Kuna nini kwenye kifo, Je ukifa unaenda wapi?

Zero IQ

JF-Expert Member
Dec 21, 2016
13,917
24,674
Kuna maswali mengi sana wanadamu tunajiuliza mengine yana majibu na mengine yanakosa majibu sana sana maswali yale ya kiimani zaidi.

KIFO _Kuna maandiko yanasema kila kilicho na Uhai basi siku zake za kuishi zinaesabika hapo haijarishi ni binadamu,Mmea au mnyama basi chochote chenye uhai ni lazima kife na hapo ndio tunapata neno kifo.

Kifo kililetwa na nani? Na kwa nini kuna kifo? na baada ya kifo kile kilichokufa kinaenda wapi? kuna siri gani kwenye kifo?

Hayo ni baadhi ya maswali ambayo ukiuliza baadhi ya wanazuoni kila mmoja atakupa jibu lake hii ina maana hakuna jibu la moja kwa moja kuhusu kifo,

Lakini leo tujadili Swali hili ,

Je Ukifa unaenda wapi?

Ukija kwenye imani za dini wanasema kinachokufa ni mwili lakini Roho inabaki hai na hiyo uchukuliwa mpaka mbinguni ambako kuna hukumu kama ulitenda mema basi Roho yako itaingia kwenye Raha ya milele ila kama ulitenda Dhambi Roho yako itatupwa Motoni.

Lakini pia ukija kwenye upande wa wale wasio na imani watakujibu kwamba kifo hakitenganishi Mwili na Roho bali ukifa Umekufa hakuna kingine kinachoendelea juu yako.

Kutokana na majibu hayo hapo juu hauwezi kujua yupi yuko sahihi kwa sababu hakuna ithibati iliyowahi kusibitisha kwamba kuna maisha mengine baada ya kifo.

Nami nisiwakatishe Tamaa au kuwaingiza uoga mioyoni mwenu ila Kifo hakina budi kuheshimiwa kwa sababu kila aliye na uhai ni lazima atakufa tu.

Ukitaka kujua ukifa unaenda wapi basi jaribu kufikiria kabla ya kuzaliwa kwako wewe ulikuwa wapi?

Na ndivyo hivyo Kifo kitakavyokuwa baada ya kifo Chako.

_Jf Mtawangu.
 
Ukifa unarudi mavumbini ulipotoka na pumzi ya Mungu aliyokupulizia puani ili uwe nafsi hai inamrudia yeye hii pumzi haina utambuzi wowote

Kwa kifupi tu ukifa unabaki kaburini mpk marejeo ya Kristo mara ya pili
 
Kifo ni chanzo sio mchakato... Death is the state not the process...
Nashindwa kufika kwenye uzi wako sijajua tatizo lipo kwenye link au lah lakini niulize tu swali kutokana na title ya uzi wako unaosema Sanaa ya Kifo.

Kama kifo ni sanaa ni kwa nini wale waliokufa parmanent wanashindwa kuitumia sanaa hiyo hiyo ya kifo kurudi tena na kuwa hai.?
 
Ukifa unarudi mavumbini ulipotoka na pumzi ya Mungu aliyokupulizia puani ili uwe nafsi hai unamrudia yeye hii pumzi haina utambuzi wowote

Kwa kifupi tu ukifa unabaki kaburini mpk marejeo ya Kristo mara ya pili
Kumbuka kwamba ukifa ni lazima utaoza hautabaki kama ulivyo je hiyo pumzi inayochukuliwa na wewe kubaki pale kaburini mpka siku ya ufufuo inavyosema itamkuta nani na wakati mpka kipindi hicho kifike wewe utakuwa tayari umefutika mpaka mifupa iliyo katika mwili wako.?
 
Nashindwa kufika kwenye uzi wako sijajua tatizo lipo kwenye link au lah lakini niulize tu swali kutokana na title ya uzi wako unaosema Sanaa ya Kifo.

Kama kifo ni sanaa ni kwa nini wale waliokufa parmanent wanashindwa kuitumia sanaa hiyo hiyo ya kifo kurudi tena na kuwa hai.?
Hebu ipate kupitia Google nitakutag pia kisha ukishaisoma turejee hapa kwa mjadala
 
UKIFA CONSCIOUS YAKO INATOKA KATIKA MWILI INAENDA ULIMWENGU WA ROHO NURUNI(RAHANI) AU GIZANI(KUZIMU), RAHANI= AMANI TIMILIFU,SHIBE TIMILIFU, AFYA TIMILIVU, KUPENDWA TIMILIFU,KUPENDA TIMILIFU, TIMELESS, UTIMILIFU WA KILA NAMNA GIZANI NIKINYUME CHA RAHANI
 
Kumbuka kwamba ukifa ni lazima utaoza hautabaki kama ulivyo je hiyo pumzi inayochukuliwa na wewe kubaki pale kaburini mpka siku ya ufufuo inavyosema itamkuta nani na wakati mpka kipindi hicho kifike wewe utakuwa tayari umefutika mpaka mifupa iliyo katika mwili wako.?
Wakati Mungu anamuumba mwanadamu alitumia mavumbi ya ardhi lakini hakuwa nafsi hai mpaka alipopuliza pumzi ya uhai

Kwa hiyo mwanadamu hai ni muunganiko wa mavumbi ya ardhi plus pumzi ya Mungu

Sasa kujibu swali lako atakaporudi Kristo atahuisha tena mwili wako ambao utakuwa umedecay kwa kurudi katika hali yake ya mavumbini ulipotoka kwa kukupa pumzi ya uhai kwa hiyo kule kuoza ni hali ya kurudi ulipotoka Mkuu
 
Na vipi kuhusu wale walioliwa na wanyama wakati wa kifo chao je hiyo Pumzi ya Uzima itaurudia mwili upi?
 
Hebu ipate kupitia Google nitakutag pia kisha ukishaisoma turejee hapa kwa mjadala
Done mkuu nimeisoma vyema kabisa lakini mkuu katika mada yako nzima umejikita kuelezea safari ya kifo na nini hutokea baada ya kifo ,

Ushahidi wako ulidili sana kwenye mambo ya kiimani ukiusisha ile dini ya kishetani,budha,na imani zingine lakini umesahau kuleta na ushahidi wa kisayansi pamoja na wale wasioamini katika Imani kwamba nao wamekiri maisha au safari mpya inaanza baada ya kifo.

Bado nasema hakuna Ushahidi wa moja kwa moja kuhusu Kifo kwa sababu hakuna mfu aliyerudi na kuja kutoa ushuhuda wa kile kinachoendelea mara tu baada ya kifo bali ni ushahidi wa theories mbali mbali zilizokusanywa kutoka kwenye imani za watu ambazo hazina ukweli wala ithibati ya uhakika.
 
Ukifa unarudi mavumbini ulipotoka na pumzi ya Mungu aliyokupulizia puani ili uwe nafsi hai inamrudia yeye hii pumzi haina utambuzi wowote

Kwa kifupi tu ukifa unabaki kaburini mpk marejeo ya Kristo mara ya pili
upuuzi,yesu harudi sababu hajawahi kwenda popote
ni utunzi wa wazungu tu,hivi kwa nini hamuelewi!!!!!!

even if we assume he existed,he was a famous liar too
mathew 16:28
"Truly I tell you, some who are standing here will not taste death before they see the Son of Man coming in his kingdom."
 
UKIFA CONSCIOUS YAKO INATOKA KATIKA MWILI INAENDA ULIMWENGU WA ROHO NURUNI(RAHANI) AU GIZANI(KUZIMU), RAHANI= AMANI TIMILIFU,SHIBE TIMILIFU, AFYA TIMILIVU, KUPENDWA TIMILIFU,KUPENDA TIMILIFU, TIMELESS, UTIMILIFU WA KILA NAMNA GIZANI NIKINYUME CHA RAHANI
nani alikwambia haya?
 
Na vipi kuhusu wale walioliwa na wanyama wakati wa kifo chao je hiyo Pumzi ya Uzima itaurudia mwili upi?
Siyo hao tu bali hata wale waliofia baharini, waliokufa kwa ajali za moto wote hawa wakati wa mwisho watarejeshewa uhai aidha katika ufufuo wa kwanza wa wenye haki au ule wa pili wa watenda maovu
 
Miili yao itapatikana wapi au watapewa miili mipya?
 
upuuzi,yesu harudi sababu hajawahi kwenda popote
ni utunzi wa wazungu tu,hivi kwa nini hamuelewi!!!!!!

even if we assume he existed,he was a famous liar too
mathew 16:28
"Truly I tell you, some who are standing here will not taste death before they see the Son of Man coming in his kingdom."
Hayo uyasemayo ni yale uliyoichagua kuamini mkuu Ila mimi ninaamini Kristo alikuja duniani akaishi na kuitimiza kazi ya ukombozi kisha kupaa mbinguni na baadaye tena atarudi kuja kuwachukua watakatifu wake kama alivyoahidi katika Yohana 14

YN. :14:3
Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo.
 
Hiyo aya ya mwisho hayo maneno aliyaandika kwa mkono wake au kuna mtu alinukuu baada na kuyaandika mahali?
 
Back
Top Bottom