teh teh ...hiyo picha ya chini enzi hizo ilikuwa inatwa msaragambo ,watu hujitolea muda na nguvu kufanya kazi za umma chini ya usimamizi wa serikali za vijiji .kulikuwa hakuna cha huyu ni mheshimiwa wote mnakuwa sawa kwenye kazi ,wale wasio hudhuria kazi hiyo kuna mgambo wa kijiji hupita nyumba hadi nyumba kumsaka baba ,ambaye wakati huo huwa amejificha darini .wale askari wakimkosa hukimbiza kuku na kumpeleka ofisi ya kijiji kama fidia ya kutokuja kufanya kazi .hapo namuona mwalimu aliitikia wito wa kufanya kazi .kazi hiyo huchukua masaa 2 hadi 3 kutegemea ni kazi gani ..
[QUOTE=Unajenga huku umevaa suti na suti yenyewe ya kupewa,kaziii kweli kweli
Tofauti kubwa kati ya picha hizi ni kwamba, hiyo picha ya chini ilipigwa ENZI ZILE AMBAZO VIONGOZI WOTE WALIKUWA WANAITWA NDUGU na hiyo picha ya juu imepigwa kipindi hiki ambacho kila kiongozi hadi wa Mbio za Mwenge WANATAKA KUITWA WAHESHIMIWA!!!
Kituko kwenye picha ya pili askari anatembea tu wakati Rais amebeba mawe! Kimaadili hii inakubalika kweli? Askari unaangalia bosi wako anabeba mzigo halafu wewe hubebi?
Picha ya juu anaekti kama anajenga (akiwa ndani ya suti na walio mzunguka nao wanaekti). Picha ya chini anawapaka walalahoi mafuta kwa mgongo wa chupa kwa kujitia naye ni sawa nao kumbe ............ i.e picha ya chini ni msanii zaid kwani pamoja na kuekti anajenga lakini amejivisha ulalahoi ili kuteka nyoyo za wasioona upande wapili wa shilingi.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.