Kuna rafiki yetu mmoja mke wake kajinyonga

Kuna rafiki yetu mmoja mke wake kajinyonga

Sungusunguu

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2018
Posts
1,280
Reaction score
998
Habarini!

Kuna rafiki yetu mmoja mke wake kajinyonga wakiwa pamoja ndani na mpaka sasa mwanaume kakamatwa na yuko polisi.

Je, ni sahihi kijana huyo kushikiliwa na je sheria inasemaje mtu akifa ndani ya nyumba na mkiwa pamoja kwani kwa maelezo ya uyo jamaa anadai yeye aliwahi kulala na mwanamke alibaki sebuleni ambako akakuta kajinyonga na anadai aliwahi kumtoa kamba shingoni na kumfungua kisha baadae ndo akaanza kutoa taarifa kwa majirani.
 
Habarini!
Kuna rafiki yetu mmoja mke wake kajinyonga wakiwa pamoja ndani na mpaka sasa mwanaume kakamatwa na yuko polisi
Je ni sahihi kijana huyo kushikiliwa na je sheria inasemaje mtu akifa ndani ya nyumba na mkiwa pamoja kwani kwa maelezo ya uyo jamaa anadai yeye aliwahi kulala na mwanamke alibaki sebuleni ambako akakuta kajinyonga na anadai aliwahi kumtoa kamba shingoni nakumfungua kisha baadae ndo akaanza kutoa taarifa kwa majirani
Suspect wa kwanza akifa mwenza ni mwenzake. Unless labda haukuwepo na una ushahidi wa hilo. Ukitazama Crime and investigation utagundua upelelezi uwa unaanzia ndani kwenda nje. Yani suspect uwa wanaanza kwua watu wa karibu, mfano anaoishi nao mtu labda mume, au mke, ndugu, kama ana watoto wazima, then ndiyo wanaenda nje iwe amejinyonga au kauawa.
 
Ikiwa aliyejinyonga katokea kule kwa shujaa Mkavi Nyika, jua kwamba kaongezea idadi ya mashujaa mbinguni. Hata hivyo, duniani pagumu sana, ukiona mtu kajiua/kauwawa, basi tuhuzunike kidogo tu, na kazi iendelee. Maana tuliobaki, hatujui tutakufaje!
 
Kuna masuala mengi ya kujibu
1 Alikuwa wapi mpaka mwenziwe ajinyonge?
2 Hakusikia kishindo chochote?
3 Kwanini amfunguwe kamba badala ya kuita polisi nao ndio wakafungua kamba?
4 Mwilini mwake ana mikwaruzo yoyote ile?
5 Kuna ujumbe wowote wa marehemu wa kujinyonga.

Simu ya marehemu inahitajika kuangaliwa kwa umakini kama kuna ujumbe wa usaliti kwa mwenza wake mpaka kupelekea mauti kumfika.
Jeshi la polisi lifanye kazi yake kwa haki pande zote isitumuke hisia bali ushahidi kamili wa kujiridhisha.

Lunatic
 
Kujiua kama ilivyo kosa kisheria pia kwa Mungu ni dhambi. Hivyo ni wazi kwa upande wa kiroho huwezi kumwita shujaa mtu aliyejiua bila kutilia maanani sababu iliyomfanya ajitoe uhai; na wala huwezi kusema yupo mbinguni labda kama alijirudi na kutubia dhambi ya kujiua kabla hajakata roho.
 
Alipaswa amuache hapohapo ananing'inia hadi polisi waje wamtoe
Unajua kiwewe cha kumkuta mwezi wako amejinyonga wewe? Fikiria unaingia chumbani unarudi unamkuta ananging'inia! Yaani usiache kujaribu kumuokoa useme unasubiri polisi? Kwanza nikuambie: kitendo cha kumuacha eti unasubiri polisi wakati muda mfupi mlikuwa wote kitaleta mashaka zaidi kuwa wewe ndiye uliyemuua.
 
Kuna masuala mengi ya kujibu
1 Alikuwa wapi mpaka mwenziwe ajinyonge?
2 Hakusikia kishindo chochote?
3 Kwanini amfunguwe kamba badala ya kuita polisi nao ndio wakafungua kamba?
4 Mwilini mwake ana mikwaruzo yoyote ile?
5 Kuna ujumbe wowote wa marehemu wa kujinyonga.

Simu ya marehemu inahitajika kuangaliwa kwa umakini kama kuna ujumbe wa usaliti kwa mwenza wake mpaka kupelekea mauti kumfika.
Jeshi la polisi lifanye kazi yake kwa haki pande zote isitumuke hisia bali ushahidi kamili wa kujiridhisha.

Lunatic
Hili la kusema asingejaribu kumtoa kwenye kitanzi nakataa. Yaani uko na mke wako sebuleni, na ni mzima, ukaingia chumbani, haijalishi umekaa muda gani, kurudi ukakuta ananing'inia kwenye kitanzi uache kujaribu kumuukoa eti unasubiri polisi? Haki ya nani itakuchukuwa muda sana ku-convince polisi kuwa siyo wewe umemuua. Kawaida kwenye mazingira kama hayo jambo la kwanza hutaamini kama ameshakwisha kufa na utakimbilia kumtoa.
 
Alimtoa kamba kwa kumfungua au kuikata? Kama aliifungua hapo uchunguzi utakua mrefu sana maana mtu aliejinyonga ni ngumu sana kumfungua kamba ukiwa peke yako labda uikate

Lakin pia Kuna matukio mengi ya watu kuuwawa alaf wananing'inizwa kama wamejinyonga lazma ichunguzwe, isije ikawa alitaka kutumia mbinu hiyo ila akashindwa kumnyanyua na kumning'iniza baada ya kumnyonga mwenyewe akaamua kusema alimtoa kamba

Kwahiyo uchunguz lazma ufanyike kutokana na mazingira yaliyokutwa hapo Kama hajatenda ataachiwa tu endelea kumuombea jamaa na kumfariji katka kipindi hik kigumu hiyo ndo mitihan ya maisha
 
Je, ni sahihi kijana huyo kushikiliwa na je sheria inasemaje mtu akifa ndani ya nyumba na mkiwa pamoja kwani kwa maelezo ya uyo jamaa anadai yeye aliwahi kulala na mwanamke alibaki sebuleni ambako akakuta kajinyonga na anadai aliwahi kumtoa kamba shingoni na kumfungua kisha baadae ndo akaanza kutoa taarifa kwa majirani.
Je alikutwa ana majonzi au analia kwa hisia kali!!? Kama alikutwa mkavu atasumbuka sana
 
Kama si yeye kasababisha kifo chake wala hapo polisi hakuna shida ukilinganisha na machungu anayopitia.
 
Back
Top Bottom