Kuna mwenye info zozote humu toka MDH kwa nafasi za Data Officer?

lazima ukae

JF-Expert Member
May 15, 2013
789
382
Hawa jamaa walitufanyia usaili wa oral kwa nafasi ya Data Officer hapa Dar na walituhaidi kwamba ukiwa successful basi utapokea simu toka kwao baada ya wiki mbili

Sasa yapata mwezi na kitu hakuna cha simu wala text, kibaya zaidi hata ukimuuliza mwenzako na mwenzako nae akamuuliza mwenzake lakini jibu ni moja tu kwamba kila mtu bado hajapokea simu toka kwao.

Sasa kuna wakati mpaka najiuliza huu usaili ilikua tu ni formality au kitu gani. It's ok kwamba huenda mimi nilifeli huo usaili lakini ndo kila unaemuuliza asema hajapigiwa kweli?

Let's say bado wanafanya maandalizi, walikua na ulazima gani wa kuendesha usaili haraka ilhali wanajua fika kwamba mipango yao bado haijakaa sawa? Mana mpaka unaitisha usaili tafsiri yake ni kwamba kila kitu kipo tayari kuanzia finance na mazingira yote ya kazi unakua umeshaandaa.

Hata serikalini kwenyewe hawana mlolongo mrefu kiasi hiki, Utumishi ukishamaliza kufanya saili zote ndani ya mwezi mmoja baada ya kumaliza kufanya usaili lazima bandiko la watu kuitwa kazini litatoka tena ni ndani ya kipindi cha mwezi mmoja.

Kama kuna mwenye update yoyote humu tunaomba atujuze.

NB:Kama huna cha kuchangia basi soma tu kimya kimya kuliko kuja na kejeli wakati wewe tayari una uhakika na maisha.
 
kua na amani mkuu,hakuna aloitwa kazini mpaka muda huu,kua na subira mambo mazuri yanakuja
 
Back
Top Bottom