LICHADI
JF-Expert Member
- Feb 4, 2015
- 4,146
- 11,192
Gaidi nnaemuongelea mimi sio mlipuaji mabomu au muuwaji bali ni mtu mwenye roho ngumu pale ambapo anahitaji kufanya mambo yake ili afanikiwe.
Mada hii inagusa hasa Graduates ambao ndio wanaanza maisha baada ya kupata ajira au kijana yoyote anaeanza maisha ya kuingiza kipato ni lazima uwe na roho ngumu kweli kweli hasa kwa ndugu wanaopenda kuwa tegemezi kwa mtu anayeanza kufanya kazi.
Ukiendekeza ndugu utakuja kujikuta hujapiga maendeleo yoyote hata kiwanja hujanunua, alafu ukija kupoteza kazi huenda hao hao ndugu ndio watakao anza kukucheka kuwa umepoteza kazi na haukuwahi kufanya maendeleo yoyote, saidia ndugu kwa kiasi tu na sio kutoa akiba yote, hautopiga hatua yoyote.
Sio kila tatizo likitokea nyumbani we ndio wa kwanza kutoa hela, mda mwingine jifanye una hali ngumu kwani haukuzaliwa peke yako kusaidia ukoo mzima.
Pale unapopata kazi ndio mda wa kuwa kama gaidi kweli kweli ili ufanye maendeleo yako haraka kabla hujaowa, Yani hao ndugu inabidi uweke kizibo masikioni kwa muda.
kwasababu ukija kuwa na mke na watoto kama haukufanya maendeleo mapema kipindi ambacho upo single, utakuja kujutia na endapo utakuja kuowa mwanamke asiyejishuhulisha au anaefanya kazi lakini ni mbinafsi ndio utajuta kwa nini haukujenga mapema na hao ndugu uliokuwa unawasaidia ndio watakuwa wa kwanza kukucheka.