Otorong'ong'o
Platinum Member
- Aug 17, 2011
- 39,131
- 28,589
Dah wadau wa Old Moshi High School mmenikumbusha mbali sana. Nakumbuka those years early 90s tukiwa O level kulikuwa na headmaster aliyeitwa Mtui (RIP). KJJ Mtui alikuwa bomba sana alikuwa akihutubia school assembly anamaliza na slogan yake ya Love your school, love one another.
Kwa wale wanaokwenda pale A level ukiwa serious utafaulu vyema kwani mazingira ni rafiki hakuna wa kukufuatilia na jua wajibu wako. Nawakumbuka walimu wa A-Level ( Chemistry- Mama Samanya, Mama Mlingi na Ngwinya) Biology kulikuwa na Mama Kimaro (RIP) Mama Rutazaa, Physics -Shayo na Maths- Kinunda duh dogo anavuta fegi kama kapagawa. Kuna walimu wengine O level nawakumbuka Lisapita, Kimbi Mzee wa French. Yaani nikikumbuka "Ongoza vema Angaza" nasisimka.
Mkuu mama Samanya bado yupo ati!!! Ila Kimbi naona alikuwa promoted akaja kuwa ticha wa Adv Chemistry....Ila alienda kupiga Master yake hapo Udsm sijui kasepa wapi......
.
Mkuu vp kuhusiana na kuruhusu uvaaji wa nguo za nyumbani shulen hapo???? Na je simu zinaruhusiwa ??? ........na ratiba ya msosi je???? Nisaidie mkuu!
Mkuu mama Samanya bado yupo ati!!! Ila Kimbi naona alikuwa promoted akaja kuwa ticha wa Adv Chemistry....Ila alienda kupiga Master yake hapo Udsm sijui kasepa wapi......
Vipi wewe ....? Unata kusoma au konesha fashion show hapo shuleni...? Au una maanisha nn unaposema nguo za nyumbani zinaruhusiwa....?
Kijana ukifika shuleni siku ya orientation utapewa sheria za shule ambazo utatakiwa kuwa abide kuzifuata...Kwenye sheria za shule hakuna kipengele kinacho ainisha mwanafinzi awe na simu shuleni na pia mavazi ambayo unatakiwa kuwa nayo pia yameainishwa kwenye Joining Instruction utakayo tumiwa....
Halafu kumbuka Waziri wa Elimu alitoa onyo kali kuhusu wanafunzi kumiliki simu za mkononi.....Kama wewe ni mfuatiliaji mzuri wa taarifa za habari utakuwa umenielewa.....
Mkuu hapo umeenda kusoma na sio mambo mengine..Ukifanya mchezo utatoka na aibu kubwa sana...
mwambie mkuu, pale kama huna nidhamu binafsi hakuna muda wa mtu kuanza kukufuatilia. Unaweza ukaingilia geti kubwa linalotazamana na ccp kisha ukaacha one yako then ukatokea geti dogo la kupitia ushirika bila hata four.
Kama huwezi kujimonitor mwenyewe, wewe si kuku wa kienyeji usijaribu kwenda pale
nilitoka hapo 2009, na mwaka jana mwishoni nilipitia gamba langu, mazingira ni yaleyale ila waliongeza michepuo ya arts, kwa sasa h/m anaitwa Angalo aliyekuwa anafundisha physics kinunda still yupo na hajaacha mkawara wake.
Inspecta chami yupo pia
kwa upande wa accademic dogo nikwambie pale ni wewe na akili kichwani, ukitaka kusoma utatoka, ukiwa mpenda starehe hakuna wa kukufuatilia.
Walimu wapo wa kutosha na wanahudhuria vipindi bila kudoji ila hawana time y kumfuatili mwnafunzi kama ameingia darasani au la
pia kuna maabara tatu za physics chemistry na biology na practical ni kila wiki.
"ONGOZA VYEMA ANGAZA"
.
Mkuu vp kuhusiana na kuruhusu uvaaji wa nguo za nyumbani shulen hapo???? Na je simu zinaruhusiwa ??? ........na ratiba ya msosi je???? Nisaidie mkuu!
Mama Samanya......Alikuwa fiti ila lafudhi yake ilikuwa noma sana....Alikuwa yupo fit kwenye practical
Wewe lazma ni somebody siao... Nimeshakujua..
Shule za vilaza hizo , ungesema kibaha,mzumbe,taboraboys na ilboru ningekuelewa
Mbona kwa shule za serikali msosi mzuri tuu huu!!! Kama mtu anataka umaridadi basi aende shule za private. Ila niwatahadharishe tu kuwa shule za private A level si nzuri kama za serikali zile nzuri. Private O level ndiyo nzuri. Kwa mfano mwanao akifaulu kwenda Ilboru, Mzumbe, Kibaha, Old Moshi, na nyingine nzuri za serikali bora umpeleke kama hutakuwa na ubavu wa kumpeleka Feza Boys!!! Kudos shule za serikali miaka ile mlitufikisha hapa tulipo. There were dedicated and intelligent teachers.Ohhh I almost forgotten.....
Kuhusu ratiba ya sosi ni kama ifuatavyo...
Uji ni kila siku saa 12.00 Asubuhi...
Chai ni kila siku saa 4.00 Asubuhi
Jumatatu:
Mchana- Ugali Samaki
Jioni. - Ugali maharage
Jumanne:
Mchana- Ugali nyama
Jioni. - Ugali maharage
Jumatano:
Mchana - Wali Maharage( Siku hii ukitaka kujua shule ina wanafunzi wangapi, basi ni siku muafaka....)
Jioni. - Ugali maharage
Alhamisi:
Mchana- Ugali nyama
Jioni. - Ugali maharage
Ijumaa:
Mchana- Wali maharage( siku special
sana hii)
Jioni- Kama kawaida ugali maharage
Jumamosi:
Mchana- Ugali samaki
Jioni. - Ugali maharage
Jumapili full day ni ugali maharage....
Masomo mema..
Halafu nyie madogo mkienda pale msije mkatuangusha manake Old boys waliotoka pale ni vichwa sana. Kuna Engeneers, Drs, Wahasibu, Wanasheria na wanazuoni waliobobea walipita pale. Unaweza kutoa mfano wa Ma Engeneer, Drs, Lawyers waliopita pale. Mh Cleopa Msuya alisoma Old Moshi,.....