Zitto
Former MP Kigoma Urban
- Mar 2, 2007
- 1,562
- 10,890
Kuna nini Tanzania na India
Kwenye ziara tunayotembelea madiwani wetu wa ACT Wazalendo kuna jambo nimeliona linajitokeza mahala pengi kila ninapoongea na Wananchi. Jambo hilo ni kushuka kwa bei za mazao ambayo Wakulima walikuwa wanategemea soko la India. Mbaazi, Choroko, Dengu na giligilani ni baadhi ya mazao ambayo nimesikia malalamiko makubwa ya bei zake.
Jana nilipokuwa Sumbugu, Misungwi Wananchi walinieleza kuwa mwaka 2016 waliuza choroko kwa shilingi 300,000 kwa gunia Lakini bei hiyo ilishuka mpaka shilingi 150,000 na kwamba wanunuzi wamepungua mno. Vile vile Dengu imeshuka sana bei kutoka shilingi 7000 kwa kilo 4 hadi kufikia shilingi 2500.
Nilipokuwa Gehandu, Hanang nilielezwa kuwa bei ya giligilani imeshuka kutoka shilingi 150,000 kwa gunia mpaka shilingi 25,000 tu.
Chama chetu kilifanya utafiti wa zao la mbaazi kwa mikoa ya kusini mwaka Jana. Kadhia ya mbaazi tumeikuta pia Mkuranga, Morogoro na Mkoa wa Manyara. Bei imeshuka kutoka wastani wa shilingi 1500 kwa kilo mpaka shilingi 50 kwa kilo na maeneo mengine hakuna soko kabisa.
Swali
Mazao yote haya yaliuzwa India. Kwanini Bei zimeshuka na masoko kuanguka kabisa wakati mahitaji ya bidhaa hizi huko india yanakua mwaka hadi mwaka? Kuna nini kati ya Tanzania na India? Kuna nini Wakulima na Watanzania hawaelezwi?