Kuna raha au amani ya roho kupita kwenye daraja la juu ya bahari huku ukiwa katika msongo huu wa mawazo?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,014
144,371
1. Una miaka mitano mshahara wako serikalini ni ule ule aliouacha JK

2. Una madai yako serikali na huu ukiwa ni mwaka wa tano hujalipwa na wala juju utalipwa lini

5. Kila mwisho wa mwezi unakatwa asilimia 15 ya mishahara wako kulipa mkopo wa Bodi ya Mikopo

6. Una mzee wako kastaafu huku hajui ni lini atalipwa mafao take.

7. Una mazao yako huko kijijini hayana soko

8. Una watoto au wajukuu kadhaa nyumbani Kwako wamehitimu vyuo na hawana ajira na pa kuwapeleka hunan

9. Una gari lako la mkopo lakini unalazimika kuliacha nyumbani kisa mifukoni kumechacha

10. Unakatiza kwenye daraja la juu huku nawazo kulipa kodi ya nyumba inayoongezeka wakati mishahara wako umegota kwa miaka mitano sasa

11. Au unapita kwenye daraja la juu pale Ubungo huku mikopo ya kibiashara uliokopo hailipki

12. Au unakatiza pale Ubungo interchange ili uende kuhudhuria mkutano wa kisiasa wa chama upinzani huku una hofu ya kukamatwa

13. Au unaona SGR inajengwa wakati huo bei ya mfuko wa saruji haishikiki

14. Au unaona Bwawa la Umeme linajengwa wakati uwezo wako wa ku-invest unashuka au unalazimika kufunga biashara zako kutokana kushindwa kulipa kodi

15. Unapita pale kwenye Ubungo interchange huku unajiuliza nikiacha hii kazi mafao ya kujitoa ni mpaka nifikishe miaka 55 huku ukiwa na miaka 40 au 35 leo hii

Hakika yataka moyo na zaidi kujitoa akili kuridhika na hali hii.
 
Usipite huko na hali hiyo,ilinitokea napita darajani na chini kuna bahari ya kina kirefu. Yaani shetani akawa anasema hapa hapa aisee mpk nayumba yaani km vile nasukumwa na daraja ni refu liko juu sana alafu kingo zake fupii yaani mpaka nalimaliza🙏.
 
Rubbish ,wapiga kura wengi hawana smartphone na wapo buza,hapa unafurahisha kijiwe cha kahawa na hakiwezi pindua matokeo ya ushindi wa Magufuli
 
Salary Slip,
Unawaza kuwa kuna maeneo Watanzania wananunua ndoo ya maji Mia tano.
Wengine wanakunywa maji kwa kushirikiana na punda,wakienda kuchota maji wanaoga huko huko!
Wengine wanatembea Kilomita 10 kwenda kupima malaria
Vituo vya kutolewa huduama za afya zimegeuka mkazi ya pop
 
Twende na TL atatufikisha tunapopata. Tumechoshwa na ubabe uliopo, Mungu mkubwa siku hazigandi Mbabe amebakiza miezi mitatu kuwa katika ofisi ya umma.
 
MaCCM mada Kama hizi hua either yatukane!, au yatoke nje ya mada!, Au vyote viwili...the tallest ameanza hapo juu. Ukweli unasumbuaga sana nafsi 😂😂😂😂😂😂
 
Back
Top Bottom