Serikali ina watu wengi, wenye tabia tofauti. Wakusanya kodi, hufanya kwa juhudi kukusanya ili kulinda kibarua na wengine hapo hapo kujipatia cha juu.
Wanaopanga matumizi ya hizo pesa ndio wanatoa kichefuchefu, maana haijulikani ni nini kipaumbele. Wananchi wana matatizo makubwa, na bado pesa zinaelekezwa katika maeneo ambayo hayana uhitaji wa lazima. Mfano malipo kwa wabunge na mambo ya kisiasa kwa ujumla.
Hivyo ninaloona katika uzi huu, si serikali bali watumishi ndio ambao hawana mfumo unaowaongoza, na hapa naona umuhimu wa Katiba nzuri itakayo waongoza kwa haki na uwajibikaji, na kuwaadhibu vile vile pale wanapoenda kinyume chake.
WaTz tuamke.