Kuna shida gani kwenye hii kozi ya Clinical Medicine siku hizi?

Afisa Tabibu

JF-Expert Member
Oct 29, 2021
484
799
Clinical Medicine ndo kozi ya Afya ngazi ya vyuo vya kati inayoongoza kuchukua wanafunzi wengi, lakini ndo kozi inayoongoza wanafunzi kufeli, nimepitia data za vyuo vitano nchini, nimeshtuka kidogo;

Chuo A, mwaka wa 1 walidahiliwa wanafunzi 217, waliomaliza mwaka wa 3 ni 42.

Chuo B, waliodahiliwa mwaka wa kwanza 183, waliomaliza mwaka wa 3 ni 29.

Chuo C, waliodahiliwa mwaka wa 1 ni 160 waliomaliza mwaka wa 3 ni 18

Chuo D, waliodahiliwa mwaka wa 1 ni 116 waliomaliza mwaka wa 3 ni 52

Chuo E, waliodahiliwa mwaka wa 1 ni 98 waliomaliza mwaka wa 3 ni 30.

Kwa mwendo huo hapo juu unaweza ona kabisa kuna shida sehemu, either wanafunz vilaza au Walimu sio bora, ni kozi ya ajabu, kuna mzee ana mtoto wake huu ni mwaka wa 6 ndo yupo mwaka wa 3 sasa, na ni wengi tu kama yeye.

Shida ya kozi hii ni nini hasa hadi imekuwa ngumu sana kumaliza straight ndani ya miaka 3 iliyopangwa?
 
Clinical Medicine ndo kozi ya Afya ngazi ya vyuo vya kati inayoongoza kuchukua wanafunzi wengi, lakini ndo kozi inayoongoza wanafunzi kufeli, nimepitia data za vyuo vitano nchini, nimeshtuka kidogo...
Ni mengi yanayochangia..safari ya maisha ina misukosuko mingi.

Kuna kokosa ada
Kudisko
Kuhama chuo
Kuolewa na kuzaa
Kufreez
Kufariki
Kuugua magonjwa
Kuhama nchi.

Na mengine mengi.

Life halijawahi kuwa static.

#MaendeleoHayanaChama
 
Clinical Medicine ndo kozi ya Afya ngazi ya vyuo vya kati inayoongoza kuchukua wanafunzi wengi, lakini ndo kozi inayoongoza wanafunzi kufeli, nimepitia data za vyuo vitano nchini, nimeshtuka kidogo;

Chuo A, mwaka wa 1 walidahiliwa wanafunzi 217, waliomaliza mwaka wa 3 ni 42.

Chuo B, waliodahiliwa mwaka wa kwanza 183, waliomaliza mwaka wa 3 ni 29.

Chuo C, waliodahiliwa mwaka wa 1 ni 160 waliomaliza mwaka wa 3 ni 18

Chuo D, waliodahiliwa mwaka wa 1 ni 116 waliomaliza mwaka wa 3 ni 52

Chuo E, waliodahiliwa mwaka wa 1 ni 98 waliomaliza mwaka wa 3 ni 30.

Kwa mwendo huo hapo juu unaweza ona kabisa kuna shida sehemu, either wanafunz vilaza au Walimu sio bora, ni kozi ya ajabu, kuna mzee ana mtoto wake huu ni mwaka wa 6 ndo yupo mwaka wa 3 sasa, na ni wengi tu kama yeye.

Shida ya kozi hii ni nini hasa hadi imekuwa ngumu sana kumaliza straight ndani ya miaka 3 iliyopangwa?
Sasa hapo unaambiwa kuwa wapo wengi mtaani Kama walimu
 
Sababu kila mwanafunzi mbovu anatafuta short cut ya kuwa daktari kwa kusoma hio sijui mnaita clinical medicine mara clinical ofisa,
Mmetuchosha na siredi za clinical medicine....

1653482589477.png
 
Nchi ninayoishi hakuna wababaishaji hao wanaitwa CO
Ni madaktari kwa kwenda mbele yaani na manesi wa huku wamewezeshwa hasa na MSc/PhD ya Nursing na wanaruhusiwa kumuona mgonjwa awali na kabla ya Dr
Hakuna elimu ya kuungaunga kwenye fani ya afya
Nipe tofauti kati ya CO na daktari kimajukumu?
 
Mtaala wa Elimu ya clinical medicine ni Mgumu sana,kozi ya clinical medicine imeokoa taifa kwa sehemu kubwa sana,kwa sababu ukifatilia kwenye dispensary au vituo vya Afya ambako ndo kuna idadi ya kubwa ya watu!! Wao ndo watu wa kwanza kuwaona na kuwati u wagonjwa.....wao ndio wanatibu idadi kubwa sana ya watu,wao ndo mara nyingi hata kwenye hospital kubwa wanapangiwa shift za uck kuwaona wagonjwa....
Ila kukitokea dharura kubwa au mgonjwa anahitaji upasuaji mkubwa au mgonjwa ana shida kubwa sana!! Ndipo Daktari mkuu (second on call) anapigiwa simu otherwise km ni kwenye dispensary Daktari hayupo!! Ndipo wanatoa rufaa....kwenda hospital kubwa kwa uangalizi zaidi na matibabu zaidi!!

Hali ya kiuchumi kwa Sasa hivi ni ngumu,kiac kwamba Ni ngumu kuajiri madaktari tupu!! Au ma specialist tupu kwa sababu ya gharama ya kuwalipa ....

Mfano!! Uwaajiri ma Dr 10 kwenye kituo chako,kwa mwezi max uwaandae utleast mil 16 kuwalipa,pia Kuna matumiz mengineyo na ma nurse nk!

Wakati ma CO 10 kwa mwezi waweza ukawa na utlest mil 5 kwa mwezi (km ni mkataba wa laki 5) na wakafanya kazi kama wanazofanya ma Dr wakawaida tena kwa kiwango kikubwa....(shift ndefu) mf matibabu ya malaria,UTI,typhi, Diarrhhea, sinusitis,skin disease,, peptic ulcers, constipation nk ambayo ni common, magonjwa makubwa km cancer na mengine kwanza ni machache kutokea (huenda hata kwa wiki au mwezi akapatikana client mmoja) lakini pia hata akiwepo Dr kwenye kituo kidogo,pia hataweza kufanya matibabu kwa sababu ya vipimo,na dawa...lazima nae atoe rufaa kwa hospital kubwa

Kwanini CO wanafunzi wengi wanafeli, ??
Mtaala wao ni Mgumu sana,na karibu kila mwaka unabadirishwa badirishwa,mfano mwanafunzi mwaka wa kwanza asome masomo 6,then pia kila SoMo limegawanyike sehemu mbili... theory na practical (jumla ni masomo 12)
Mwanafunzi aingie Darasani kusoma!! Them mwanafunzi huyo anatakiwa akashinde hospital kujifunza practical then atafute muda wa ziada ajisomee!!

Cha ajabu Zaid, mitihani ya mwisho yoote inatungwa na wizara ya Elimu (NACTE) ni kama vile mitihani ya form 4 inatungwa na nacte,

So, inawezekana mwalimu concept aliyowapa ni nyingine,may be kutokana na uzoefu wake kazini.....lakini NACTE wanatunga wao,na marking scheme zao!! Unahic watoto watafaulu??? Na kwanini kozi nyingine za Diploma kama IT au uwalimu,au secretary mfumo wao ni tofauti na huu??? Me cjui...
Unahic mfumo Ungekuwa sawa na kozi zingine wangefeli sana??

Kitu kingine,
Wanasoma mambo mengi sana.... tofauti na wengi wanavyofikiria!!
Mfano!! Mwaka wa Tatu...
SoMo la pediatric...Lina topic 27
SoMo la forensic Medicine...topic 22
Surgery....topic zaidi ya 20
Internal medicine zaidi ya 26
Gyna na obsy .....topic zaidi 25
SoMo la

Then ukiwa mwaka wa Tatu,inabidi usome masomo yoote ya mwaka wapili...kila SoMo Lina topic zaidi ya 20

Pia upate muda wa kwenda field,kwenda hospital,
Semister kawaida Ina miez 4
Halafu hapo hapo madogo wameambiwa mitihani itawahi?? Ety kwa sababu ya sensa.....

Unahic wata compsate vp muda????
Akili kichwan.....??

Wanaofeli na kushindwa kumaliza,ni wengi zaidi .. tofauti na inavyokisiwa!! Me mwenyewe nimeshuhuduia au pengine nilikwepo kwenye hiyo field! Ila problem pia hakuna statistics zinazokusanywa na wizara ..watu wangapi wameshindwa kufanya mitihani au kuendelea na kwa sababu zipi???

Nahic kwa Sasa takwimu na research,zitakuwa hazina faida kwao,zikiwa na umuhimu watatafuta....na ku review mtaala wa Elimu upya...kwa upande wa CO......

Kwa Sasa tuwaache kwanza,waendelee kufeli
 
Tofauti ya kimajukumu ni hivi..

Daktari - Alipasua PCB ya O level na Advance...
Daktari - Miaka mpaka 6 kuwa Daktari kamili...
Anafundishwa:
Kudadavua magonjwa- kwa kutumia vifaa tiba vyote, kama Ultrasound, CT, MRI, X ray, na vinginevyo vingi tu kama ECG, EEG, ERG, EMG yaani Daktari anafundishwa kujua kila kifaa kinachotumika kudadavu na kuchakachua magonjwa...mpaka atakapoamua ku specialize awa mbobezi kwenye utaalamu gani..lakini anajua yote...anatakiwa ajue nyanja za Radiologist zote
Usifananishe Radiographer na Radiologist,..Radiographer ni mpiga picha za tiba na Radiologist ni Diagnostic Doctor...

Kutibu magonjwa - Daktari anaenda kufundishwa fani za ziada kama Pharmacology ya jinsi dawa inavyofanya kazi mwilini, hii ni fani ya wasomi tofauti na kazi zao, lakini Daktari kamili lazima ajue haya...

Daktari - anafundishwa kufanya upasuaji, yaani Surgery operation, japo hatakiwi kufanya zile ambazo ziko zaidi ya viwango vya kitaaluma kama kupandikiza viungo...unless amesomea kuwa Specialize Surgeon..

Daktari - Anasomea utaalamu wa kuyafuatilia magonjwa na jinsi yanavyoongeza au kupungua(Monitoring)

Na hii list ya majukumu ya Daktari ni ndogo sana niliyoleta hapa, ningejaza kama siredi mbili au tatu .....

CO - Alikuwa kilaza fulanI wa Biology, Physics, Maths na Chemistry kwa O level na Advance..
CO - Miaka 3 ya masomo tu anataka kunichunguza Cancer...huu ni ulozi...
CO - Ni upuuzi mtupu, sieendelei na huyu imetosha hapa...
Wee huna akili ya kufaulu CO,kwa uwezo wako tu inavyoonekana ulifeli shule
 
Nisomee CO....🤣🤣🤣

Mkimaliza kusoma hio, mnatakiwa mpangiwe vijiji mkasaidie huko, sio mnataka na kupigana vikumbo na madaktari kwenye hopitali za rufaa...eti na wewe unataka title ya Dr 🤣🤣🤣

Mimi nimesomea Engineering na nina heshimu sana mtu aliyesomea na kuwa udaktari kamili, hata kama alisomea nchi za kimasikini.....Udaktari ni level nyingine......sana tu...
 
Sorry can I get ur numbers coz I want to take the same course and I could use some advice
 
Nisomee CO....

Mkimaliza kusoma hio, mnatakiwa mpangiwe vijiji mkasaidie huko, sio mnataka na kupigana vikumbo na madaktari kwenye hopitali za rufaa...eti na wewe unataka title ya Dr

Mimi nimesomea Engineering na nina heshimu sana mtu aliyesomea na kuwa udaktari kamili, hata kama alisomea nchi za kimasikini.....Udaktari ni level nyingine......sana tu...
Injinia Tanzania au kibarua wa wachina
 
Tofauti ya kimajukumu ni hivi..

Daktari - Alipasua PCB ya O level na Advance...
Daktari - Miaka mpaka 6 kuwa Daktari kamili...
Anafundishwa:
Kudadavua magonjwa- kwa kutumia vifaa tiba vyote, kama Ultrasound, CT, MRI, X ray, na vinginevyo vingi tu kama ECG, EEG, ERG, EMG yaani Daktari anafundishwa kujua kila kifaa kinachotumika kudadavu na kuchakachua magonjwa...mpaka atakapoamua ku specialize awa mbobezi kwenye utaalamu gani..lakini anajua yote...anatakiwa ajue nyanja za Radiologist zote
Usifananishe Radiographer na Radiologist,..Radiographer ni mpiga picha za tiba na Radiologist ni Diagnostic Doctor...

Kutibu magonjwa - Daktari anaenda kufundishwa fani za ziada kama Pharmacology ya jinsi dawa inavyofanya kazi mwilini, hii ni fani ya wasomi tofauti na kazi zao, lakini Daktari kamili lazima ajue haya...

Daktari - anafundishwa kufanya upasuaji, yaani Surgery operation, japo hatakiwi kufanya zile ambazo ziko zaidi ya viwango vya kitaaluma kama kupandikiza viungo...unless amesomea kuwa Specialize Surgeon..

Daktari - Anasomea utaalamu wa kuyafuatilia magonjwa na jinsi yanavyoongeza au kupungua(Monitoring)

Na hii list ya majukumu ya Daktari ni ndogo sana niliyoleta hapa, ningejaza kama siredi mbili au tatu .....

CO - Alikuwa kilaza fulanI wa Biology, Physics, Maths na Chemistry kwa O level na Advance..
CO - Miaka 3 ya masomo tu anataka kunichunguza Cancer...huu ni ulozi...
CO - Ni upuuzi mtupu, sieendelei na huyu imetosha hapa...
Ndo tupo huku vijiin kaka, ukisikia shangaz yako ulimuacha kijijin ameenda hospital ana ametibiwa na amepata unafuu sisi wapuuzi ndo tumemtibu braza. Tunaongoza Zahanat zote Tanzania, na ndo Health Facility nying zaid Tanzania na inahudumi Watanzania weng zaid, na unaposikia hali ya afya ya Watanzania inaimarika sisi tunahusika mkuu.

Sisi ndo Wahasibu huki,.Wafamasia, makatibu n.k. Mungu yupo nasi.
 
Nilijua ni wa AAA kumbe kilaza unatafuta shortcut…
Nitakuja kufungua kampuni ya ambulance nikuajiri kamaCO…..ndio itakufaa lakini sijui hata sijui kama utapasi

View attachment 2245745
naona umeshaanza bangi,maana sentensi uloiandka inaonesha ni bangi tupu,Sasa kuna kampuni ya ambulance wap,acha bangi mzeeunakoelekea tunakukosa kabisa

Sent from my CPH2179 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom