Kuna nini nyuma ya pazia?

nyumbatatu

JF-Expert Member
Jul 19, 2013
1,076
938
Salaam wanajamvi!

Tumemalizana na kibwagizo cha Taifa kuhusu NIDA na usajili wa laini za simu kwa alama za vidole bila laini hata moja kufungiwa pamoja na makelele yote na vitisho kutoka kwa wenye mamlaka.

Binafsi sijawahi kujua uhusiano mahsusi uliopo kati ya simu yangu na kitambulisho changu cha Taifa zaidi ya utaratibu wa kawaida wa kujulikana utambulisho wangu kama nilivyokuwa natumia passport/kitambulisho cha kura/leseni ya udereva/kitambulisho cha ajira.

Lakini katika nchi yetu kumekuwa na kawaida "ikitokea makosa ya kiutendaji au kashfa kubwa kwa watunga sera wetu basi kuna kitu kitatengenezwa kuwa habari na mjadala mkubwa " rejea Dr. Shika na 900 itapendeza yake na Babu Mwaisapile na kikombe chake.

Sasa baada ya NIDA/usajili wa simu kwa alama za vidole kufanywa habari kuu ya Taifa na kusababisha taharuki nchi nzima halafu hakuna simu iliyozimwa ni nini kimepita/pitishwa nyuma ya pazia wakati wananchi wote tunaimbishwa wimbo mmoja wa NIDA! NIDA! NIDA!

Wenye vibatari wafanye kuwasha tuondokane na hili giza kabla hatujazingwa tena na pafomansi ya ndugu yetu Mbwana Samatta huko ipielo.

Nawasilisha.

20200121_185853.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom