Kuna nini nyuma ya huu mpango?

He he he, siku hizi ukitwaanga chuya hazitoki badala yale mchele unabadikila kuwa chuya, khah!
 
Yaani akilipata tu hilo tumbo atakuja kutemea mate hapo kwa mkeo na kumjulisha hadi gesti uliyobandikia mimba. Stuka aisee. Yeye mwenyewe hajiogopi? Manake ningekuwa mie hadi iq test ingekuhusu kabla ya kuomba mbegu.
 
umeoa halafu bado unapelekeshwa na kutongozwa??????.

siku hizi watu wengi wanaoa tu ili kutimiza wajibu,lakini kiuhalisia bado hawajakomaa kiakili.sasa kama huyu mleta mada,angekua ni mtu aliyekomaa kifikra hili suala lake la kipuuzi asingelileta hapa,ni suala ambalo alitakiwa alimalze mwenyewe..lakin ndo vile akili yake iko empty,na sidhani kama kweli huyu ni baba mwenye mke na watoto wawili!
 
Nimefahamiana na dada mmoja,
Kila siku akawa ananitumia ujumbe mfupi kwenye simu yangu, i miss u, nikadhani kawaida. Baadaye akanitafuta facebook, Jambo moja alilogundua bila hata kuniuliza, nina watoto wawili ambao picha zao nimeweka facebook. Jana jioni akanitumia msg, kumbe una watoto wawili? nikajibu ndiyo.

Baadaye akanitumia message kuwa ana ombi moja kwangu. Nikadadisi ni ombi gani hilo? Akasema nataka mtoto unizalie, kama niko tayari tukapime then nimpe ujauzito basi, nikamwambia nina familia, akasema hataki ndoa, wala hataki mimi nimlee mtoto, anachotaka ni mimba tuuu. Kilichonishangaza hatujajadili mambo ya mapenzi, hatujajadili mambo ya kusema "i love you" sasa from "i miss you" to "nataka unipe mtoto" imenishangaza kidogo.

Nimeshindwa kumjibu lolote, kwani kuna agenda gani nyuma ya pazia?
Nimemhoji kwani huna mume? akasema ana mchumba lakini kwa kuwa hajamuoa bado, yeye ana maamuzi yake mwenyewe na maisha yake na haingiliwi na mtu.

Leo asubuhi nimefungua facebook, nimekuta ameweka comment kwenye picha za watoto wangu "hongera sana kwa watoto wazuri sana.."

Nimeshindwa kumwelewa, anataka kunitega kwa mimba ili baadaye avuruge ndoa yangu? au amevutiwa sana na watoto wangu kiasi cha yeye kutamani kuwa na watoto kama wangu, na hatima yake ni nini?


Mkuu hayo ni majanga. Tupa kuleeeeeeeeeeeee kisha umtunze mkeo na watoto wako. Inawezekana huyo ni changu hakudai humdai kwa nini akuumize kichwa kiasi hicho? Again tupa kuleeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee.......
 
simple issue kama hiyo gonga tembea {kama wewe malaya}, kama mcha mungu mpe vipengele na kama wewe kama sisi act ukorofi kwishney
 
Mwanaume na wewe umekuwa domo zege au. ungekuwa mwanamke kama mnavyotusemaga wangekuwa waita kwa shingo tu. mwambie humtaki hata bure full stop.
 
SIPIYU30, jihoji mwenyewe, uone kama ni busara kumpa mimba mtu kirahisi kama ng'ombe wa mbegu wanavyofanyiwa! Na pia angalia kama unaipenda familia yako vilivyo na upo tayari kuisaliti kupitia kwa huyo dada 'usiyemjua'. Nitashangaa sana kama utaona kumsaidia huyo dada usiyemjua ni kitu chema zaidi kuliko heshima yako, ya familia yako na ndoa yako kwa ujumla achilia ,mbali kama lengo lake ni kukuhaibia maisha au laa!
 
we nenda kamuulize mke wako kama atakubali sawa, sidhani km sisi tuna ya ziada wakati umeshaoa na una akili zako timamu......ungekuwa mbele yangu ningekutemea mate usoni
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom