Kuna ulazima gani wa kusema tunamshukuru Rais Samia? Kwanini isiwe tunashukuru Serikali yetu?

The Lastdream

JF-Expert Member
Jan 23, 2024
1,581
3,487
Wakuu mambo ni vipi?

Leo nilikuwa naomba kuuliza hivi ni lazima kumshukuru mtu ambaye umemuajiri?
Wakati anafanya kazi na unamlipa pesa yake?

Sikatai mtu kupongezwa Lakini inapozidi inashusha ufanisi wa kazi kwa mtu huyo,
Kuna ulazima gani wa kusema tunamshukuru rais Samia? Kwanini isiwe tunashukuru Serikali yetu?

Jenerali ulimwengu anasema “mtu aliyeomba kazi mwenyewe asipofanya wajibu wake lazima tumseme na akifanya tutakaa kimya sababu huo ni wajibu wake”

Embu wataalamu mseme hapa Mbona Kama kipindi cha hayati mzee Mkapa haya mambo hayakuwepo? Kwanini Hivi vitu vimeshamiri kuanzia kwa hayati Magufuli?
 
Kiufup tu niseme hatuna haja ya kushkuru yeyote apo, sababu kazi wanayofanya kukusanya kodi kuleta maendeleo wanalipwa mshahara wao kama mwalim au dr na fani zingn wanavolipwa. Mfano kuna haja ya kushukuru mwalim akimfundsha mwanao? Au dr akitibu mgnjwa c analipwa kwa anachokifanya. Vinginevyo ni wiz na kujipa umiliki ambao sio wao. Wao na sis tunatakiw tumshkur Mungu tukipat maendeleo yeyote
 
Umeshawahi kusikia kuwa Kenyatta alimkejeli Nyerere kuwa alikuwa akiongoza maiti? Inawezekana bado kuna viongozi ambao wanaakisi kile ambacho kilimfanya Kenyatta amsimange Nyerere.

Kwa exposure aliyo nayo, sikutarajia kuwa na mama Samia naye angeridhia sifa za kinafiki kutoka kwa machawa, eti Rais katika bilioni tano wakati hata mshahara wake haufiki milioni mia mbili kwa mwezi.

Kodi zetu zimegeuzwa fedha za mama Samia? Nina mashaka na uwezo wa kufikiri wa wanasiasa wetu.

Rais ni mtumishi wa umma. Akifanya vizuri apongezwe na siyo kupakwa mafuta kwa mgongo wa chupa.
 
Umeshawahi kusikia kuwa Kenyatta alimkejeli Nyerere kuwa alikuwa akiongoza mauti? Inawezekana bado kuna viongozi ambao wanaakisi kile ambacho kilimfanya Kenyatta amsimange Nyerere.

Kwa exposure aliyo nayo, sikutarajia kuwa na mama Samia naye angeridhia sifa za kinafiki kutoka kwa machawa, eti Rais katika bilioni tano wakati hata mshahara wake haufiki milioni mia mbili kwa mwezi.

Kodi zetu zimegeuzwa fedha za mama Samia? Nina mashaka na uwezo wa kufikiri wa wanasiasa wetu.

Rais ni mtumishi wa umma. Akifanya vizuri apongezwe na siyo kupakwa mafuta kwa mgongo wa chupa.
Maza ni mpenda sifa vibaya sn
 
Taifa la watu conscious/wanaojielewa huwezi sikia hayo Bali taifa linaloendekeza uchawa na kiki za kijinga
 
Umeshawahi kusikia kuwa Kenyatta alimkejeli Nyerere kuwa alikuwa akiongoza maiti? Inawezekana bado kuna viongozi ambao wanaakisi kile ambacho kilimfanya Kenyatta amsimange Nyerere.

Kwa exposure aliyo nayo, sikutarajia kuwa na mama Samia naye angeridhia sifa za kinafiki kutoka kwa machawa, eti Rais katika bilioni tano wakati hata mshahara wake haufiki milioni mia mbili kwa mwezi.

Kodi zetu zimegeuzwa fedha za mama Samia? Nina mashaka na uwezo wa kufikiri wa wanasiasa wetu.

Rais ni mtumishi wa umma. Akifanya vizuri apongezwe na siyo kupakwa mafuta kwa mgongo wa chupa.
Jamani, wakati ule wakenya ndiyo walikuwa wamelala, ndiyo maana Mzee Kenyatta alijichukulia ardhi karibia yote ya Kenya ikawa yake binafsi na familia yake. Sasa jiulizeni nani alikuwa anaomgoza mizoga kama hapo kama mnavyofanywa leo
 
Back
Top Bottom