Kuna muunganiko gani wa kijasusi kati ya Serikali na Kanisa Katoliki?

JOKA55

Senior Member
Nov 1, 2014
110
74
Heshima kwenu wanajamvi
Napenda kuleta kwenu hii hoja tusaidiane kuelimishana,

Nimesoma na jamaa mmoja kwa sasa ni Padre wa Shirika fulani ndani ya Kanisa Katoliki, huyu bwana kipindi tuko shule hakua mwanadini sana wala hata katika siasa hakuwa mpenzi sana yeye alikua mtu mkimya ila akiamua alikua na vichekesho sana.

Baada ya kumaliza form 6 kila mtu alishangaa kusikia eti jamaa huyu kaenda kusomea upadre, miaka mingi ilipita na jamaa huyu alienda kusoma nchi mbalimbali kwani hilo shirika alilojiunga linafanya kazi karibu dunia nzima. Miaka kama 7 iliyopita huyu jamaa alimaliza masomo yake na kupadrishwa, kama kawaida baadhi ya wanadarasa wake tulikuwepo siku ya upadrisho wake kushuhudi na kushangaa jinsi huyu bwana alivyoamua na kusimamia maamuzi yake ya kuwa mtumishi wa Mungu.

Sasa kitu kinachonishangaza kwa sasa Padre huyu ni mpenzi wa siasa sana na wakati mwingine anafahamu matukio serikalini kana kwamba naye ni mfanyakazi wa serikali. Kwa mfano safari nyingi za viogozi wa serikali anazifahamu kabla na ukifuatilia utakuta ni kweli. Safari za raisi zote anazo kabla hata hazijafika, siri nyingi za serkali anazo, mfano ishu ya Kagame kusarender anaijua vizuri sana. Jinsi Mama Banda alivyokuja kushtuka kuwa ramani zote na mahali silaha za nchi yake zilipo hata zile alizozania ni siri Watz wanazo, kwamba kumbe hata baadhi ya madreva wa malori kwenda nchi za jirani ni watu wa usalama

Biography za viongozi wa serikali ndo basi tena, karibia viogozi wote wa serikali anafahamu makabila yao, sehemu walikosoma, marafiki zao, wengine hata aina ya vinywaji wanavyopendelea. Hapa nilipo ni jiji na vikao vingi vya kiserikali huyu bwana anaitwa, ana safari nyingi na viongozi wa serikali, na baadhi ya mashirika ya kimataifa.

Upande wa kanisani nako ni kati ya Mapadre wanaoaminika ndani ya hilo shirika, na anafanya kazi kama Paroko msaidizi na watu wanampenda sana. Kwa vile ni rafiki yangu wa tangia enzi, tunashirikishana mengi ila nimemuuliza hahusiano yake na serikali na hajawahi kuniambia chochote zaidi ya kucheka.

Pia huku kanisani anawahamu vizuri viongozi wa kanisa hasa maaskofu, walikosoma, wale wanaopenda hela, wanaotumia vibaya mali za majimbo yao, wanaoliwa kwa kucheza bahati na sibu huko ulaya kwa tamaa za hela.
Wanaopenda wanawake, wenye roho nzuri, wenye ukabila, wenye ukanda.
Pia anawafahamu maaskofu walioko kwa ajili ya kanisa na walioko kwa ajili ya masliahi yao na makabila yao.

Swali langu kwenu ni hili, kuna muunganiko gani? Je huyu jamaa anatumiwa na serikali kutoa siri za kanisa au anatumiwa na kanisa kutoa siri za serikali?

Karibuni
 
Uhusiano wa kanisa katolik na Serikali za Dunia hii ni mkubwa sana tu...hata kihistoria ukiangalia zamani hapakuwa na demacation kati ya kanisa katoliki na serikali za nchi za ulaya!Pope aliogopewa na kuheshimiwa sana na wafalme na watawala mpaka Jessuits walipokuja na utaratibu mpya kabisa wa kiutawala...But as of now Papa ni mtu anayeheshimika sana na viongozi wa mataifa yote...Infact hata hapa Tanzania nadhani unaliona hili..Maaskofu wana sauti sana hata kwa mambo ambayo sii ya kiroho...
 
kiongozi wa kanisa katoliki ndiye mkuu wa viongozi wa nchi zote duniani zilizopo ndani ya umoja wa mataifa..
japo humtumia sana mmarekani katika mambo yake. ingia goole tafuta zaidi maana hata tutaonekana kunachafua kanisa japo ndio ukweli.
 
Kuna Muunganiko fulani ambao unakua siri ya nchi hasa kwenye mambo ya kijasusi.

Nakumbuka miaka ya nyuma enzi za utawala wa mwalimu Kiongozi mkuu wa kanisa Katoliki hapa nchini alikua anaingia mpaka kwenye vikao vya baraza la mawaziri, na hii ilikua wazi kabisa mpaka pale wapiga kelele walipopiga kelele zao.

Kimsingi uhusiano upo ila ni ngumu kuuelezea kwa kuwa "ni siri ya nchi"
 
Huwezi kutenganisha serikali na kanisa katoliki, hebu ona hata hapa kwetu kanisa Kstoliki lilivyo na nguvu... kwa kugusia tu hata Cardinal Pengo anafanya kazi zote mbili, ya Kitume na ya Kaisali!

Dunia ya sasa isingekuwa hivi ilivyo sasa kiutawala pasipo mchango wa Katoliki! Ndio maana Pope anaheshimika dunia nzima, hata Middle East ambako ukiristo ni less than 10% bado ana sauti kubwa kwao!
 
middle east muongo hana sauti Obama itakuwa papa papa hana sauti dunian kote ila n kwaabadhi ya nchi e.g saudia Iraq Yemen Qatar na zngne km Sudan papa atawambia nn pia papa hawez kuipangia Tz jinsi ya kuish nyerere alkkuwa amejarbu kulitia kanisa ndani ya chama na kuwapa pesaza walipa kodi lkn watu now wamesoma sio wajinga kupiga kelele mengi yamepungua ndomana znz wanasema na bara pia kirefu.cha CCM n Catholic Church Movement..... lkn me nakataa n nyerere tu kulingiza kanisa ila kumbukeni uhuru wa nchi hii haukupiganiwa na nyerere wala wakristo Bali waislam na nyerere aliitwa tu na baadae kuwauwa wengne na kuwaweka vizuizini lkn na yeye kashaonja mauti ladha yake
 
Waislamu wakilalamikia mfumo kristo na MoU huwa tunawaponda na kuwatukana saaaana. Ni kweli there are second class citizens in our own country..
Nchi haiwezi kuwa na amani mpaka itendeke haki na ionekane inatendeka. Otherwise the oppressed group has the right ya kufurukuta na kupiga kelele, kupigania haki yao..
Tuwe wakweli na tupunguze unafiki!! Because this is the reality!!
 
middle east muongo hana sauti Obama itakuwa papa papa hana sauti dunian kote ila n kwaabadhi ya nchi e.g saudia Iraq Yemen Qatar na zngne km Sudan papa atawambia nn pia papa hawez kuipangia Tz jinsi ya kuish nyerere alkkuwa amejarbu kulitia kanisa ndani ya chama na kuwapa pesaza walipa kodi lkn watu now wamesoma sio wajinga kupiga kelele mengi yamepungua ndomana znz wanasema na bara pia kirefu.cha CCM n Catholic Church Movement..... lkn me nakataa n nyerere tu kulingiza kanisa ila kumbukeni uhuru wa nchi hii haukupiganiwa na nyerere wala wakristo Bali waislam na nyerere aliitwa tu na baadae kuwauwa wengne na kuwaweka vizuizini lkn na yeye kashaonja mauti ladha yake

Kama unadhani umesoma, basi hujaelimika. Kasome tena. Hizo nchi za arabuni ulizozitaja ni vijidagaa tu mbele ya mamlaka ya papa. Fanya uchunguzi huru ndipo utajifunza jambo.
 
Kanisa limeshaweka mfumo imara wa kulinda maslahi yake tangu siku za mwanzo...
Ndo maana inakuwa ngumu kutenganisha shughuli za serikali na za kanisa kwasababu serikali lazima iguse maslahi ya kanisa kwa namna moja au nyingine...
 
middle east muongo hana sauti Obama itakuwa papa papa hana sauti dunian kote ila n kwaabadhi ya nchi e.g saudia Iraq Yemen Qatar na zngne km Sudan papa atawambia nn pia papa hawez kuipangia Tz jinsi ya kuish nyerere alkkuwa amejarbu kulitia kanisa ndani ya chama na kuwapa pesaza walipa kodi lkn watu now wamesoma sio wajinga kupiga kelele mengi yamepungua ndomana znz wanasema na bara pia kirefu.cha CCM n Catholic Church Movement..... lkn me nakataa n nyerere tu kulingiza kanisa ila kumbukeni uhuru wa nchi hii haukupiganiwa na nyerere wala wakristo Bali waislam na nyerere aliitwa tu na baadae kuwauwa wengne na kuwaweka vizuizini lkn na yeye kashaonja mauti ladha yake

Sentensi za chuki na hasira huku zikiwa nje ya mada.

Kwa mtizamo wangu.

Serikali na dini ni kama sarafu moja yenye pande mbili, zote zipo kwa ajili ya makundi ya watu ili kupata faida.
mfano, huwezi tenganisha mamlaka ya papa na utawala wake juu ya NCHI ya Vatican.
Papa ni kiongozi wa kidini na vivyo hivyo ni rais au tuseme mtawala wa nchi,
hapo tunapata maana kwamba viongozi wengi wa kidini wana fursa/tamaa/malengo ya kuongoza nchi au eneo husika.

lakini ukiangalia asili za dini zetu nyingi za sasa zipo kwa maslahi binafsi zaidi.
Hivyo ili wahusika wa dini hizo kupata maslahi hayo ni lazima kucombine nguvu zao na za watawala wa kimwili.

Mtawala wa kiroho akiungana na mtawala wa kimwili, nadhani waweza kadiria matokeo.

so it is not a coincidence, it is/was planned
 
middle east muongo hana sauti Obama itakuwa papa papa hana sauti dunian kote ila n kwaabadhi ya nchi e.g saudia Iraq Yemen Qatar na zngne km Sudan papa atawambia nn pia papa hawez kuipangia Tz jinsi ya kuish nyerere alkkuwa amejarbu kulitia kanisa ndani ya chama na kuwapa pesaza walipa kodi lkn watu now wamesoma sio wajinga kupiga kelele mengi yamepungua ndomana znz wanasema na bara pia kirefu.cha CCM n Catholic Church Movement..... lkn me nakataa n nyerere tu kulingiza kanisa ila kumbukeni uhuru wa nchi hii haukupiganiwa na nyerere wala wakristo Bali waislam na nyerere aliitwa tu na baadae kuwauwa wengne na kuwaweka vizuizini lkn na yeye kashaonja mauti ladha yake

Naomba tujikumbushe kidogo historia. Wamisionari walikwenda sehemu mbalimbalimbali duniani kutangaza neno la mungu na wakati huohuo kutengeneza njia kwa watawala wa nchi zao kuweza kupata maslahi ya kiuchumi na ndiyo mwanzo wa ukoloni. Vile uislam ulienea duniani katika harakati za kufanya biashara tena hata biashara ya binadamu iliyomfanya binadamu mwafrika kuwa na thamani ya shanga.. Ukoloni umebadili sura ns kuwa ukolonimamboleo na biashara ya utumwa imeisha ikabakia hali ya ukibaraka. Waafrika tumebaki tunauguza majeraha ya kubaguana, kudharauliana na kuisahau asili yetu. Tunajidhalilisha tunaposhindwa kupambanua mazuri na mabaya yaliyoletwa na wageni tukayachukua yale ambayo yatatuunganisha badala yake tunakumbatia yale ambayo yatazidi kututenganisha. Hivi tunagikiri kabla ya uislam naukristo kuja afrika waafrika hawakuwa wanamwamini mungu?
 
Mkuu barikiwa kwanza

Ukweli kwa tanzania ubaguzi haukuwepo we jiulize kwa nini waislam walimpa mkristo nchi tena wao ndio walimchangia nauli kwenda ulaya huu ubaguzi umeanza lini.

Kipindi cha harakati za kudai uhuru kanisa lilikua mbali sana na harakati hizi sababu ilikua ni usaliti kudai uhuru kwa wazungu ambao ndio wakuu wa makanisa na ni watawala ivyo waislamu show ikawahusu kwa % .

Lakini haya yote haya baada ya mtu kushika hatamu akaanza kuwaona firigisi waislam firigisi wale waliokuwa watumishi wa wazungu na kujitenga na harakati za uhuru ndio wakapewa shavu kuwa karibu na serikali rejea katika kitabu cha KANISA KATOLIKI NA SIASA ZA TANZANIA BARA (mtunzi nimemsahau kidogo) waislam walikua na chombo chao cha Afrika mashariki nani alikivunja na kuiweka BAKWATA?

Waislamu walitiwa vizuizini bila sababu za msingi wengine kuuliwa kutokana na uchochezi tu wa makanisa. Hapa ndipo kubaguana kulipoanza na hawa watu mpaka leo hawataki kuungana angalia kiwete alivyotaka kujalibu kuweka mambo sawa ili tusipunjane nini kimemkuta? Wema wake wote anaonekana hafai mbele ya jamii.

Ukweli hawa jamaa walijikita mizizi kupitia serikali na walizoea kuinyonya nchi hii na ndio wamefanya tuwe maskini mpaka leo na hawataki kuiachia nchi hii baada ya kuona CCM ya JK imewanawa wameingia upinzani na wanataka kuturudisha kulekule.

Hili halitowezekana na huu ndio ukweli utaki kaandamane.
 
Huyu ni pandikizi tuu hakuna kingine mbona hata mashekh wa dizaini ya huyo padri wapi mfano shekh mkuu wa Mkoa huu
 
Back
Top Bottom