Kuna uhusiano gani kati ya vitu vibayavibaya na Uswahili?

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,871
155,840
Nauliza hili swali, maana naona Kila kitu kibaya ni kama Kiko kwa ajili ya Waswahili.

Makazi yakiwa Bora na mazuri huitwa Uzunguni, makazi yakiwa mabaya na duni huitwa Uswahilini. Mbwa Koko wabaya (Basenji) huitwa mbwa wa Kiswahili, na wale wazuri huitwa wakizungu.

Ng'ombe wazuri wanono, mbuzi, Bata na vingi vinevyo. Mtu mwenye tabia mbayambaya huitwa Mswahili. Mtu muungwana huitwa mzungu. Mtu asiyetunza muda hufananishwa na Mswahili na hafanishwi na mzungu.

Kuna kiongozi mmoja anaogopa kuhudhurua mikutano ya kikanda na ya kimataifa kwakuwa hajui vyema kuongea Kingereza.

Jamani tuachane na huu ubazi tupende vya kwetu
 
Waswahilina hao, wengi hawana shule kichwani.unategemea nini kutoka kwa watu wa dizaini hiyo kama siyo mambo ya hovyo hovyo, fitina, ulozi, majungu, utapeli, umbea wa kusutana vibarazani, stori zisizoisha kwenye vijiwe vya gahawa...
 
Nauliza hili swali, maana naona Kila kitu kibaya ni kama Kiko kwa ajili ya Waswahili.

Makazi yakiwa Bora na mazuri huitwa Uzunguni, makazi yakiwa mabaya na duni huitwa Uswahilini. Mbwa Koko wabaya (Basenji) huitwa mbwa wa Kiswahili, na wale wazuri huitwa wakizungu.

Ng'ombe wazuri wanono, mbuzi, Bata na vingi vinevyo. Mtu mwenye tabia mbayambaya huitwa Mswahili. Mtu muungwana huitwa mzungu. Mtu asiyetunza muda hufananishwa na Mswahili na hafanishwi na mzungu.

Kuna kiongozi mmoja anaogopa kuhudhurua mikutano ya kikanda na ya kimataifa kwakuwa hajui vyema kuongea Kingereza.

Jamani tuachane na huu ubazi tupende vya kwetu
Nyuki wametulia zao kwenye mzinga wao na shughuli zao, bila sababu ya msingi unaenda kuutikisa mzinga. Hivi kweli wakikuuma utawalaumu?
 
Back
Top Bottom