Kuna uhusiano gani wa lugha ya kiarabu na majini?

majini ni viumbe kama tulivyoumbwa sisi, mimi na wewe. wapo majini wa kike na wakiume. wapo majini wa kila kabila kama tulivyo mimi na wewe. aisha pia kuna majini waovu na majini wenye imani kama tulivyo mimi na wewe........... HAKUNA MAHUSIANO YEYETO KWA HILO ULILOULIZA.
 
Umeshawahi kusikia jini linaitwa Thomas?
Mkuu wewe nahisi haujatembea kabisa ndio maana unauliza swali la kitoto kama hilo. Nilienda sehemu huko kwa wanyamwezi yule mwenyeji wangu alikuwa ana matatizo ya mashetani alivyopandisha jini alijitambulisha anaitwa John tena sio mswahili anaongea kiingereza. Can you imagine mtu wa kijijini hajui hata kusalimia kwa kiingereza lakini alikuwa anaongea ile yenyewe kabisa british English.

Tukirudi kwenye hoja ya mleta uzi hiyo imani ya maneno ya kiarabu kuhusishwa na majini ipo Tanzania tu kwa sababu waganga wengi wanawadanganya watu kwa kuandika herufi za kiarbu maana hata wao ukiwaambia wasome walichokiandika hawakijui.

Nahitimisha kuwa hakuna uhusiano kati ya mashetani na kiarabu kwa kusema kuwa mashetani yote lazima yajue kiarabu.
Nawasilisha.
 
Mkuu wewe nahisi haujatembea kabisa ndio maana unauliza swali la kitoto kama hilo. Nilienda sehemu huko kwa wanyamwezi yule mwenyeji wangu alikuwa ana matatizo ya mashetani alivyopandisha jini alijitambulisha anaitwa John tena sio mswahili anaongea kiingereza. Can you imagine mtu wa kijijini hajui hata kusalimia kwa kiingereza lakini alikuwa anaongea ile yenyewe kabisa british English.

Tukirudi kwenye hoja ya mleta uzi hiyo imani ya maneno ya kiarabu kuhusishwa na majini ipo Tanzania tu kwa sababu waganga wengi wanawadanganya watu kwa kuandika herufi za kiarbu maana hata wao ukiwaambia wasome walichokiandika hawakijui.

Nahitimisha kuwa hakuna uhusiano kati ya mashetani na kiarabu kwa kusema kuwa mashetani yote lazima yajue kiarabu.
Nawasilisha.


mkuu kuhusu john hilo ni la kawaida mbona

home kwetu kuna mama/kama ndugu yetu kwa mbali alikuja ana majini.
alivyopandisha tukamuuliza yule jini jina ,dini na alipotoka.
yule jni alidai yeye ni mkristo tukamuuliza maswali kadhaa kama anamuamini yesu kama nani akawa anajibu

sasa tukamuambia huyu mama ni muislamu na wewe ni mkristu kwanini usiondoke umwache ,jini akawa mbishi anakataa

tukaanza kumpiga mawaidha asilimu akawa mbishi


kuhusu kuitwa john sikubishi mimi nmeshuhudia matukio mengi ya watu wanaopandisha na wanaotolewa.
 
Hakuna uhusiano wowote wa lugha ya kiarabu wala maandishi ya kiarabu na majini/ushirikina.Mara nyingi ktk kumuhadaa mwanadam hasa mtanzania waganga/majin hutumia herufi/lugha ya kiarabu ili kuendana na kasumba iliyotawala moyoni mwa wahusika ili kumuaminisha ni jini AMA kuna nguv z kipepo.Ukwel Uislam ambao kiarabu kimesheen una elimu/ujuzi juu ya hao majini basi watu wakayakinisha Uislam na majin lao moja wakat si kwel.Kama ilivyo waganga kuwahadaa kwa nyimbo zisizoeleweka AMA kwa vitambaa vyekundu na vyeupe AMA pengine na vibuyu,ndivyo hivyo pia majini na waganga huwaadaa kwa maashishi ya kiarabu.MAJINI YATABAKI KUWA MAJINI NA LUGHA ITABAKI KUWA LUGHA PASI NA MAHUSIANO.
Lugha by dfn ni njia tu yakuwasiliana ama utambulisho wa nchi/mahala fulani.
 
  • Thanks
Reactions: RTI
Ana malaria huyo ishapanda kichwan,

Muwaishen hospital,mtauwa watu kwa iman hiz wakuu
 
swali lako ni zuri kiongozi

1.kwanza inabidi utambue kwa hapa Tanzania kuna dini 2 kuu Uislamu na Ukristu hawa mimi nawaita watani wa jadi kama vile simba na yanga.Kila upande lazima ikandie na itoe propaganda kwa pande nyingine.

2.Kuhusisha Lugha ya kiarabu na Majini?kwanza naomba nikuambie kitu kuna majini wa kila namna ndio maana unaweza kukuta mtu kapandisha majini anaongea kimasai ,mwingine anazungumza kiingereza,mwingine anazungumza lugha haieleweki na wengine wanazungmza kiswahili fasaha?swali huyu anayezungumza kiswahili fasaha inakuwaje kwahiyo kiswahili ni lugha ya mapepo??

3.Mimi hapa binafsi nilipatwa na majini nikiwa nchini China nikipata mafunzo yangu binafsi ,na nilitupiwa jini na wachina ''Mabudha'' hivyo tambua majini kila mahala wapo na wa kila aina wapo..na pindi natibiwa tabibu wangu alipata shida sana.

4.wakati napatiwa matibabu nilijifunza mengi kutoka kwa mganga ambaye hutoa majini,kuna majini ya kila namna ,labda subiri nikujibu swali lako kuna matabibu ambao hutoa majini au hutuliza kwa kutumia ''Ruqya'',Ruqya ni nini??

"Ruqya"

ni kisomo ambacho huhusisha baadhi ya sura au aya ndani ya Qur an kumsomea mtu aliyepatwa na majini na mara nyingine huandikwa kwenye karatasi na kupewa mgonjwa..Ruqya ni tiba mashuhuri kwa wenye matatizo ya majini miongoni mwa waislamu..kma vile unavyoona mafuta ya mzeituni wanaotumia akina upako na wachungaji wengine hivo hivyo kwa Ruqya....mfano mtu ana majini basi mtu anayetibia au yeyote yule husoma aya hizo na yule mtu hupandisha kisha yule tabibu au yeyote yule huongea na yule jini kumuuliza maswali kadhaa mfano ni kwanini anamsumbua mgonjwa,labda ni nani aliyemtuma, alimuingia vp mgonjwa ,aondoke nk..hii kitu huwa ndio inawachanganya sana wachungaji binafsi mimi hii ruqya nimeitumia kwa jamaa zangu nilivyokuwa bweni pindi wakipandisha majini huwa nawasomea kisha hutulia...misconception ya wachungaji au mbinu tu ya kuwahadaa waumini wao waone lugha fulani ndio ya mapepo na waumini bila ya research huamini na kukariri..


NB:kama awali nilivyosema kuna mtu anapandisha jini anazungumza lugha ya kiswahili,ina maana lugha ya kiswahili ni lugha ya mapepo....Hilo swali ungewauliza hao jamaa unadhani ni jibu gani wangekukupa??mpaka hapo huoni kuwa ni propaganda...

Alamsiki[/QUOTE
AHSANTEEEE, UMEMJIBU UZURI KABISAA... Nami namwalika kama yuko Dar,anitafute nimwonganishe na mtu alienauwezo wa kumwomba Mungu na hayo majini yakaondoka. 718 45 88 33 K.Lungu mim hapa hlf tamuonganisha na Ustaadh Daruesh amsaidie
 
Ukinpigia takuonganisha na Ustaadh, anaeza muomba Mungu na Mungu akamsaidia jini hilo likaondoka Piga 718 45 88 33
 
Ndugu zetu huwa mnajitahidi sana kukataa hili, ila ukweli kuna uhusiano mkubwa wa quran, kiarabu na majini.

Hivi vitu vinaenda sambamba kama nyanya kitunguu na chumvi.
Fikra duni kabisa hizi zinazoongozwa na mafundisho ya wachungaji waweze kukunasa kirahisi fanya utafitj ukiweka akili yako huru utaelewa mkuu.
 
imekuaje hadi nikajiuliza hilo swali?

story yenyewe iko hivi.

nina rafiki yangu wa kike,siku za hivi karibuni yapata kama mwezi sasa,mara kwa mara na humtokea baada ya kutoka kusali tu,anajikuta anandika vitu ambavyo hata yeye havijui.anakuja kushtuka tu ameandika.hiyo hali haikutushtua na tuliona kawaida tu

kilichotushtua ni hiki

alianza kuandika kwa kukoroga koroga kama ambavyo watoto wa awali huwa wanafanya wakipewa daftari na peni bila kufundishwa chochote.kisha akaanza kuimprove kidogo kidogo na ikafikia hatua anaandika kitu furan kinachoeleweka ambacho hatujui ni nini na ni lugha gani.

kwa kifupi kapitia hatua zote za mtu ambaye anajifunza kuandika lakini hata yeye binafsi hajui.ila anaandika mtindo kama kikolea au kichina kwa kwenda chini,tumejaribu kugoogle lugha mbali mbali hatukupata hata lugha moja ya mtindo huo

mashaka yakaanza
baada ya hiyo hali tukaanza kupata mashaka kua inawezekana kuna namna kiroho,pengine ni lugha ya kiMungu au ni mapepo.

tukaona tuwashirikishe watu wa Mungu(nazungumzia waokovu).siku ya ijumaa ikabid aende kwenye jumuiya na akawasimulia kila kitu.
baada ya kuonesha hilo daftar analoandika mama wa kwanza tu ambaye ndio mkuu wa jumuiya akashtuka ,akasema hiki si kiarabu lugha ya mashetani au majini.kisha akamwambia chukua namba ya simu badae utanipigia.lakini mpaka saizi hatujampigia maana bado tunamaswali mengi juu ya kauli yake.

swali liko hivi.
Ni kwanini ?hasa wakristo huwa wanahusisha lugha ya kiarabu na mambo ya kishirikina,majini,mapepo nk.
ikitokea sehemu yoyote ambayo inautata frani hivi kukawa na lugha ya kiarabu basi wazo la kwanza ni mapepo.

hiki kitu nmekisikia mara nyingi na nlijua ni kwa watu ambao hawajui.mambo ya Mungu sasa kilichonishangaza hadi myu wa Mungu nae yumo kwenye huo mkumbo.

mwenye ufahamu tafadhali tubadirishane uzoefu.

Angalizo,mimi ni mkristo na naamini katika Mungu,pia naheshimi dini zote duniani.kama.ninavyoheshimu dini yangu.mada kama hizi huwa hazichelewi kuhama lakini mimi sipo hapa kukashifu dini ya mtu yeyote.nipo hapa kupata ufafanuzi.na pia kama kutakua na mtu ambaye anaweza kunisaidia kuhusu tatizo la huyo dada nitamshukuru sana.

kama kuna sehem patahitaji kueleweshana nipo hapa,

natanguliza shukran
sipo upande wa dini yoyote
ila unapokuja katika swala LA hawa viumbe majini huwa wanatumia lugha nyingi na anaweza piakujifunza lugha nyingi hata ile wanayoita enock lugha ya mailika ili tu kufikisha ujembe kwa mlengwa na kiarabu kipo cha aina nyingi ni lugha kama lugha nyingine ila swala LA huyo rafiki yako anaweza kuwa na connection ambayo yy au ww au mchungaji asikuwa na elimu ya viumbe hao kutoijua na connection ishia kukemea na kukemea bila mafanikio mwisho wa siku unakuta rafiki yako anaumia bila mafanikio yyt ninacho kushauri tafuten watu ambao wana elimu na mambo hayo ili wakupeni mwanga wa kutatua tatizo nafsi zetu zina upande mzuri na mbaya pia hivyo hata kwa viumbe wengine.
 
Fikra duni kabisa hizi zinazoongozwa na mafundisho ya wachungaji waweze kukunasa kirahisi fanya utafitj ukiweka akili yako huru utaelewa mkuu.
tatizo MTU akisoma mistari miwili kesho anataka aanze kuwa mhubiri ndio maana akili zao na nanilizao zipo sawa kabisa kujifunza kitu usichokijua huwa in jambo LA maana sana
 
Fikra duni kabisa hizi zinazoongozwa na mafundisho ya wachungaji waweze kukunasa kirahisi fanya utafitj ukiweka akili yako huru utaelewa mkuu.
tatizo MTU akisoma mistari miwili kesho anataka aanze kuwa mhubiri ndio maana akili zao na nanilizao zipo sawa kabisa kujifunza kitu usichokijua huwa in jambo LA maana sana
 
Mkuu!kwa uwelewa wng finyu juu ya hayo nambo sio lugha ya kiarabu tu ila wngne wanaandika au kuongea lugha nyngne km kiingereza na lugha nyngne..kwn me nimeshaona mtu anaongea kiingereza,na wkt yeye ajui hiyo lugha akiwa kawaida..
Kuna mwingine anaongea kimasai na yeye si mmasai. Hayo yote yapo. Namshauri wampate anayeijua hiyo lugha kisha atafsiri maandishi hayo ili wajue yana maana gani.
 
Back
Top Bottom