Kuna viongozi wengi ni Usalama wa Taifa!?

Kuna viongozi wengi sana ambao ni usalama wa taifa. Mmoja ambaye nina uhakika naye kwa 💯 ni Professor Mkumbo ambaye ni waziri kwa sasa. Miaka yote hata kabla ya kuingia Chadema alikuwa usalama wa taifa.
Mkuu Mundu, Kamundu , kwa lengo la kusaidiana tuu, kukusaidia wewe na wengine wasiojua, kumtaja kwa majina mtu yoyote wa TISS na kumu expose kuwa ni TISS, huyo mtu akiwa ni TISS kweli, then kumtaja kwa jina ni kosa la jinai!.

I can just imagine, kama sisi tuliajaliwa jicho la tatu, ma Tiss tunawajua kwa kuwaona tuu sura, je tungewataja ma Tiss wote tunaowajua, tungebaki salama?
Huwezi kutoboa boti mnayasafiria. Ikizama mnakufa wote!, au kulikata tawi la mti uliolalia!.

Kwa taarifa yako ma TISS ni wengi kuliko unavyodhania hata Sultani naye ni Tiss, hata Mkuu nanilii pia ni Tiss
Ila sio kila Tiss ni Tiss

Kuna ma Tiss wa aina kuu 3.
  1. Staff hawa ni waajiriwa rasmi wa tiss, wamepitia deppo Mbweni, na ni wafanyakazi wa Tiss, ni watumishi rasmi wa tiss na wameajiriwa kama wanausalama, hawa wote lazima wapite deppo na wana mishahara ya tiss, kama ilivyo kila polisi lazima apite CCP, kila jeshi lazima afanye deppo. Hawa staff rasmi wa tiss wako wa aina mbili, kuna open staff, hawa wale ma TISS wanajulikana rasmi ni ma tiss na ofisi yao ni TISS, kama DGIS na maofisa wote wa TISS wanaojulikana kama RSO, ma DSO etc, wana makundi matatu, Tiss main kulinda usalama wa nchi, GSU kulinda usalama wa serikali, na kitengo cha ulinzi wa viongozi, hawa kuwataja hakuna tatizo.
  2. Kuna ma TISS ambao ni ma tiss lakini wanafanya kazi under cover, SS, secret service, hawa wanapostiwa sehemu mbalimbali na kuajiriwa kama watu wa kawaida, (watu wa kazi mbilimbili) hawatakiwi kujulikana kuwa ni ma tiss, wako kila mahali, kila wizara, kila idara, kila taasisi, kila wakala, kila kitengo, na wanapenyezwa kila mahali hadi private sectors, wanakuwa planted, ikitokea ukawajua, huruhusiwi kuwataja!
  3. Viongozi wote, wateuliwa wote na watendaji wote, ambao wamepata uteuzi kupitia kufanyiwa, na tiss, hawa ni ma Tiss kwa mujibu wa positions zao, wana wajibu wa kufanya reporting kwa ofisa wa tiss by virtue za ajira zao.
  4. Wafanyakazi wote wa vitengo vya nusa nusa, ma ps, mesenja, posta kila barua suspicious zinafunguliwa kusomwa, zikikutwa na kitu zinakuwa scanned, inafungwa inakwenda kwa mhusika, hao ni ma tiss, wako makampuni yote ya simu, wana tap mawasiliano suspicious, wakiwemo mabenki yote yana mtu wa kitengo cha FIU hawa ni ma TISS, by virtue of reporting, mtoa taarifa wa FIU ni tiss, taarifa yake lazima ipite kwa bank manager hivyo mameneja wote wa banks na big financial institutions zote ni ma Tiss kumonitor miamala suspicious, au money laundering.
  5. Kundi la mwisho la ma tiss, na hili ndio kundi kubwa, ni la tiss ambao ni ma Informers, hawa ni watu wa kawaida kabisa, hawakupitia mafunzo yoyote, sio wa ajiriwa wa tiss, wanakuwa recruited kuripoti Tiss na kulipwa posho tuu, huku wakiendelea na shughuli zao za kawaida, tiss ina recruit informers kwenye eneo lolote lenye vested interest kuanzia ma shoe shiners, wadada poa, kutengenezea honey traps, wahudumu wa bar, mahoteli, walinzi, wasichana wa kazi, madereva taxi, bajaji, boda boda, saloon, mtu yoyote anaweza kuwa recruited, na kuwa planted kwenye area of interest, hivyo no one knows who is who.
NB. Mimi nina damu ya TISS kwenye veins zangu kwa wazazi wangu wote wawili, na tumezaliwa 8, haiwezekani sisi wote nane tukawamo!. Kunidhania mimi ni mmoja wao rukhsa na angalia hapa ninavyoisifia ofisi yangu TISS Ikanushe tuhuma za uvamizi, utekaji, utesaji na mauaji!. Wasijadiliwe na Bunge kwa uwazi bali wachunguzwe, wakithibitika wafumuliwe!

Hapa namtishia bosi wangu Wanasheria Waelimisheni Viongozi Wetu Kitu Kinachoitwa "Vicarious Liability", Hata Kama Wewe Hujaua, Kama Muuaji ni Mtu Wako, Then Unawajibika Wewe

Na kunapotokea matishio ya kiusalama, badala ya kuripoti ofisini, mimi tiss mimi, naripoti humu jf Security alert kwa Serikali yetu: Tuwe makini sana na Marekani, kuna kitu kinapangwa halafu wajifanye walionya kabla. Je, wanapanga kutu-Libya?

Boss wa TISS ni CinC, mwenyewe amepania ile mbaya 2025-2030, mtumishi wa idara anaweza kweli kuandika hivi ?. Kuna Kitu Rais Samia Amekisema Kuhusu Kurejea Kizimkazi “Post 2025”. Nashauri na Nasisitiza Wenye Uwezo Kusaidia, Tumsaidie Kumshauri Ukweli!

Boss wako anajipanga kwa mserereko wa 2025, kijana wake anaweza kupandisha kitu kama HII?.
Acheni hizo!, ila ma tiss wenyewe humu wapo na wengine tunawajua!.
P.
 
Kuna viongozi wengi sana ambao ni usalama wa taifa. Mmoja ambaye nina uhakika naye kwa 💯 ni Professor Mkumbo ambaye ni waziri kwa sasa. Miaka yote hata kabla ya kuingia Chadema alikuwa usalama wa taifa.
Hii ndio Tanzania......Toka enzi ...umdhaniae ndiye .......kumbe ndiye siye....aliye...ndiye...siye ...ndiye.....
hta Mizengo Pinda mpaka na leo ni systemaaa
 
Mkuu Kamu, Kamundu , kwa lengo la kusaidiana tuu, kukusaidia wewe na wengine wasiojua, kumtaja kwa majina mtu yoyote wa TISS na kumu expose kuwa ni TISS, huyo mtu akiwa ni TISS kweli, then kumtaja kwa jina ni kosa la jinai!.
P.
Na ndio maana ya JF na sababu ya kutumia fake username, especially kwa hawa wasiokua na msaada wowote kwa Umma, tuwajue tu sisi ndio tunaowalipa kwa kodi zetu. Sheria zipo ili zifatwe au zivunjwe na Magereza yapo kwaajili yetu, tukifwata wote sheria, magereza yatafungwa sasa.
 
Back
Top Bottom