Kuna ukweli juu ya internet money

Kuna ukweli juu ya internet money

Wakuzi wa mambo hizi issue za kazi za online kuna ukweli chech hiyo. GetPaid4Visits.com Earn 10$ for every 30 second Task. Internet Job
  • Hakuna ukweli katika hili.
  • Usipoteze muda - kamwe hakuna fedha ipatikanayo kwa njia hiyo
  • If you need to make money online fanya yafuatayo

  1. Kuwa na account ya Paypal
  2. Pia fungua account Ebay
  3. Kisha tafuta hiki kitabu"how to make money online using Paypal and Ebay"
Kwa kifupi wewe utakuwa mtu wa kati na utapata asilimia furani kwa bidhaa ambazo utakuwa ukiuza kama reseller wa hizo bidhaa.
Pia waweza fungua kijiofisi cha kuagiza bidhaa toka nchi za ulaya na ukalipwa mfano asilimia 15 ya kila bidhaa ambayo mteja wako ataagiza.
 
Asante mkuu. Hiki kitabu kinapatikana wapi kwa hapa bongo au online?
 
Asante mkuu. Hiki kitabu kinapatikana wapi kwa hapa bongo au online?
  • Kinapatikana online kwa ghalama isiyozidi 6 USD
  • Pia jenga urafiki na google utanufaika na kujifunza mengi
 
kaka its possible kupata hela online sema ni ngumu si kama unavyofkiria, hizi ndo njia za kupata hela online

kwa kumiliki website
ukiwa na website yako utaweka matangazo na kupata hela kuna makampuni mbali mbali ila so far inayolipa vizuri ni google adsense

niliwahi kuwa publisher wa admob kabla haijanunuliwa na google na walikua wanalipa hivi
-tangazo la picha (banner) usd 0.04 kila click
-tangazo la maneno usd 0.01 kwa kila click
hawa ndo walikua wanalipa vizuri ila wengine walobakia wote walikua wanakaba
kwa hio unaona jinsi gani ilivyo ngumu. inahitaji kuwa na website yenye trafic kubwa kama jf ili upate mshiko wa maana

kwa kujiunga na website za kupata hela online
inawezekana kupata hela online na mimi nishapata sema pia ni ngumu hizi ndio kazi unazopewa kufanya

1. kuangalia matangazo, kila tangazo unaloangalia hawa jamaa watakulipa na kila tangazo unalipwa kuanzia 0.001 usd mpaka 0.01 inategemea na eneo ulipo matangazo yanakua mfumo wa picha, maandishi au video. hapa ina maana unaweza ukaclick matangazo 1000 ndo ukapata dola 1 nafkiri hapa unapata picha jinsi ilivyo ngumu.

2. kukamilisha offer, hapa unaweza ukaambiwa udownload application za android na iphone au ukapewa task yoyote kisha unalipwa app nyingi utazodownload ni virusi na malware wa kutosha inabidi uwe mtaalamu kidogo kwa kila app unapata hadi 0.25usd

3. kufanya survey, si rahisi kuzipata kibongo bongo ila ukitumia vpn za marekani utapata survey za kufanya na kupata hela.

kwa kuwa wakala
unaweza ukapata hela online kwa kuwa wakala mfano unapewa bidhaa uuze online sehemu kama ebay, kila bidhaa itayotoka na wewe unalipwa.

njia za kulipwa
1. kwa kutumia online banking kama paypal, payza na bitcoin
2. wire transfer hela zinaingia moja kwa moja kwenye account
3.kupitia cheque
4.western union

tahadhari
kuna wezi wengi online na karibia 99% za website za kupata hela ni za uwongo, njia hizi zitakujulisha website za uongo
1. offer zao hazileti maana, mfano mtu anakwambia invite watu tukupe hela kila mtu anakuja tutakupa dola 10, je wao wanapata wap hela? hapo unaona kuwa hamna ishu
2. kuireview hio site online, mfano site inaitwa earnmoney.kom basi igoogle earnmoney.kom scam or not then utaona revie ya hio site.
 
kwa kuwa wakala
unaweza ukapata hela online kwa kuwa wakala mfano unapewa bidhaa uuze online sehemu kama ebay, kila bidhaa itayotoka na wewe unalipwa.

njia za kulipwa
1. kwa kutumia online banking kama paypal, payza na bitcoin
2. wire transfer hela zinaingia moja kwa moja kwenye account
3.kupitia cheque
4.western union
  • Nimeupenda huu ufafanuzi, ndio kitu nilichomgusia ndugu yetu hapo juu.
 
mimi pia nadhani kujifunza juu ya forex market ni jambo zuri kama una mtaji unaoeleweka
 
@Mwl.RCT mimi niko nje ya hii topic..ninachopenda kujua ni juu ya hii biashara ya vpn.. unaweza kunifafanulia?
 
Back
Top Bottom