Kuna Vyuo Vikuu vinaaibisha elimu ya juu Tanzania(hasa vinavyoitwa 'Branch')

ikiumasema

JF-Expert Member
Oct 9, 2015
917
1,275
Unakuta Chuo kikuu kina sifa zifuatazo wakuu tusaidiane kina hadhi ya kutoa elimu ya Chuo kikuu.

1.Chuo kipo mjini katikati kimezungukwa na barabara kila upande...hivyo kuna makelele ya muziki ndani ya Chuo...makelele ya magari,honi za kila aina yaan kwa ufupi Ni full kelele asubuhi mpaka jioni.

2.Chuo kikuu hakuna hostel za wavulana ..hapa utashangaa Chuo hiki kilipataje ithibati wakati hakuna sehemu za kuwaaccomodate wanachuo?wanachuo wanapanga mitaan 97%...si kwa sababu wanapenda bali sababu hakuna sehemu za hosteli za wanachuo ambazo Ni nafuu

3.Chuo kikuu hakina facilities hata moja za michezo...yaan hapa namaanisha hakuna hata uwanja wa netball

4.Chuo kikuu hakuna sehemu ya kuweka vimbweta vya kusomea wanachuo...yaan jinsi kachuo kalivyo kadogo vimbweta vinakaa nyuma ya darasa.

5.Chuo kuingilia serikali ya wanachuo na kutishia kuwafukuza wanachuo pindi wanapoamua kusema madhaifu ya wazi wazi ya Chuo

6.Chuo hakuna madarasa ya kutosha yaan Chuo kikuu kina ghotofa moja lenye floor tatu tu huko ndio kila kitu ofisi mpaka lecture rooms...

6.Chuo kama hiki kina wanafunzi zaidi ya 800.
Sasa Mh Ndalichako tunakuomba utazame tena upya vyuo vya aina hii ili kuwapa wanafunzi mazingira rafiki ya kusomea

Vyuo vya aina hii vifungwe kabisa na vyuo vya aina hii hasa Ni vile ambavyo vinaitwa branch la Chuo kikuu Fulani.Asanten wadau .
 
Aisee.... Ndio hivyo sasa vimeshasajiliwa na kuviondoa tena ni process labda mkuu atoe amri... Na perhaps amri ishatolewa vifungiwe...... Lakini kwa upande mwingine vikifungiwa hivyo watanzania wengine watapata wapi elimu? Ndio hivyo acha tujikongoje na elimu yetu hivyo hivyo
 
Vipo vingi tuu na Ni vyuo vikuu sasa hata kama shule za sekondari na msingi Ni mbovu kwanini vyuo vikuu visiwekewe masharti viwe bora?inauma sana kuwa na mavyuo ya ovyo kama haya.....vifutwe tuu na mm sio chichiemu ila naunga mkono vifutwe tuuu
 
Back
Top Bottom