Kuna serial killer[s]?

Kuna serial killer[s]?

Naona kama mauaji yao mengi yanakuwa yapo 'subtle' kidogo...polisi 8,trafiki, wenyekiti vijiiji, viongozi wa ccm, hawa ni magaidi, wanalengo la ku achieve political aim fulani

Hmm...haya..labda...
 
Wewe Nyani huna unachoelewa zaidi ya kumpigia zumari mfalme. Hakuna kitu kama udini Tanzania ila kuna chama moja chakavu kinachoeneza chuki na uadui kati ya watanzania!
Wewe ndiyo hujui kuna udini huko muda utaeleza na wewe nadhani mhusika unataka hilo jambo uligeuze hizo kung fu za miskitini zilikuwa za nini. Acha ujinga mnaua kuna dini inayoruhusu kuua. Hakuna siasa hapo ZNZ mliua kwa jina la siasa auae kwa upanga hufa kwa upanga.
 
Wewe ndiyo hujui kuna udini huko muda utaeleza na wewe nadhani mhusika unataka hilo jambo uligeuze hizo kung fu za miskitini zilikuwa za nini. Acha ujinga mnaua kuna dini inayoruhusu kuua. Hakuna siasa hapo ZNZ mliua kwa jina la siasa auae kwa upanga hufa kwa upanga.
Acha kusikikliza propaganda za ccm eti kungfu misikitini...shame on you! I'm a Christian but I know better than huo ukichaa wa maccm wa kungfu misikitini!
 
Body camera's zinaweza kusaidia kama hao jamaa wauaji hawana mafunzo yoyote ya ki-ulinzi. Kinachosumbua watu ni ujuzi wa hao watu, wanaua then wanaziharibu ili kusiwe na picha. Na wangekuwa ni raia kwa kawaida kwa mkwara waliopigwa wangekuwa wameshaogopa.

Hapa kuna tatizo tayari, maana amri jeshi mkuu anasema wapeleekeeni salaam, nao wanajibu hizo salaam kwa kuua askari wake. hii sasa ni vita.

Kwa elimu yangu ndogo ya Jeshi kama askari wa akiba ( x- JKT Makutupora); Nafikiri ni muda muafaka sasa kulibadili hilo eneo na kuwa eneo la operation ya kijeshi kwa muda. Ni operation ya kijeshi ndiyo inaweza kusaidia kuwatokomeza hawa jamaa kwa haraka.

Kwa mfano hako ka eneo ka wilaya ya Rufiki kanahitaji askari 2000 tu ambao wako trained ki-komandoo ambao kila askari ku-cover eneo la mraba la heka 5 kwa mfano.

Komandoo ama askari wa mwituni anashushwa kwa helkopta, na anaweza kuishi kule msituni kwa siku zaidi ya 10 bila usaidizi wowote ule.

Askari huyu anabeba:
1. Kibuyu cha Maji
2. Biskuti na Mikate.
3.Bunduki za kisasa
4. Camera's
5. Kisu
6. Vyombo vyake vya mawasiliano bila kusahau GPS ili kujua mahali alipo.

Tunawahitaji hawa jamaa wakamalize hiyo kazi - just 10 days operation inatosha kabisa.

Angalizo:

Isitangazwe siku ya kuanza operations ama kusitisha; maana hawa jamaa ni waviziaji - wanaua then wanakimbia nduki kujificha. sasa huko wanakokimbilia kila eneo la mraba la heka tano yupo askari - usiku na mchana = hawawezi kukimbilia kokote kule, ni kuwakamata kama chickens.


1280px-thumbnail.jpg
 
Pattern si ndo hiyo ya askari....au?

Kati ya askari waliokwishauliwa na raia wa kawaida, ipi ni idadi kubwa?
Hata kama inaonekana askari ndio victims zaidi lakini bado hakuna pattern inayounganisha askari wanaokumbwa na mauaji yenyewe!! Askari is just a set lakini ukiwa na pattern utatengeneza subset or even subsets!

Kwa mfano, unaweza kukuta ni kweli wanaouawa ni askari lakini ukifanya triangulation unakuta karibu wote wamewahi kufanyia kazi, mathalani Arusha!

Tayari hapo umeshapata pattern inayokutengenezea subset... kwamba, not just cops bali askari walio Arusha au waliopata kufanyia kazi Arusha!

Hapo utaangalia ni matukio gani yenye sura ya kuweza kulipiza kisasi ambayo yamepata kutokea Arusha! Utayachuja kisha utakuja kuhusisha na Pwani... kwamba, victims wa hayo matukio origin yao ni ipi hasa ili tujaribu ku-connect dots kwamba huenda mauaji/matukio yalifanywa na polisi dhidi ya XYZ ambao asili yao ni Pwani na kwahiyo ama ndugu zao or anything like that wanachofanya ni kulipiza kisasi!!!

... au kama ni issue za dini; matukio gani polisi wa Arusha waliyafanya ambayo yaliwalenga watu wa dini fulani. Unaweza kumpata labda D... n.k!!!

Kinyume chake, ninachokiona Pwani ni just killings na victims ni askari polisi na viongozi wa serikali za mitaa!!!

Anyway, si mimi wala wewe tunaofahamu undani wa hao wanaouawa... labda polisi wenyewe wameshaanza ku-connect hizo dots ninazosema!!!
 
kazi ya polisi kwa hapa Tanzania inaonekana ni nafuu ya maisha ya ajira tu sio kama kazi ya kitaalamu. leo vijitoto toto vinajipaka poda poda kivulana ndo kipolisi kweli ? lazima tujizatiti tuweke mikakati si kwa sababu ya hili tu bali kwa mambo yote yanayohusu ulinzi na usalama wa nchi.

Duuh!!

Kuna sehemu kuna bint ni askari wa usalama barabarani anavaa kisketi kifupi akikaa kwenye mawe/magogo wakiwa kazini kisketi kinapanda juu mapajaa yanabaki nje huku usoni amejimwagia wanja.

Unabaki unajiuliza huyu kweli alipita CCP kule uwanja wa damu kweli?
 
..hata mimi hii dhana kuwa ni serial killer niliifikiria.

..lakini serial killer mara nyingi hua anaua mtu mmoja mmoja.

..Pia Sina kumbukumbu ya serial killer kuua/kushambulia kundi la watu (askari 8..).

..sababu hizo zimenifanya niamini kwamba siyo serial killer bali ni kikundi cha watu.

NB.

..hakuna namna moja ya kumkamata serial killer.

..mara nyingi serial killer hukamatwa kutokana na uzembe wake mwenyewe.

..kutokana na kufanya mauaji mengi kwa mafanikio serial killer anaweza kuishiwa ujanja/maarifa au akawa too bold/careless na hivyo kuishia kudakwa.
 
Haya mauaji yanayoendelea huko Pwani yamenifanya nifikirie huenda kuna serial killer huko.

Kwa kumbukumbu zangu sijawahi kusikia Tanzania tukiwa na tatizo la watu wa hivyo lakini hiyo haimaanishi hawawezi kuwepo.

Pamoja na uwezekano wa matukio hayo kuwa ni ya kighaidi [unaosukumwa na dini], ingekuwa vyema kwa vyombo vyetu vya usalama kuangalia uwezekano wa uwepo wa serial killer pia.

Halafu, nadhani ni muda muafaka sasa kwa askari wetu wa polisi na wale wa usalama barabarani kuanza kuvaa body cameras.

Uvaaji wa hizi camera utasaidia mengi sana ikiwemo kuondoa utata wa unyanyasaji wa polisi.

Kwa sasa sidhani hata magari ya polisi yako mounted na cameras.....

06212017_bodycam2_062832-780x532.jpg
Ushauri wa maana sana huu
 
Duuh!!

Kuna sehemu kuna bint ni askari wa usalama barabarani anavaa kisketi kifupi akikaa kwenye mawe/magogo wakiwa kazini kisketi kinapanda juu mapajaa yanabaki nje huku usoni amejimwagia wanja.

Unabaki unajiuliza huyu kweli alipita CCP kule uwanja wa damu kweli?

Ulitaka awe vipi?
 
Duuh!!

Kuna sehemu kuna bint ni askari wa usalama barabarani anavaa kisketi kifupi akikaa kwenye mawe/magogo wakiwa kazini kisketi kinapanda juu mapajaa yanabaki nje huku usoni amejimwagia wanja.

Unabaki unajiuliza huyu kweli alipita CCP kule uwanja wa damu kweli?
CCP hakuna uwanja wa damu bhana kozi yenyewe miezi 9 uwanja wa damu utatoka wapi hapo??
 
Back
Top Bottom