Kuna mtu anataka kunitapeli naomba msaada

Tafuta laki 1..nenda kachukue wahuni chang'ombe...anataitishwa mpaka akili imkae sawa...na hela anatoa
 
Unapoanza biashara hutakiwi kuingia kwa kutanguliza kichwa namna hiyo.
Unapoanza biashara hutakiwi kukurupuka.

Na mpaka hatua hiyo sidhani kama hata una idea yoyote kuhusu biashara yaani uko empty kwenye biashara hivyo nakushauri anza kusoma vitabu vya biashara kwa muda ili ukianza tena kuingia kwenye ulimwengu wa biashara ufanye biashara kama professional hata kama sio mtaji mkubwa.

Yaani uanzishe biashara.
Ujue kwanini umeianzisha.
Kwanini uchague hiyo biashara.
Watu wa aina gani utakaohudumia.
Eneo utakalo fanyia biashara.
Kuza biashara na uboreshe.
Simamisha biashara na ijitegemee.
Then anza kula matunda ya biashara na kuongeza biashara nyingine sehemu mbalimbali bila kukiuka chochote hapo juu.

Na sio ufanye biashara kama machinga ili apate pesa ya kula.

Kwa huo mtaji wako kulikuwa na uwezekano wa asilimia 76% wa kurudisha 100k to 50k per day kama usingekirupuka na kufanya ambacho kila mtu anafanya (wazazi wako).
 
duh biashara ya kuoza angefanyaje?
Alipaswa afanye research ya kutosha kabla ya kwenda kupeleka mzigo lazima ujue soko na nani utamuuzia na ujue unapataje faida, uzembe mdogo tu kwenye biashara unapata hasara kubwa sana, biashara unatakiwa uchukulie serious umemwaga mtaji wote humo then huchukui tahadhari
 
Huyu mtu anafanya biashara na watu ambao nawafahamu nakuna mmoja alitoka huko ndo akaniambia nenda ila nilikuwa nasafarisha songea
Kosa la kwanza ni hili.

Hutakiwi kufanya ambacho kila mtu anafanya bali kuwa mbunifu wa aina yako. Kuna vitu vingi vya kufanya tanzania vina thamani kubwa ukiangalia kwa sniper vision.
 
Wale mnaokejeli jamaa hatapata pesa, naimani mpaka sasa amepata nusu ya pesa yake na anaendelea na mapambano ya maisha.

Huko kwenye masoko kuna wapinga maendeleo sana, wadhurumaji mno na wakatisha tamaa, mkuu hajaamua kukata tamaa, ameamua kupambana. Safi sana

Pambana jasho lako mpaka mwisho mkuu
 
Pole Sana kijana wangu, madalali wa Dodoma ni matapeli sana na ukiripoti polisi hakuna msaada maana wanajuana nao, sidhani kama utapata pesa yako hapo, siku nyingine biashara peleka popote sio Dodoma hapo wanawezana wenyewe. Kuna binti niliishi naye nyumba moja Dar mwaka juzi kaleta Maembe kayafikishia Sabasaba alitapeliwa mzigo wote wakamwambia ukitaka nenda polisi, akaenda kushtaki akaahidiwa atashughulikiwa kawasubiri polisi hakuwaona siku ya pili asubuhi anamwona polisi wake yupo pale kwenye Maembe kabeba anayoyataka kawekewa kwenye mfuko kaondoka alichofanya binti akazoa Maembe yake akakaa pembeni akauza ili apate nauli akajiondokea zake maana hata guest alihama akahamia kwangu, hao ndio madalali wa Dodoma. Kosa kubwa kuondoka wenzako wanakaa hapo hapo mzigo ukiuzwa anachukua pesa yake hata kama ni rejareja kila asubuhi yupo nao hata wakikutisha wewe huongei wanauza unapokea hela. Madalali wa Masoko Dodoma wanalitia aibu jiji na hawana wasimamizi wa maana
 
Umemchambulia kama CPA (T) kabisa.
 
Polisi hamna msaada maana hio kesi ya mahakaman na hana ushahidi in writings. Cha kufanya labda akam confront mdeni wake akijibu shit akaandikie kesi kwamba kamtishia maisha ndo watamuweka ndani.😂😂😂
 
Mie niko poa best, ya huyo kijana we acha tu!!

Hawa wanaomkejeli natamani kuwapiga makofi... mbaya zaidi wanamkejeli kwa kitu wasichokijua manake wangekuwa wanafahamu biashara za jumla masokoni zinaendeshwaje wala wasingekuwa wanamkejeli!!
Hahahahah imagine umeshusha Fuso ya mzigo halafu baada ya siku 3 dalali analeta usenge. Hio shangazi yangu alishapigwa 16M akatoka from hero to zero. Na alikuwa mzoefu kwenye game wenzake wakapigwa 300M walifanyia biashara Zambia.

Alikuwa anazungusha mtaji wa 20M hapo bado ana marejesho ilifikia stage wanataka kuuza nyumba yake alidata almanusura tumkose. Kaka zake ndio kumpiga piga tuff akakaa sawa.

Hizo biashara za sokoni acheni tu😎 zina michezo ya hatari sana.
 
Pole sana kijana...Fanya ukatoe taarifaa polisi haraka inavyowezekana..
 
Dah nimeshindwa hata kushauri maana ukisema aende polisi, hawakuandikishana hakuna ushahidi wa hiyo biashara. Ukimtafuta mwenyewe anakuzungusha coz anakuchukulia bado dogo. Kiufupi mdogo wangu Chilunde ulifanya koda kubwa sana la kumuamini huho mtu huku ukijua kabisa alishawahi kunzungusha mama ako pia..
Tafuta means nyingine, ila ningekuwa mimi ningempeleka kwa sangoma mshenz huyo😤😤
 
Siyo madalali wa Dodoma tu ila madalali popote pale Tanzania ni watu matapeli. Tanzania dalali ndiye anakuwa na nguvu na mwenye mali anakuwa kama mtumwa. Ni tofauti kabisa na nchi nyingine ambapo madalali wanakuwa waaminifu na wanyenyekevu. Nachojiuliza kila siku: Hivi kwenye biashara zetu ni lazima tutumie madalali? Kwa nini kama unasafirisha maembe usiyatafutie soko wewe mwenyewe? Wengi nadhani watajibu haiwezekani lakini mimi nasema ni uvivu wa watanzania tu kuzoea vya kunyonga. Mimi siku yoyote nitakayopingia kwenye biashara naapa sitatumia dalali. Nitatafuta soko peke yangu na bidhaa ikidoda basi inidodee mimi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…