THE BOILER ROOM
JF-Expert Member
- Sep 17, 2018
- 1,054
- 3,210
Kwanza kabisa naomba mnisamehe kama Uzi wangu unaofanania na kudhihaki ila hii si shabaha yangu!Shabaha yangu kubwa ni kutoa taswira ya namna mabadiliko ya matumizi ya ardhi ya maeneo husika yalivyotofautiana sana na mpango wa awali wa matumizi ya ardhi ya maeneo hayo kabla;
Enzi hizo wakati naishi mimi:
Masaki ilikuwa ni Residential Area pekee huwezi kuta ofisi yoyote iwe ya serikali au taasisi binafsi ikifanya shughuli zake maeneo hayo.
Miaka hiyo Masaki huwezi kuta jengo lenye urefu wa ghorofa zaidi ya ghorofa tatu kwa uchache na upekee wake utakutana na mazingira ya namna hiyo kwny maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya flats yakiwemo maeneo kama ya TIB,THB na kule Harbors.
Masaki ya wakati huo wahudumu walikuwa hawarudi makwao zaidi ya kuishi kwenye nyumba za servants zilizokuwa nyuma ya nyumba kubwa za maboss wao
Wakati huo Masaki huwezi kuta watu wakiwa wamezagaa zagaa hovyo asilimia kubwa kwenye mtaa husika watu tulikuwa tukifahamiana kwa sura hata kama tulikuwa hatusalimiani.
Kwa kifupi mimi nimeishi na kukua kwenye mtaa wa Haile Selassie.