View attachment 374994sifa moja nzuri kwa mtoto anayotakiwa kuwa nayo ni utii, asibishane na wakubwa na akubali bila maswali yale anayoambiwa, hili ni jukumu la mzazi/mlezi
Bahati mbaya sana kuna baadhi ya wazazi na walezi wameitumia hii hakimiliki vibaya..kuwafundisha watoto mambo mabaya au kuwaingiza watoto kwenye viapo na maagano yasiyofaa
Maagano mabaya kabisa ni haya yanayohusisha damu..damu ni kitu hai hivyo hutengeneza roho
View attachment 374996tumeshuhudia wimbi kubwa la watoto wakiwa wachawi mahiri tena wanaofanya mambo ya kutisha hasa...tumeshuhudia ukubwani watu wakiteswa na mapepo yasiyojulikana chanzo chake au kuwa vigumu mno kufuatilia chanzo chake
Wakati huo unakuta wazazi au walezi wanakuwa tayari hawapo duniani na hawakuacha maandishi yoyote kwa kile walichofanyia watoto
Tunaweza kufanya mambo kwa nia njema kabisa lakini tukumbuke kuacha formula ya yale tuliyoyafanya
Hizi ishu za kinga ujasiri na kutengeneza bahati kwa watoto wetu twende nazo kwa tahadhari kubwa kwakuwa huwa na vigezo na masharti na huwa na expire date