Kuna serial killer[s]?

Mbona mnazunguka mbuyu????? mbona kuna tetesi mitaani kuwa kuwa kuna ''Makondoo' yameasi ndo yanayofanya hii kitu??
Mbona mnazunguka mbuyu????? mbona kuna tetesi mitaani kuwa kuwa kuna ''Makondoo' yameasi ndo yanayofanya hii kitu??
hizi ID zilizotengenezwa zamani lakini posts zake hazizidi elfu 3 huwa ninakuwa makini nazo!!

Sababu ya kuasi ni nini!? Nimesoma habari yote kwenye gazeti la mwananchi iliyobeba uzito wa juu.
 
Acha kumwaga vitu bro.......
 
Hawa siyo serial killers wanachagua na serial killers hawachagui.

Hawa kero zao ziko kwenye vipeperushi serial killers hawafanyi hivyo
 

You're more than right! We could well be dealing with a mad, pot smoking, vigilante/s believing he/they is/are BATMAN/BATMEN against the league of shadows, which to him/them happens to be the government!
 
Hawa siyo serial killers wanachagua na serial killers hawachagui.

Hawa kero zao ziko kwenye vipeperushi serial killers hawafanyi hivyo

..wako wa aina nyingi.

..wako serial killers wanaochagua victims wao.

..tafuta habari za serial killer anaitwa " b.t.k" ( bind torture kill).

..muuaji " b.t.k" alikuwa mzee wa kanisa, mtumishi wa halmashauri ya jiji moja marekani, na baba wa familia. Lakini pembeni alikuwa muuaji.

.."b.t.k" kichaa chake kilimcharuka akawa anaua watu kwa kipindi fulani. Baadaye akaacha kuua na kupelekea polisi kuamini kwamba huenda amefariki.

..baada ya miaka kadhaa kupita "b.t.k" akaibuka tena na kuanza kutoa vitisho kuwa ataua tena.


..Polisi wakaanza msako tena. Bahati nzuri mtoto wa "b.t.k" aliwahi kupimwa(sikumbuki kwa sababu gani) DNA. Hiyo ilipelekea polisi ku match DNA walizokuwa nazo na DNA(from the crime scene)
ya "b.t.k" na matokeo yake muuaji huyo akakamatwa.

Cc@Nyani Ngabu
 

 
Me nadhani kuliko kutumia nguvu ili kuelewa tukio la hao mabwana, ingetumika akili ya kiuchunguzi taratibu mpaka ibainike, unless serikali iwe inajua wats goin on. lakini pia matukio haya sio ya kuyafanyia mzaha mwisho wa siku linaweza likaibuka jambo zito likatikisa amani ya nchi.
 
Wanaweza kuwa mass murders pia ..maana nia zao/yao ni kuuwa zaidi ya mmoja na sehemu hio hio.
Cha muhuimu ni polisi kudumisha uhusiano wa karibu na mzuri na wanainchi wa sehemu hio... sio kuwa maadui
 
hizi ID zilizotengenezwa zamani lakini posts zake hazizidi elfu 3 huwa ninakuwa makini nazo!!

Sababu ya kuasi ni nini!? Nimesoma habari yote kwenye gazeti la mwananchi iliyobeba uzito wa juu.
Maslahi mkuu,wanayajua haya ndo maana hawataki kuyajadili bungeni.By the way sisi hayatuhusu yanawahusu askari na wana Kijani wao
 
Serial killer ni nini, mtoa mada unafikiri kila mtu ni jambazi kama wewe!? Kwamba tutakuwa tunajua aina za mauaji!!!? Fafanua
 
Nyani Ngabu, swala la chuki za kidini, ni kitu ambacho katika nchi yetu hakijachukua ama kufikia hatua ya waumini kutoaana ROHO..

Naweza kuamini mauaji haya yanayo endelea, pengine katika jeshi la Polisi ndani yao wapo wanaoelewa chanzo chake.

Sina hakika kama mauaji haya yanawalenga askari/raia, wenye muelekeo fulani wa KIIMANI.

Kwa nini mauaji kwa asilimia kubwa yawalenge viongozi wa chama, na askari wetu kutoka jeshi la usalama wa raia na sasa hawa wa barabarani...!!?

Ni jukumu la POLISI wakishirikiana pamoja na RAIA wema kukomesha mauaji haya pia kueleza ama kutoa majibu, nini sababu na lengo la mauaji haya...
 
Intelejensia ya hali ya juu inahitajika kutumika hapo,wauaji wanaonekana wana uzoefu sana inawezekana ni wanajeshi/askari waliofukuzwa au kuacha kazi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…