Kuna tofauti gani kati ya pin na password?

PIN, (Personal Identification Number) ni safu ya namba zinazotumiwa kuthibitisha kitambulisho. PIN ni namba tu (mf. 1234), na hazina herufi wala alama. Hizi hutumiwa hasa kwenye kadi zako za ATM, kuruhusu ununuzi ukitumia programu. Mara nyingi huwa ni fupi tu – kuanzia idadi ya tarakimu 4 hadi 6.

PASSWORD ni kama kufuli la kulinda mambo yako binafsi. Tofauti na PIN, PASSWORD inaweza kuwa na herufi kubwa na ndogo, namba na alama. Kwa kawaida PW ni ndefu kuliko PIN.
 
Back
Top Bottom