Kuna ombwe kubwa la uongozi nchini

Kuna ombwe kubwa la uongozi nchini

Hakuna ombwe la Uongozi nchini kaka bali watanzania walio wengi hawakubaliana na misimamo na maamuzi wa Rais Magufuli ktk kuendesha Serikali kwasababu tulizoea kutofuata Sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa Kikatiba.

Kwani yeye anafuata katiba, sheria na kanuni?
 
Mtu wa kwanza kusema kwamba kuna Ombwe la uongozi nchini mwetu ni Mwalimu kwenye kitabu chake cha "Uongozi wetu na Hatima ya Tanzania. Wakati huo Rais alikuwepo na uongozi kama uliopo sasa ulikuwepo pia. Ombwe la Uongozi si kutokuwepo watu kwenye nafasi bali kuwa na watu wasioenea kwenye nafasi walizopo.

Halafu ujinga wa kudhani eti ukiandamana utakiona cha mtema kuni kama ndiyo ishara ya kuwepo kwa uongozi hauna maana. Leo hii Somalia kuna Ombwe la Uongozi lakini si kwamba ukiandamana dhidi ya waliopo madarakani hautushughulikiwa.

Kusema hakuna Ombwe la Uongozi kwa kuwa Reli inajengwa, Fly Overs zinajengwa, huo tena ni ujuha. Hata kwenye zile nchi zinazotawaliwa kwa mkono wa chuma kama Korea ya Kaskazini hayo pia hufanyika. Jee hizo reli zinajengwa kwa kuwa hakuna Ombwe la uongozi ama zinajengwa kwa kuwa wajengaji na wao wanatafuta mlo wao na wameuona nchi mwetu?
Napendekeza ilo ombwe lizibwe na lowasa na sumai. Manake mbowe nae yupo kwenye uongozi. Au toa alternative basi na sio kulalama tu, unakua hueleweki.
 
Hakuna ombwe la Uongozi nchini kaka bali watanzania walio wengi hawakubaliana na misimamo na maamuzi wa Rais Magufuli ktk kuendesha Serikali kwasababu tulizoea kutofuata Sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa Kikatiba.
Ili aaminiwe lazima awe mfano katika kuheshimu katiba na sheria za nchi,pakiwa na watu walio juu ya sheria na katiba uhalari wa kuaminiwa unatoweka bila notisi.
 
Hata kama ilikuwepo kwa miaka yote hiyo tuliishi kwa mazoea tu ya kijamaa ambayo ni tofauti sana na ukomunisti.
...Kipindi cha Mkapa na KJ tuliishi kijamaa siyo? Viongozi wa serikali hii walikuwa pia awamu ya nne, hawakuyaona haya?
 
Hiyo santuri ya ombwe tumeanza kuisikia tokea zama za mkapa,ikapata nguvu zama za Kikwete,ya kuwa anasafiri sana,hajali,vasco da Gama.
Sasa hili ombwe la Magufuli naona ni la wapinzani kukosa hoja mbadala tu.Nchi inakwenda mambo yanaenda ombwe hilo labda lipo chadema katibu anapwaya
Hapana usiwasingizie wapinzani kwani tunaona huyu kiongozi anavyoongoza vibaya ndani ya ccm hakubaliki na viongozi wa ccm na pia kwa wananchi waake kajitengenezea mamlaka yake pekeyake isiyokuwa na tija kwa wananchi
 
Acha kuonyesha ujuha wako hadharani na kuidumaza akili yako. Mwinyi ambaye aliwahi kuwa Rais na Mwenyekiti wa CCM alisema nchi inaendeshwa kama gari bovu halina sukani. Aliyewahi kuwa Jaji Mkuu na Waziri Mkuu wa Tanzania pia alitamka kwamba nchi imepoteza mwelekeo. Kinana pia juzi juzi katamka haya. Hebu acha kujitoa ufahamu na kujifanya hamnazo ili uendelee kutetea uozo wenye madhara makubwa kwa Tanzania na Watanzania.

Wasichofahamu,wala kukizingatia ni teknolojia ya sasa kila wanachokitenda na kukinena kinahifadhiwa hawa viongozi wetu wa leo IPO SiKu watayakana Maneno yao na matendo yao na hapo historia itawashukia kama mwewe na hapo ndipo msiba wa koo zao utaanzia
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Ni shida sana kuongoza kwa style hii kila anafanye lake kujiokoa na balaa
 
Kumsikiliza Msigwa wakati nae ana ombwe la uongozi,kwani anadhani tumeshau alivyobebwa na mwenyekiti wake dhidi ya Ole Sosopi,ukiwa mchafu usiwanyoshee vidole wenzako kuwa wachafu wakati mwenyewe unanuka
 
Acha kuonyesha ujuha wako hadharani na kuidumaza akili yako. Mwinyi ambaye aliwahi kuwa Rais na Mwenyekiti wa CCM alisema nchi inaendeshwa kama gari bovu halina sukani. Aliyewahi kuwa Jaji Mkuu na Waziri Mkuu wa Tanzania pia alitamka kwamba nchi imepoteza mwelekeo. Kinana pia juzi juzi katamka haya. Hebu acha kujitoa ufahamu na kujifanya hamnazo ili uendelee kutetea uozo wenye madhara makubwa kwa Tanzania na Watanzania.

Kaka yangu BAK hawa uliowataja wana credibility gani mpaka wawe reference katika huu mjadala? What have they done to merit this reference? au simply because wamewahi kukalia hizo nafasi ulizozitaja? Maana Mwinyi (well mzee tumuache apumzike tusianze kufukua makaburi), Kinana sidhani kama ana hata moral authority ya kusimama na kukemea lolote katika nchi hii (tupo hapa tulipo kwa sababu ya watu kama yeye). Mzee wangu Warioba....he may be credible but kwa lipi? One might say Katiba...iko wapi? Whatever we do..hawa wazee ndo wamechangia kutufikisha hapa tulipo.

I agree uongozi wetu leave a lot to be desired. We could certainly do better. and we should!

Wengine tumechoka kuona wale wale waliokuwa kwenye hizo nafasi..leo kwa sababu wamewekwa pembeni..ndo wanapata courage ya kuongea! na kuanza kutuhubiria huu ujinga... Wengine tunakwenda na Pombe si kwamba tunamkubali lakini kwa sababu tunaona kila mwanasiasa anatuchezea akili. Wakiwa peponi..hawana habari. wakitoswa..ndo unafiki unaanza wa kutuletea ukombozi.

Wengi ni matapeli wa siasa hawana lolote.
 
Ili aaminiwe lazima awe mfano katika kuheshimu katiba na sheria za nchi,pakiwa na watu walio juu ya sheria na katiba uhalari wa kuaminiwa unatoweka bila notisi.
Tatizo letu tunalazimisha kuaminisha wanainchi kuwa Rais ktk hafuati Katiba.

Ukiuliza ni nini anachofanya nje ya Katiba hata hatuelezi chochote zaidi ya kuanza kutoa tu hisia zetu.

Rais Magufuli anafuata sheria kama alivyoapa na Katiba kwa kuitii na kufuata.
 
Hakuna ombwe la Uongozi nchini kaka bali watanzania walio wengi hawakubaliana na misimamo na maamuzi wa Rais Magufuli ktk kuendesha Serikali kwasababu tulizoea kutofuata Sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa Kikatiba.
Nani hafuati sheria na Katiba kati ya raia n.a. Rais?
 
Nani hafuati sheria na Katiba kati ya raia n.a. Rais?
Chagua mwenyewe jibu la awali lako nachojua Mimi ni kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anafuata sheria kama zilivyoanishwa kupitia ktk Ibara mbalimbali za Katiba ya mwaka 1977 na marekebisho yake.
 
Hapana usiwasingizie wapinzani kwani tunaona huyu kiongozi anavyoongoza vibaya ndani ya ccm hakubaliki na viongozi wa ccm na pia kwa wananchi waake kajitengenezea mamlaka yake pekeyake isiyokuwa na tija kwa wananchi
wewe umejuaje hakubaliki wakati ni mpinzani na hutaki wapinzani waingizwe.
Mtu aliechaguliwa kwa 100%,vikao halali vinafanyika kwa mujibu wa katiba,hakuna hata upande ulioasi,chama kimetulia
Enzi za mkapa walikuwepo watu akina sabi munasa,enzi ya JK walikuwepo akina lowassa na mansour himidi
Kwa Magufuli bado anapeta tu
 
Mwehu utaanza kuwa wewe punguani. Hakuna chochote nilichoandika ambacho ni cha uongo. Huwa sikurupuki humu kama wewe mchumia tumbo usiyejitambua uliyekubali kujazwa ujinga na kutetea uozo mkubwa nchini.
Nakushauri tu fanya kazi kwa kutumia akili na maarifa usikae kusubiri kupewa mgao wa ruzuku ya chama umri unaenda, utabaki kulaumu kila mtu mwisho utaanza kujilaumu mwenyewe
 
Nchi ipo kwenye mstari kuliko wakati wowote ule tangia uhuru. Kama unafikiri nchi ina ombwe la uongozi ingia mtaani uandamane kisha utakuja rejesha majibu kama nchi ina uongozi ama vipi. Mtaleta heshma tu ata kama haupendi na maendeleo ni kila kona mpaka treni za umeme na fly over. Mafisadi wa Chadema Wamepoteana wamebanwa kila kona.
Unaongelea maendeleo ukiwa mjini Tanzania sio ubungo kaka kuna namtumbo, kuna katesh kuna bariadi ...... Usiongelee masuala yenye faida tu katika uchumi mkubwa ongelea na uchumi mdogo, kwa nn unga ipande kilo,mchele pia Umeme maji mahosipitali shule bure lakini bado watu wanashindwa kuwapeleka watoto(kuna wenzako hata kumnunulia viatu vya plastic mwanae n tabu) acha ushabiki Wa flyover wakati bibi ako anakunya vichakani
 
Tatizo lako unapenda sana kujibaraguza ili kuonyesha unanifahamu. Kwa taarifa yako sitegemei ruzuku ya yoyote yule ninachoandika humu ni kwa mapenzi ya nchi yangu tu ambayo inaangamizwa na wahuni pamoja na utajiri mkubwa uliokuwepo nchini.

Nakushauri tu fanya kazi kwa kutumia akili na maarifa usikae kusubiri kupewa mgao wa ruzuku ya chama umri unaenda, utabaki kulaumu kila mtu mwisho utaanza kujilaumu mwenyewe
 
Tatizo lako unapenda sana kujibaraguza ili kuonyesha unanifahamu. Kwa taarifa yako sitegemei ruzuku ya yoyote yule ninachoandika humu ni kwa mapenzi ya nchi yangu tu ambayo inaangamizwa na wahuni pamoja na utajiri mkubwa uliokuwepo nchini.
Na mwanao atalaumu pia
 
Nchi ipo kwenye mstari kuliko wakati wowote ule tangia uhuru. Kama unafikiri nchi ina ombwe la uongozi ingia mtaani uandamane kisha utakuja rejesha majibu kama nchi ina uongozi ama vipi. Mtaleta heshma tu ata kama haupendi na maendeleo ni kila kona mpaka treni za umeme na fly over. Mafisadi wa Chadema Wamepoteana wamebanwa kila kona.

Huyo Mwenyekiti wa Chama Cha Mauaji naye ni wale wale.Kama ana ubavu aseme aliyemtuma ya zile Bilioni nane za Kivuko kibovu.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom