta ya kujipaka na ya mwisho kwenye kinywaji.

Siku ya kwanza yule dada ameweka dawa kwenye sahani ya mume wake. Alipompelekea chakula ile anamkaribia tu mume wake, akateleza chakula chote kikaanguka sakafuni na sahani kuvunjika.

Ile ya kupaka alichanganya na mafuta anayopaka mume wake. Yule mwanaume baada ya kuoga anashika chupa ya mafuta ikaanguka na kupasuka, mafuta yakamwagika chini.

Ya kunywa ilimtokea hivyo hivyo. Alirudi kwa mganga, mganga alimwambia nguvu zinazomlinda mume wako ni kubwa sana.

Baada ya muda danguro lilijulikana na vyombo vya dola na dada yule na bestie walikwenda jela. Yule kaka alipata mke mlokole mwenzake.
 
Na hadithi yetu inaishia hapa..

Ujumbe;ukimfanya MUNGU kuwa rafiki,atakulinda na kukutongoza katika njia zenye miiba na majaribu ambazo macho yako ya kawaida hayawezi kuona,yeye ni rafiki mwaminifu
Nafikiri hapo mkuu ulimaanisha "kukuongoza" badala ya "kukutongoza"
 
Back
Top Bottom