Kuna tatizo gani bandarini na wafanyabiashara wa Congo?

Mkuu naona unaliongelea hili swala upande mmoja....serikali inakosa mapato kwenye transit pale mfanyabiashara anapofanya ujanja mzigo Wa transit unapoishia hapa hapa nchini

Sent using Jamii Forums mobile app
Sijakataa serikali kusimamia transit cargo na hasa ukijua kuwa kuna wafanyaibiashara wengine sio waaminifu, ninachosema ni juu ya kuongeza gharama ,na hasa unapomtaka mteja tena alipe extra money,uwekwe mfumo mzuri ambao si lazima mteja alipe la km suluhisho ni escort basi Tra imlipe si yuko kazini?
 
wafanyabiashara ni wajanja sana, ndio maana siku hizi kila lori unalo liona mengi yao yanakuwa na customs officer analisindikiza mpaka mpakani, vile vingamuzi vya kutrack mizigo wafanyabiashara wamekuwa wakivichezea
escort charge zinaongeza gharama ndio, ila lazima serikali ilinde mapato yake

Lichaguliwe swala moja tu kati ya king'amuzi au usindikizaji,haipo haja ya mfanyabiashara kulipia vyote viwili kwa pamoja.
 
Mimi hakuna kitu nachukia kama ubabaishaji kwenye biashara. Bandari yetu inabidi ifumuliwe na kusukwa upya. Kweli wabongo ni vigumu sana kuendelea kwa namna hii. Ningekuwa rais ningetupa wao washenzi baharini.
Ifumuliwe na kusukwa mara ngapi??
 
wafanyabiashara ni wajanja sana, ndio maana siku hizi kila lori unalo liona mengi yao yanakuwa na customs officer analisindikiza mpaka mpakani, vile vingamuzi vya kutrack mizigo wafanyabiashara wamekuwa wakivichezea
escort charge zinaongeza gharama ndio, ila lazima serikali ilinde mapato yake
hapa lazima tufikirie sana, kama kila lori litakuwa na escotter wa TRA, duuh hii ni ujima hakuna njia za kisasa kutrack?!? kama SUMATRA wanaweza kutrack speed za mabasi nchi nzima TRA wanafeli wapi?, kama kuna car tracker tunashindwaje kutrack mzigo wa transit?. Hebu tujiongeze buana dunia hii ina tecknolojia nyingi sana.
 
Kwa kweli hali ni mbaya kwa hawa wafanyabiashara jirani zetu, Tra kazi yao ni kufacilitate process nzima ya mzigo wa transit ili ucross border husika , kuanzia pale hao customs wengine wanaendelea, kwetu ni kinyume, TRA anataka kuchukua ushuru hata kwa transit cargo, hii si sahihi, nitoe mfano,

Kuna hili zoezi la escort kwa mizigo ambayo wao wanaita ni sensitive, hatukatai,ila tangazo lao halijasema ni mzigo kiasi ndio uwe na escort, je ni pkg 10 au ni container nzima? haingii akilini una contr yenye pkgs 1000, ila pkg 5 tu zina ctn za betri unasema lazima nilipe escort, hii haijakaa sawa, isitoshe, hizi contr za transit tuna fix tracking seal ambazo wao ndio wanacontrol.

Sasa kazi yake nini?tunawaongezea gharama zisizo kua na msingi wowote, tusijidanganye, itafika mahali tutawakosa hawa watu, wao wanaangalia factors nyingi km tuko expensives wata opt kwenda Port zingine, tutabaki tunaangaliana tu na kutoa lawama, kuondoka ni rahisi sana ila kumrudisha itachukua muda mrefu sana. Ushauri wangu kwa TRA swala la escort liondolewe kabisa tayari kuna tracking seal watu wao wafanye kazi kama inavotakiwa na si kuimpose sheria ambazo ni burden hasa kwa mizigo ya transit.
Mkuu nakuunga mkono kwahili, watu wengi hawajui kuna garama nyingi sana zipo port, na wafanya biashara wa transit ni kati ya kiungo muhimu sana kwa mamlaka ya bandari yetu, kuna mahali tukipakosea tutakuja pajutia lakini muda utakuwa umekwenda.Handling,Wharfarg,kingamuzi,na garama za usafirishaji tunazibadi kila mara mafuta yanapo pandishwa bei hivi vyote anabeba mwenye mzigo na container ikichelewa kutoka stooreg ni yake tena. Kunahaja yakuangalia kwa kina wapi tunakosea kwakweli,Beira anatutizama kwa jicho la wivu akiwapunguzia baadhi ya garama na uslama ukiwa mzuri,Malawi,Zambia, DRC katanga hatuwaoni tena litakuwa pigo kuu sana kwetu, mamlaka husika tunawaomba walichukulie yhili jambo kwa kina sio lakulipuuzia kwakwe. Nakumbuka serekali iliyo pita ilipata changamoto kwa Rwanda lakini hekima ikatumika wanalipa road toll 152$ kama sisi tunavyo lipia kwenda kwao nijambo lakuliangalia kwa kina,hekima,busara,na weledi mkubwa sio kiburi.
 
Asanteni wadau kwa maonimuhimu sana ambayo yanaweza kutupeleka mahali katika kukuza uchumi wetu naomba basi mamlaka husika wayaangalie maoni ya wadau hawa waliochangia ili tuinusuru bandari yetu kwa ukuwaj wa uchumi wetu asanteni sana
 
lakini tatizo hasa ni nini kwanini tusiweke wazi naimani wakubwa pia wanapitia humu jf wanaweza wakachukua mawazo yetu yakafanya kazi pia
Shida kubwa kwa taasisi za Tanzania hua hawatoi taarifa hadharani juu ya utaratibu fulani yani mpaka ufikwe na tatizo ndo wanakuelezea utaratibu mfano ukitaka kutoa msaada wa kitu chochote kama hivyo vitu unavyotaka kuvitoa vinatakiwa kulipiwa ushuru utatakiwa kua na barua za msamaha wa kodi toka wizara ya afya sasa kama haufahamu utafahamishwa siku utakayokua na huo mzigo na siku ambayo unataka kuutoa huo mzigo
 
Ndugu wana JF wiki sasa nasikia minong'ono wafanyabiashara wa congo wanalalamika mizigo inachelewa wanaingizwa gharama zisizo na umuhimu mara escot mara stripping hapana bial maandalizi hivi mbona inatokeaga mara kwa mara tuna wa discourage.

Hawa wadau wakubwa wa bandari yetu badala ya kuweka mazingira rafiki ili washawishiane kuja kwa wingi bandari ya dar? viongozi tuliangalie hili kwa jicho la tatu maana macho haya mawili naona hayakidhi kuona usumbufu unaotokea bandarini kumpata mteja nikazi ngumu sana.

Lakini kumpoteza ni dakika tu anahama tumesha invest vya klutosha kuiweka bandari katika ubora sasa tuangalie tusije kuwa tumepoteza gharama za bure, tuna hamu kufika kuwa taifa lenye uchumi wa kati hapo ndipo tuta enjoy matunda ya nchi

nawasilisha
Bandari yenyew tu haijakaa kimataifa imekaa kitaifa zaidi
Wenzenu wana birth 22 we una kumi tu..kichekesho kweli

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bandari ni ugonjwa wa kisukari kwa serikali kila mkurugenzi anaewekwa hpo anakua mzuri kiutendaji dakika kadhaa, baadae na yeye anakua sehem ya Matatizo ya Bandari nchi hii kila sehem mpka Rais afanye ziara za kushtukiza, Watendaji ni kama vile watu walioko usingizini, Serikali ya Congo imesema inahamishia mizigo yake Mombasa, TRA ndio mchawi wa serikali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Please Please Tanzania Yangu,tukiweza kuwashawishi wafanya biashara wa DRC na serikali yao kupitishia bidhaa zao kwenye bandari zetu ,tutakuwa sawa na kumiliki visima vya mafuta,tatizo letu wengi wetu tunaangalia matumbo yetu na sometime mada muhimu kama hii tunaingiza siasa,ni muhimu tutambue kuwa DRC ina uwezo wa kuivuta nchi yetu kwenda mbele,na sio siri wengi wao wameamua kupitishia mizigo yao Walvis Bay,Durban na ndio sababu hii Zambia imejenga barabara nzuri sana kutoka Livingstone hadi few kms before Lusaka,wana mpango wa kujenga upande wa pili wa barabara kutoka Lusaka hadi Kabwe,Kapiri Mposhi imerekebishwa sana na road tolls zao ni classic,sisi bado tumelala na tutakapo amka biashara zote za DRC ZIMESHAHAMA,(kwa makusudi mazima Zambia imepuuzia kabisa ujenzi wa barabara yao ya kutoka Mpika hadi Nakonde(border na sisi na matokeo yake zile 300kms imekuwa njia za farasi,wenye mizigo kutoka DRC wanakwenda kusini sio kuja kwetu huku ambako ndio karibu zaidi;reality tukiikosa DRC TUMEKWISHA,mizigo ya Rwanda ni upuuzi mdogo ambao hta bandari ya kilwa inamudu kuhudumia.
 
Kazi za kutoza ushuru wangewapa kampuni kama serekali iangalie tu mambo ya ukaguzi na kupata pesa safi isio na figisu kampuni haiwezi kufanya makosa na pato litaonekana watanzania wengi sio wafanisi wakiajiriwa na serekali direct.
 
Bandari ni ugonjwa wa kisukari kwa serikali kila mkurugenzi anaewekwa hpo anakua mzuri kiutendaji dakika kadhaa, baadae na yeye anakua sehem ya Matatizo ya Bandari nchi hii kila sehem mpka Rais afanye ziara za kushtukiza, Watendaji ni kama vile watu walioko usingizini, Serikali ya Congo imesema inahamishia mizigo yake Mombasa, TRA ndio mchawi wa serikali

Sent using Jamii Forums mobile app
Tunawashukuru wote humu ndani kweli hili jukwaa kiboko, Serikali imefyekelea mbali changamoto zote za transit cargo, hii ni kwa mujibu wa taarifa ya Waziri mwenye dhamana, BIg up.
 
Bandari yenyew tu haijakaa kimataifa imekaa kitaifa zaidi
Wenzenu wana birth 22 we una kumi tu..kichekesho kweli

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu hata tungalikuwa na birth nyingi hatuna uongozi madhubuti kwakweli ukifanya kazi mle ndani ndio utajua nasema nini, jamani kuna vitu vinafanyika vyaajabu sana bandarini chakushangaza wale viongozi wako kama wametia pamba masikioni,inasikitisha sana hata ile kazi wanafanya ya kusafisha na kuongeaza kina ni kazi bure kwa muundo wa viongozi tulio nao inasikitisha sana utawala mbovu sana kwakweli mamlaka ya bandari tz.
 
Bandari ni ugonjwa wa kisukari kwa serikali kila mkurugenzi anaewekwa hpo anakua mzuri kiutendaji dakika kadhaa, baadae na yeye anakua sehem ya Matatizo ya Bandari nchi hii kila sehem mpka Rais afanye ziara za kushtukiza, Watendaji ni kama vile watu walioko usingizini, Serikali ya Congo imesema inahamishia mizigo yake Mombasa, TRA ndio mchawi wa serikali

Sent using Jamii Forums mobile app
Wanawaza matumbo yao mdau.....pale pesa za bwerere ni nyingi sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
aisee mkuu unamaono sana ya kuijenga nchi yetu tatizo lingine jamani mkuu wa nchi kama ingekuwa inawezekana siku moja angepanga aongee na watu wanaitwa CLEARING AND FORWARDING AGENTS hawa watu ndiyo wana kumbana na matatizo yote yanayohusu bandari wanajuwa kila kitu akifanya mikutano na tra wanampotosha hata kaa ajue tatizo liko wapi maana mambo mengi watamficha mkuu naomba kama kuna mtu anaweza kumuambia mkuu wa nchi aongee na hawa watu kupata mawazo ya nini kifanyike kuinusuru badari yetu
 
Back
Top Bottom