Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 41,611
- 65,061
Hii ilitokea kwa rafiki yangu ambaye tulikuwa tunafanya naye kazi miaka mingi iliyopita. Ilikuwa ni kipindi cha mwezi kama huu.
Tulikuwa tumepanga nyumba nzima tukawa tumegawana vyumba. Jamaa alikuwa ni mtaratibu sana na mpole, kutokana na malezi aliyokulia.
Nikawa nimepata likizo, nikasafiri kwenda kutembelea familia yangu, na huyo rafiki yangu nikawa nimemuachia mjengo. Baada ya likizo kuisha nikarudi mzigoni, kufika tu mjengoni napata habari jamaa amekuwa chizi, na amepelekwa kwao na mwajiri.
Kwa kuwa nilikuwa nafunguo za mjengo, nikafungua nikaingia ndani, pale sebuleni nikakuta chupa za pombe na nguo za mwanamke; mitandio, taiti, na vitenge.
Nikatafuta kijana wa usafi, asafishe ili mazingira kuwa safi. Kesho yake nilipoingia kazini ndio napata taarifa kamili, kuwa jamaa alilala na mke wa mtu mle ndani, jimama aliyekuja mapumzikoni, matokeo yake jamaa amekuwa kichaa.
Kwa sababu nilikuwa naishi naye nyumba moja jamaa, ikabidi niombe ruhusa niende kumtembelea huko kwao. Nilipofika nilikuta mshikaji anaongea mwenyewe, sikuamini kama ndio yule jamaa aliyekuwa mtaratibu. Kuna wakati kumbukumbu zinamjia na kunielezea matukio, baadaye akili inaruka.
Baada ya hapo, niliwapa pole ndugu zake, nikarudi mzigoni.
Wakuu, nimekumbuka kuwapa hii stori hasa kipindi hiki, kwa sababu watu wengi wanasafiri, unaweza kuona mtu mtaani kwako amenona, kumbe ni balaa tupu; kumbuka kuna vingine huwa havionjwi!