Kuna sababu zipi za msingi zilizofanya Serikali yetu iipe uzito mkubwa sana kesi iliyofunguliwa na Tundu Lissu dhidi ya Spika Ndugai?

Hivi Mkuu kipendaroho, inakuwaje serikali hii inakiuka kanuni ya msingi kabisa ya binadamu, inayosema YOU CAN NOT BE CONDEMNED UNHEARD??

Ninachojua ni kuwa kwenye sheria ya kazi, ni takwa la kisheria kwa mwajiri kuitisha kikao cha Disciplinary Hearing kwa ajili ya kumpa nafasi, mfanyakazi anayetuhumiwa, ili ajitetee........

Hivi ina maana Spika Ndugai haijui kanuni hiyo??
Ndio maana akina mashamba wanataka kumtoa Ndugai kwenye case eti yeye hakumfuta ubunge o Lissu
 
Pamoja na kuwa ni Banana Republic tangu uhuru, siku za karibuni tumekuwa nchi ya kishamba sana. Tumekuwa na priorities za kipuuzi sana, uonevu uonevu hivi, ukandamizaji, dhuluma, ubabe wa kitoto, yaani ujinga ujinga tu.
tumewakabidhi walimbukeni na washamba madaraka-zitto voice!
 
Wewe unasema muda wake uishe ili aondoke??

Kwani wewe hukumsikia jinsi alivyosema kuwa "haoni" mtu atakayeendeleza kasi yake.......

Hiyo ni "indicator" kuwa anataka kujiongezea muda wa kutawala
 
Shauri hili limeweka historia ya pekee.
Hiyo ni kweli kabisa

Na hasa utamu utakuja pale mahakama itakapoanza kuisikiliza kesi yenyewe, ambapo Tundu Lissu anamtaka Spika Ndugai aje atoe ushahidi mahakamani, kuwa yeye Spika hajui alipo Tundu Lissu
 
Habari iliyostua sana katika kesi iliyofunguliwa na Tundu Lissu siku chache zilizopita, dhidi ya Spika Ndugai, ni kusikia kuwa walikuwepo mawakiki 15, kutoka ofisi ya mwanasheria mkuu, akiwemo Mwanasheria Mkuu mwenyewe, wakimtetea Spika Ndugai,dhidi ya mawakili 4 tu wanaomtetea Tundu Lissu, katika kesi iliyofunguliwa ya kupinga kuvuliwa ubunge wake

Kwa mujibu wa duru za kimahakama ni kuwa idadi hiyo ya mawakili, imevunja rekodi, kwa kuwa haijawahi shuhudiwa, katika mahakama hiyo, kwa mawakili wengi kiasi hicho kusimamia kesi.moja.

Sisi wananchi tungeiomba serikali yetu itujibie maswali yafuatayo:-

1. Ni kwanini serikali ndiyo iweke mawakili, tena wengi kiasi hicho katika kesi ambayo "haiwahusu" kwa kuwa anayeshitakiwa ni Spika wa Bunge, ambapo Bunge hilo ni mhimili mwingine na Bunge hilo lina mawakili wake, ambao wangweza kumsimamia kikamilifu Spika Ndugai??

2. Iweje serikali iweke mawakili wengi kiasi hicho, kwa ajili tu ya kuweka mapingamizi ili kesi hiyo isisikilizwe. Je serikali wanaogopa nini, ikiwa kesi hiyo itasikilizwa??

3. Kama mawakili hao wa serikali wanajiamini kuwa wako makini kisheria, si wasubiri kesi ya msingi ianze, ndiyo waonyeshe umahiri wao na kuwashinda mawakili wanne pekee wa Tundu Lissu??

4. Hivi kuna mantiki gani kwa serikali hii kuweka nguvu zote hizo kwa kesi inayohusu Mbunge mmoja tu kulalamikia kuvuliwa ubunge wake wakati huu ambapo tumesikia kuwa lipo jambo "very serious" la ndege yetu, ambayo imenunuliwa kwa kodi zetu, imekamatwa huko Afrika Kusini, kwa ajili ya madeni tunayodaiwa??

5. Hivi si ingekuwa busara zaidi kwa serikali yetu kutoa uzito mkubwa, katika suala hilo la ndege, ambalo ninaamini ndilo lenye maslahi mapana zaidi kwa Taifa letu, kwa vile limetuweka katika sura mbaya sana kimataifa, kwa vile Taifa letu haliaminiki tena, kwa kuwa dunia nzima imeshafahamu kuwa nchi yetu hivi sasa ni "wakachaji" wa kulipa madeni tunayodaiwa??
Mtu mpumbavu au mwendawazimu aghalabu anaweza kuacha fedha barabarani lakini akatumia jitihada kubwa kulinda gazeti.
 
Back
Top Bottom