Adui mwingine Mkuu wa maendeleo ya Biashara nchini Tanzania ni huyu hapa

kijangwajunior

New Member
Jun 9, 2019
1
1
Utangulizi

Heko Mpendwa wetu Daktari JPM, Huu ni mchango wangu kwa Taifa langu, ambao ni imani yangu kuwa nautoa kwa muda mahususi na kwa Mtu mahususi aliyeteuliwa na Mungu kulivusha Taifa lake la Tanzania kutoka katika maisha ya ufukara, udhalili, utapeli wa kisiasa na kiuchumi na unyongwaji wa haki za Wanyonge.

Wasifu wangu

Mhe. Rais wetu, naomba upokee wasifu wangu fichi wenye nia na makusudi ya kutoa msaada wangu wa dhati katika kipindi ambacho Watanzania wenzangu wameanza kuuelewa msimamo na muelekeo wako na Serikali unayoiongoza. Moyo Huu umevutwa na hisia za ukweli, uthubutu na uzalendo ulioonyeshwa na Wafanyabiashara wazalendo kwenye kikao kilichofanyika Ikulu ya Dar es salaam kwa mwaliko wako binafsi, imenigusa Mhe. Rais mpaka nikatamani ningehudhuria kikaoni hapo nitoe dukuduku langu na la Watanzania kwa ujumla.

Nilianza kufanya biashara ndogondogo jijini Mwanza mwishoni mwa Mwaka 1993, nilifanya biashara za mitumba kwa muda mwaka mmoja na kisha nilianza kununua dagaa safi za Chakula na kupeleka Congo, kipindi hicho biashara hii ilikuwa inalipa sana hivyo Mtaji wangu ulikuwa kwa haraka sana mpaka nikajikuta naongeza mradi mwingine wa kununua mazao kama Kahawa mkoani Kagera na Mpunga Shinyanga na Sengerema. Katika kipindi hicho biashara ya magendo ya Kahawa kutoka Kagera kwenda Uganda ilikuwa inatengeneza faida kubwa hivyo watu wengi waliikimbilia na ndiyo wakati huo mimi niliiacha kwa sababu nilijiapiza kwamba sitafanya biashara ya kilaghai kwa mujibu wa imani yangu ya Kiislamu kwa kuwa nikifa nitaulizwa chanzo cha mali yangu. Baada ya hapo nilianza biashara ya usafirishaji wa mizigo kwa Malori makubwa na nikafungua kampuni ya Clearing and Forwarding biashara ambazo naendelea nazo hadi leo.

Kutokana na kutokuwa na kazi yoyote zaidi ya biashara, nikajikuta nikiwa na uelewa makubwa juu ya masuala ya biashara, changamoto, fursa na utatuzi wa mambo mbalimbali ya kibiashara. Ni uzoefu huo nitakaoutumia kutoa ushauri wangu mdogo Mhe. Rais wangu.

Adui Mwingine Mkuu wa Maendeleo ya Biashara Nchini


Mhe. Rais, ni ukweli kwamba kuna vikwazo vya Maendeleo ya biashara yatokanayo na Wafanyabiashara pamoja na taasisi za serikali, hata hivyo yatokanayo na Wafanyabiashara yanachangia zaidi ya 60% wakati yale ya taasisi za Serikali yanachangia kama 40%. Hii ni kutokana na kila mfanyabiashara kujaribu kutumia mwanya wowote upatikanao kukwepa au kulipa kodi pungufu iwezekanavyo.

Wakati nafuatilia mkutano wako na Wafanyabiashara wenzangu nilisikia malalamiko dhidi ya OSHA, TANESCO, TRA, NEMC nk. Hawa wote walikosa kutaja taasisi moja muhimu sana kinagaubaga, taasisi ambayo baadhi ya jirani zetu wanatamani wangemiliki taasisi kama hiyo, wangefanya maajabu katika maendeleo ndani ya muda mfupi.

Mhe. Rais taasisi yenyewe ni bandari yetu (TPA) ikiongozwa na Mkurugenzi wake mkuu Engineer Kakoko. Ukweli ni kwamba takriban kwa awamu zote zilizopita bandari ilikuwa imekufa na kuoza, kila mtumishi wake aligeuka tajiri mkubwa ndani ya muda mfupi sana kutokana na Rushwa na Ufisadi uliopitiliza huku serikali ikiambulia masalia kidogo tu.

Ulipoingia madarakani Mhe.Rais bandari ilianza kupata mabadiliko makubwa na Chanya na ni imani yangu kwamba hata mapato yatokanayo na bandari yatakuwa yameongezeka mara dufu, hii imempa sifa kubwa Bw. Kakoko kwa kudhaniwa kwamba yeye ndiye chanzo cha mabadiliko makubwa ya TPA. Ukweli Mhe. Rais ni kwamba watumishi wa bandari wamebanwa kutokana na macho mengi yaliyojaa bandarini hususan kutokana na vijana wako kutoka vyombo vya ulinzi na usalama kama jeshi, TDA, TBS nk na siyo uongozi wa Ofisini wa Mheshimiwa Kakoko. Kazi anayoifanya ingeweza kufanywa na mtu yoyote kutokana na kuwa na watu sahihi kwenye shughuli za kila siku zikiwemo za kimapato bandarini.

Pamoja na wasifu mzuri wa kitaalam na kitaaluma wa Kakoko na kufanya kazi nyingi peke yake kwa juhudi kubwa, ni vema Mhe. Rais ukafahamu kwamba mtu huyu kaigawa taasisi hii muhimu, ametengeneza kakikundi kadogo ka vijana watiifu kwake, Hawa anawatumia kama mashushushu wake, ingawa hata wao akishawatumia vya kutosha anawageuka na hata kuwahamishia bandari nyingine zisizo na kazi nyingi. Hii imeibadilisha taasisi hii muhimu kuwa kama kijiwe cha majungu. Mhe.Rais usione utendaji mzuri wa bandari kwa nje kwa ndani kuna moto mkubwa unafukuta.

Mheshimiwa Kakoko amejilimbikizia madaraka yote kama vile TPA ni kampuni yake binafsi, haamini utendaji wa Mkurugenzi hata mmoja wala Meneja na hivyo wakurugenzi wake wote na Mameneja ni wa majina tu. Ana kauli za matusi na kejeli kwa watumishi heri ukafanye kazi kwenye duka la Mhindi (naomba radhi, kauli hii siyo ya kibaguzi bali ni mfano). Ana dharau kila mtu, awe mkubwa au mdogo hata kama ni mtaalam kwenye eneo husika. Hali hii imewalazimisha baadhi ya watumishi wenye uwezo na msaada na nchi hii kuacha kazi ili wamuachie gurudumu lake, na waliobaki hawana kauli hata kwenye maeneo yao ya kitaalam zaidi ya kumsikiliza na kufanya anachotaka yeye hata wakijua kitaalam anakosea, na wengi wanamuacha makusudi akosee ili atumbuliwe hivyo amefanya makosa mengi ajabu ambayo hayawezi kuonekana mpaka akitoka. Mheshimiwa Kakoko ni mtu mzuri kwenye kujieleza, akiongea na wewe unaweza kudhani ni Mzalendo namba moja lakini ni kinyume chake.

Ni wazi na kweli kwamba Mheshimiwa Kakoko siyo mpenda Rushwa, anachukia ufisadi na ni mfanyakazi hodari sana, tatizo lake ni mlevi wa madaraka, hana utu kwa wenzake na amejitengenezea umungu mtu. Hata wale suppliers wa vitu mbalimbali bandarini anayeamua apate anapata na asiyetaka asipate hapati na hata anayepata yeye anaamua nani alipwe nani asilipwe. Hii inafanya taasisi hii kuwa na rundo la madeni yasiyolipwa kwa wakati na ilihali fedha za kuwalipa zipo na bila sababu za mashiko za kufanya mambo hayo.

Mhe. Rais naomba niwasilishe haya machache sana kwenye mengi ninayoyajua, siwezi kuandika kila kitu hapa kutokana na kwamba heshima ya nchi na viongozi wetu ni muhimu kutunzwa kwa gharama yoyote, na kuendelea kutoa kila kitu hapa kunaweza kusababisha heshima za watu kuguswa. Ni imani yangu kuwa tuna taasisi zinazoaminika duniani kote kufanya tafiti na kutafuta taarifa za siri, imani yangu ni kwamba zikitumika zitakujuza mambo mengi kuhusu huyu mtu ambaye anaharibu taswira mzuri ya Serikali yetu na taasisi yetu muhimu. Mhe.Rais wangu, kutokana na kwamba nchi yetu hii baadhi ya watu huongozwa na chuki na husda hata kufikia hatua ya kuwasingizia watu wenye kuchapa kazi na kutimiza wajibu wao ipasavyo kwa malengo waondolewe ili wao wafanikishe malengo yao, ili nisiingie kwenye dhambi ya kumsingizia mtu kwa hila, nakuomba Mhe. Rais wangu utumie vyombo vyako ili vikusaidie kuthibitisha haya niliyoyaeleza hapa.

Naomba nikushukuru na nikupongeze Mhe. Rais hususan kwa kuendeleza uhuru wa kujieleza wenye tija kwa taifa, ndiyo sababu hii leo nimeamua kwa mara ya kwanza kutengeneza akaunti yangu jamiiforums ili nitoe dukuduku langu kama walivyofanya wafanyabiashara wenzangu pale Ikulu nikiwa na imani litakufikia. Nichukue tena fursa hii kumshukuru Bw. Mello kwa kunikutanisha na Mhe. Rais wangu kupitia teknolojia.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu mbariki mtetezi wetu, Rais wetu Mhe. Daktari John Magufuli. Tunakupenda Sana.
 
Ulianza vzr kuelezea lkn mwishoni umekosa hoja ya kunishawishi kuwa huyo bw. Kakoko ni mbaya au hafai.
Kwa sababu umekiri mwenyewe kwamba bandarini paliharibika halaf unataka bw. Kakoko atumie utu.
Hapo akitumia utu wa kawaida maana yake patarudi kuwa Kama zamani Sasa ili panyooke inatakiwa huo utu ukae pembeni kila mtu achape kazi kilazima na sio kubembelezana Kama zamani.
 
Mimi namshauri tu huyo "Kakoko" kuendelea hivyo hivyo ili kuwabana wakwepa kodi na wapiga dili wote hapo bandarini. Uzuri umekiri mwenyewe kwamba huyo "Kakoko" hapendi mambo ya rushwa na ufisadi! Hivyo jitahidi tu kufuata sheria na usitegemee Magufuli kumbadili na kumteua mtu mnayemtaka nyinyi.
 
Mimi namshauri tu huyo "Kakoko" kuendelea hivyo hivyo ili kuwabana wakwepa kodi na wapiga dili wote hapo bandarini. Uzuri umekiri mwenyewe kwamba huyo "Kakoko" hapendi mambo ya rushwa na ufisadi! Hivyo jitahidi tu kufuata sheria na usitegemee Magufuli kumbadili na kumteua mtu mnayemtaka nyinyi.
Ndio nilichokiwaza mm mkuu.
Inaonekana zaman walikuwa wanatumia njia za shortcut Sasa milango hyo imefungwa wanaanza kulalamika.
 
Bwana kakoko piga KAZI Tena aongeze ukauzu nyie watu wa bandari mlituchezea vya KUTOSHA....KAZI mlikua mnapeana kwa kujuana,. Japo Hadi saiv mnapeana KAZI


Majuz zilitangazwa Kaz ila kwa akili ya kawaida mtu huwezi kuomba coz sifa za muombaji ziliwekwa dhaifu Sana ukiangalia kwa jicho la tatu unaona kabisa wameandaa mazingira mazur kwa watu wao kupenya bila kipngamizi


Leo hii seaman mwenye utimamu hawezi kuaply TPA coz anajua ni kupoteza muda wake tu
 
Bwana kakoko piga KAZI Tena aongeze ukauzu nyie watu wa bandari mlituchezea vya KUTOSHA....KAZI mlikua mnapeana kwa kujuana,. Japo Hadi saiv mnapeana KAZI


Majuz zilitangazwa Kaz ila kwa akili ya kawaida mtu huwezi kuomba coz sifa za muombaji ziliwekwa dhaifu Sana ukiangalia kwa jicho la tatu unaona kabisa wameandaa mazingira mazur kwa watu wao kupenya bila kipngamizi


Leo hii seaman mwenye utimamu hawezi kuaply TPA coz anajua ni kupoteza muda wake tu
Tena ilitakiwa waongezeke wengine watano Kama yeye ili watu wanyooke.
 
In short Hugo boss waTPA Yuki njema. Wabongo sio wakuchekea utatumbuliwa unawaacha wanakucheka.
Abane ivo ivo
 
Huyo kakoko kawekwa na nani??? Unajuaje hayo yote anayofanyA sio matakwa yake bali ni ya aliemuweka
 
Back
Top Bottom