Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,809
- 15,417
Nimekuwa nikikutana na mijadala kuhusu kile wenzetu wanachoita Teleportation.
Nimejaribu kupitia mijadala mbalimbali katika mtandao wa Youtube lakini nakutana na habari za kwamba ni uzushi hakuna kitu kama hicho.
Ukisoma definition ya Teleportation ni kwamba:
Teleportation, or Teletransportation, is the theoretical transfer of matter or energy from one point to another without traversing the physical space between them. It is a common subject of matter in the cognition science fiction literature, film, video games, and television.
Sasa basi kama ukiangalia some clip za hicho wenzetu wanachoita Telepotation unaona mtu au mnyama au gari lilikatiza barabarani ghafla bila kuonekana lilipotokea ambapo dereva anapojaribu kukwepa anapata ajali mbaya sana.
Katika familia yetu kuna madereva wengi wa mabasi na wengine wa malori. katika simulizi zao niliwahi kuwasikia wakisema kwamba kama wakiona mnyama mtu au kitu chochote kikikatiza barabarani ghafla hawafungi break na mara zote kitu hicho hawakigongi na kinapotea kama hewa na wale waliowahi kujaribu kukwepa na kupata ajali wakirudi nyuma hawakuti kitu chochote.
Yapo maeneo ambayo huhusishwa na matukio ya aina hii na madereva wengi wanayajua na matukio hayo huitwa chunusi.
Sasa baada ya kuona hiyo video hapo chini nikawa na maswali ya kujiuliza na ndiyo sababu ya kuweka mjadala mezani.
Kaka mshana jr popote ulipo unaweza kujongea katika eneo hili kutupa ufafanuzi Zaidi.